Nimemuambia wife awe anasuka style hii ya nywele ili ku-save cost, kaishia kunisunya na kunibinulia midomo

Nimemuambia wife awe anasuka style hii ya nywele ili ku-save cost, kaishia kunisunya na kunibinulia midomo

Mimi nimekua navutiwa sana na wanawake wanaosuka nywele za za asili, wanaofunika vichwa vyao na kuvaa nguo zinazo sitiri miili yao, sijawahi kuvutiwa na mwanamke aliesuka nywele za kuunganisha zinasimama kama kajitwishwa ndoo kichwani ukikaa nae karibu ukiangalia ngozi ya kichwa hadi imekua nyekundu kwa kuvutwa vutwa kisa kuunganisha nywele

Alaf unatakiwa uwe mwanaume yani anakusonya unakuja kushtaki jF ilitakiwa umfanye kitu ambacho hata siku nyingine hatarudia kuiinua sauti izidi sauti yako
 
Kwema ndugu zangu watanganyika?
Kutokana na mimi kupitia changamoto za kifedha kwa sasa,nilimuomba Wife tupunguze gharama za uendeshaji wa maisha yetu kwa kujibana sana, pendekezo langu la kwanza nilipendekeza Wife anyoe nywele zake alizosuka,akajitetea kwamba nywele zake katumia karibia miaka 10 kuzifikisha hapo zilipofikia hivyo hatoweza kuzinyoa na akaongezea kuwa akinyoa yeye huwa ana kichwa kibaya hivyo hatokua comfortable.
Basi mimi nikajaribu kupitia kwenye baadhi ya pages za wadada wenye saloon huko Instagram nikaja na pendekezo moja kuwa Wife awe anasuka style flani hivi ya nywele ambayo ni affordable kwani ni elfu 5 tu.ila mwenzangu nilipomshirikisha hivyo akaishia kunisunya na kunibinulia midomo kuwa hayuko tayari.
mpaka sasa kaninunia.ila mimi msimamo wangu uko pale pale sitotoa zaidi ya elfu 5 ya kusukia.
Asanteni

View attachment 2044854
Sijui kwanini lakini wanawake wanaosuka wapo sensitive sana kwenye suala la nywele zao. Mimi pia mpenzi wangu alikataaga kubadilisha mtindo wa kusuka ili kusave garama, yupo radhi asile ila asuke vizuri
 
Hiyo kwangu safi sana, hiyo 5k naiweka kwa miezi mitatu ifike 15k ndo niende saluni ku repair dreads zangu..na nisivyopenda kuvutwavutwa kichwa!! In the mean time utaishi na chizi fresh kwa miezi mitatu.
(NB: sikubaliani kuwa nywele zetu ni kama machizi)

Picha:google
images (56).jpeg
 
Hiyo kwangu safi sana, hiyo 5k naiweka kwa miezi mitatu ifike 15k ndo niende saluni ku repair dreads zangu..na nisivyopenda kuvutwavutwa kichwa!! In the mean time utaishi na chizi fresh kwa miezi mitatu.
(NB: sikubaliani kuwa nywele zetu ni kama machizi)
View attachment 2044936
Hauna chawa kwel mkuu?
Maana sio kwa huo mzigo kichwani.
 
Ndiyo kusema Ndoa ndoano maana wewe unataka hivi Mke naye anataka hivi.
 
mwache akatae tu kwa kweli

hakuna kitu cha thamani kwa mwanamke kama nywele.

na si ajabu akinyoa ukamchukia tena, ukaona havutii, kawa km mzee

mwisho wa siku unakuja hapa na uzi wa malalamiko, mara ooh mke wangu amekuwa na bichwa km kiberenge...

eb katoe hela ya kusuka kule
 
Hiyo twende kilioni ni buku mbili,shida ya hizi familia ni kupata mtu atakaye kuelewa nywele za miaka kumi unashindwa kuziundia staili mbalimbali ambazo hazitumii gharama?
Binafsi nywele ya mkono siwezi kuisuka nkatembea nayo naona kama kichwa sio changu tena
ila ukiweka wigi ndo unaona chako?? ahahaha wadada asee.
 
ila ukiweka wigi ndo unaona chako?? ahahaha wadada asee.
Sivaagi mawigi nasuka nywele simple but nzuri zisizokera mfano dred hazikeri na sometime nasuka yebo ama nabana mitindo tofauti nywele yangu haina dawa
 
Back
Top Bottom