Nimemuambia wife awe anasuka style hii ya nywele ili ku-save cost, kaishia kunisunya na kunibinulia midomo

Nimemuambia wife awe anasuka style hii ya nywele ili ku-save cost, kaishia kunisunya na kunibinulia midomo

Kwema ndugu zangu watanganyika?
Kutokana na mimi kupitia changamoto za kifedha kwa sasa,nilimuomba Wife tupunguze gharama za uendeshaji wa maisha yetu kwa kujibana sana, pendekezo langu la kwanza nilipendekeza Wife anyoe nywele zake alizosuka,akajitetea kwamba nywele zake katumia karibia miaka 10 kuzifikisha hapo zilipofikia hivyo hatoweza kuzinyoa na akaongezea kuwa akinyoa yeye huwa ana kichwa kibaya hivyo hatokua comfortable.
Basi mimi nikajaribu kupitia kwenye baadhi ya pages za wadada wenye saloon huko Instagram nikaja na pendekezo moja kuwa Wife awe anasuka style flani hivi ya nywele ambayo ni affordable kwani ni elfu 5 tu.ila mwenzangu nilipomshirikisha hivyo akaishia kunisunya na kunibinulia midomo kuwa hayuko tayari.
mpaka sasa kaninunia.ila mimi msimamo wangu uko pale pale sitotoa zaidi ya elfu 5 ya kusukia.
Asanteni

View attachment 2044854
Mpe hela aweke dred inapunguza gharama
 
Mtoa mada uzi unaofwata utakuwa ivi "" MKE WANGU HAOMBI HELA YA KUSUKIA ILA ANASUKA NA KUPENDEZA "[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi kila siku ninanyoa pale ninalipa 25,000 bila kuweka rangi.
Nikiweka rangi 30,000.

Wanaangalia na watu sometimes mi nilikua nanyoa, naweka wave, bleach na hinna nalipa 25,000
 
Juzi wife ananipa bei ya style aliyouliza kwenye page yao nikachoka, naambiwa elfu 70
Nikamwambia atafute mbadala

IMG_6781.jpg

Hizi ndo style za 60k na kuendelea and mind you zinakaa wiki mbili tu [emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom