Nimemuota jirani yangu akiwa chumbani kwangu usiku

Acha Imani potofu, umeshasema ni binti yawezekana unatamani upige mzee, we mtokee tu na ndoto yako itakuwa ya kweli.

You will thank me later
 
Mikopo ya vikoba haijawahi kumwacha mdaiwa salama, hata siku moja. Kawaida, mpaka usingizini huwa wana weweseka tarehe zinapo karibia kuchukuliwa vitu vya ndani (Kitanda, T.V, Godoro, Masufuria, Radio).[emoji23][emoji23][emoji23]

Utawaona watu wengi tu usingizini. Dawa ya deni ni kulipa.
 
Acha imani za kijinga za kishirikina
 
Shinyaga huko mabibi za watu wanuawa sana kwa mapanga kwa upuuzi kama huu,mawazo yako yabkipuuzi unaenda kumsingizia mtu eti kapotea ,hakuna kitu kama hicho ,washirikina lazima wakuunge mkono
 
Wakiwapo wengine waliokumbatia wewe vyumbani mwao katika ndoto zao unaona inavyokuwa tamu?

Rejea kufahamu nini maana ya ndoto kiasi hata ukaota ukamwone mwendazake haitakukusumbua wala kukusukuma kuleta uzi kama huu.
 
Okoka. Mpe Yesu maisha yako ili wachawi waache kukuchezea.

Chagua moja uwe mchawi sana au uwe mchaMungu sana ili uwe salama.

Ushauri wangu kuwa mchaMungu masharti ya uchawi ni magumu hata wao wenyewe wanajuta kwanini waliamua kuwa wachawi.
 
Tufanye utafiti bila maabara?
 
Kama ulishawahi kujiweka kwenye fikla zako kwà namna yoyote basi leo kaja kwenye ndoto. Endelea na mambo mengine

Ila kama hujawahi muwaza hata kidogo basi hapo mtafute Mshana Jr atakusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…