Nimemtia mimba mzazi mwenzangu akiwa kwenye ndoa yake ya miaka 7. Nifanye nini?

Nimemtia mimba mzazi mwenzangu akiwa kwenye ndoa yake ya miaka 7. Nifanye nini?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
27,705
Reaction score
65,343
Miaka 9 iliyopita nilimtia mimba Mwanachuo wa mwaka wa 2 akajifungua mtoto wa kiume. Hatukuweza kuoana maana na mimi ndiyo kwanza nilikuwa nina mwaka mmoja mtaani sina mbele wala nyuma.

Hivyo kila mtu alishika 50 zake na kutafuta mwenza wake mpya wa maisha. Lakini malezi ya mtoto niliyabeba kama baba.

Yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumpata mwenza wake wa maisha. Alimpata miaka 7 iliyopita na sasa wana watoto 2 ndani ya ndoa yao

Mimi nilichelewa kidogo kwasababu ya kujipanga kimaisha, ndoa yangu ndiyo kwanza ina miaka 2 na nina mtoto wa miezi 7.

Miezi 2 iliyopita nilienda semina mahali fulani. Nikakutana na mzazi mwenzangu naye akiwa ni mshiriki wa semina ile. Kwa kuwa mke wangu ana katoto kachanga ka miezi 7, na kwakuwa huyu mzazi mwenzangu tumekutana mazingira mapya ya semina, na kwakuwa jicho lilimtamani kwa jinsi alivyo nawiri na kustawi basi semina ilienda vizuri.

Juzi nimepigiwa simu na mzazi mwenzangu akidai ana mimba yangu na mumewe amegoma kuikubali.

Sasa mabibi na mabwana, nawauliza suala hili nilishughulikie vipi?
  • Nikubali ama niikatae mimba hii?
  • Nikiikataa itakuwaje endapo mtoto atafanana na mm na mumewe anaijua chapa yangu kupitia mtoto wangu wa kwanza?
  • Je, nikikubali mke wangu patakalika?
Naombeni suluhisho la suala hili pasipo kuvuruga ndoa yangu changa.
 
Mimi nakushauri hivi kama mume wake amemkataa ...basi beba majukumu yako...km baba !! Mtafutie mahali umpangishie ...maana hapo kunachofata lazima uje kuhusishwa katika kesi ya maaji ...unajua mwenzio anawaza nini kwa sasa huko aliko???
 
Mzee limeshatokea ilo wala halihitaji ujanja ujanja.We pambana na hali yako tu na usije thubutu kutoa hiyo mimba kwa sababu kila jambo lina gharama yake, sasa we jipange tu kukabiliana na outcome apo wala hakuna lingine kuliko kumbebesha mwanaume mwingine mtoto asiyehusika nae kwa upuuzi wenu mliofanya
 
Eti mabaharia mnalizungumziaje suala la kuoa mwanamke mwenye mtoto?
tapatalk_1575315463990.jpeg
 
Back
Top Bottom