Nimemtia mimba mzazi mwenzangu akiwa kwenye ndoa yake ya miaka 7. Nifanye nini?

Nimemtia mimba mzazi mwenzangu akiwa kwenye ndoa yake ya miaka 7. Nifanye nini?

Miaka 9 iliyopita nilimtia mimba Mwanachuo wa mwaka wa 2 akajifungua mtoto wa kiume. Hatukuweza kuoana maana na mimi ndiyo kwanza nilikuwa nina mwaka mmoja mtaani sina mbele wala nyuma.

Hivyo kila mtu alishika 50 zake na kutafuta mwenza wake mpya wa maisha. Lakini malezi ya mtoto niliyabeba kama baba.

Yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumpata mwenza wake wa maisha. Alimpata miaka 7 iliyopita na sasa wana watoto 2 ndani ya ndoa yao

Mimi nilichelewa kidogo kwasababu ya kujipanga kimaisha, ndoa yangu ndiyo kwanza ina miaka 2 na nina mtoto wa miezi 7.

Miezi 2 iliyopita nilienda semina mahali fulani. Nikakutana na mzazi mwenzangu naye akiwa ni mshiriki wa semina ile. Kwa kuwa mke wangu ana katoto kachanga ka miezi 7, na kwakuwa huyu mzazi mwenzangu tumekutana mazingira mapya ya semina, na kwakuwa jicho lilimtamani kwa jinsi alivyo nawiri na kustawi basi semina ilienda vizuri.

Juzi nimepigiwa simu na mzazi mwenzangu akidai ana mimba yangu na mumewe amegoma kuikubali.

Sasa mabibi na mabwana, nawauliza suala hili nilishughulikie vipi?
  • Nikubali ama niikatae mimba hii?
  • Nikiikataa itakuwaje endapo mtoto atafanana na mm na mumewe anaijua chapa yangu kupitia mtoto wangu wa kwanza?
  • Je, nikikubali mke wangu patakalika?
Naombeni suluhisho la suala hili pasipo kuvuruga ndoa yangu changa.
Mrejesho ndgu
 
Watu wakipata hofu kuoa wanawake wenye watoto/mtoto huwa ni kwa sababu kama hizi.
 
Watu wakipata hofu kuoa wanawake wenye watoto/mtoto huwa ni kwa sababu kama hizi.
Hakika. Watu wanapasha viporo. Ingawa si wote, hata ambao hawajazaa kabla ya ndpoa nao pia wanabebwa na ma ex wao kama kawa
 
rudi tena kwenye hiyo semina ikifika kipindi cha maswali/maoni omba msaada wa hili jambo watakusaidia tu,sisi hapa hata hatukuoni sio rahisi kukusaidia
 
Wewe ndiye unableed kila ukitaka kufanya mapenzi baada ya kula pesa za watu?
 
Jamanii atuletee mrejesho jeshoo maana huu Uzi toka mwaka Janaa.

Atuambie kama kweli mtoto alifananae...?
Na Je..? Mzazii mwenzie amemuelewaa...?
Na Je. Imeendeleajeee na semina zilizo fwataaaa
 
Mtoa mada kumbe ni Shigongo like, mtunga hadithi tu.

Kaumbuliwa hapa juu for his past posts

Harudi tena hapa kujibu
 
Back
Top Bottom