Nimemuota jirani yangu akiwa chumbani kwangu usiku

Nimemuota jirani yangu akiwa chumbani kwangu usiku

Sasa nimeanza kuami JF inapoteza credibility ...Kisa nilichokiwasilisha ni cha kweli na nahitaji msaada ajabu ...nimepitia michango yote na asilimia 95 watu wanechangua utani,masihara kejeli nk!
Inashangaza kidogo kwa Forum kama hii!
pole sana
 
Kwani mshana amesemaje, au nenda kwa ule uzi wa jamii intelligence wa ndoto Kuna reverend kule
 
Ni tukio la kushangaza kidogo.

Majuzi nikiwa usingizini nilimuona jirani yangu akiwa chumbani kwangu ananiangalia akitabasamu! Nilipoamka alitoweka!

Ni binti mmoja ameshika Dini yake kwa mwonekano wa kibinadamu. Nimejaribu kulipuuza tukio hili nichukulie kuwa ilikuwa ni ndoto tu, lakini moyo unakataa kwa sababu nilipoamka nilikuta naweweseka sana.

Naamini hapa nitapata maelezo ya kina ya tukio hili na pengine ushauri muafaka!

Kinachoniuma zaidi siku hiyo sikuvaa chochote na kulikuwa na joto kali kwa hiyo hata shuka sikulihitaji!
Tafsiri ya ndoto ni topic ngumu ngumu sana-Nakuelezea kama mtu mwenye experience kidogo wa mambo haya.Unapaswa kufahamu yafuatayo unapo-deal na ndoto,
-Ndoto huweza kuletwa na MUNGU au shetani.
-Shetana huweza kukuletea ndoto ya mtu ambaye hata hahusiki lengo likiwa ni kuku-manipulate.Devil is a liar always.
-Kuweza kupata tafsiri sahihi ya ndoto ni lazima umshirikishe MWENYEZI MUNGU.
-MUNGU hawezi kukuletea ndoto ambayo hutoweza kupata majibu yake,lazima atakupa na njia ya kuitafsiri pia.
*Watu wengi sana wameletewa ndoto za mama zao wakija kama wachawi-Na wahusika wakaua wazazi wao kwa kutegemea ushahid wa ndoto,kumbe mashini ya MUNGU walidanganywa na mwovu
*Watakatifu wengi zamani walipokuwa wanapata ndoto walikuwa wanakimbilia maongozo ya ki-MUNGU,na kuna ambao Mwenyezi MUNGU aliwaambia kabisa kwamba hizo ndoto hakuwaletea na yeye bali zililetwa na mwovu ili kuwaangamiza.
 
Ubongo wa binadamu una nguvu ya kukupeleka kwenye uhalisia ilihali u ndotoni, sasa ndoto ukichanganya na imani nguvu inayozaliwa si ya mchezo kila kitu kinakuwa ni halisi katika uhalisia wake ila ni ndoto.

Sasa Hapa tayari imani na ubongo umeshakuaminisha kuwa jirani alikuwepo hapo ndani, hata kama ni ndoto tu tayari ww unachotaka kutatua ni suala la jirani kuwepo chumbani kwako.

katika kusaidiwa utamsikiliza atakayekuambia masuala ya ushirikina tu ila sayansi ya mwili wa mwanadamu na tabia za ndoto kisayansi hutaiamini.
 
Mchunguze kwa makini, huenda ni mwanga.
Na inawezekana hata huyo aliyemwona siye mwenyewe-Ndoto inaweza kukukorofisha hata na wazazi mtu usipokuwa makin.Unaweza kukuta kila mara wife akipata mimba inatoka,alafu ndoto inakujia mama mzazi anakulogea wajukuu alafu unachukua maamuzi ya haraka ya kuua mzazi kumbe abortion inasababishwa na kitu kingine tofauti kabisa-Ni hatari sana 🤣 🤣 🤣 .Ndoto nyingine huletwa na mwovu kufitinisha watu
 
Ikitokea umekaona hako kabinti mtaani...

Kaambie next time kakija kuwanga basi kavae nguo, hata dera tu sio mbaya
 
Kama unaishi na mtu nyumbani kwako awe mwanao,Ndugu,mke,mine au mtu yeyote akikuambia jambo kama aliloandika hapa mtoa mada,usimpuuze,fanya utafiti.

Katika utafiti utagundua mengi,na hata kama sio kweli utagundua kua huyo aliokuambia habari Hiyo Ana matatizo makubwa na anahitaji kusaidiwa.

Pengine anaumwa,ameanza kuchanganyikiwa au vinginevyo.

Unaweza kugundua kuwa anafuatwa na wachawi,au wachawi wanaisumbua familia yako na Yeye kapewa nguvu na Mungu ya kuwaona.

Zaidi ya hapo unaweza kugundua Mambo mengine yasiyo ya kawaida.

Watu makini huwa hawadharau kitu.

Na Hiyo ndio akili.
Umenena vema mkuu
 
Salute mkuu mi niliwahi kuchanjia dawa ya kuwaona wachawi mbona inatisha sana,walikuwa wakija chumbani usiku uchi
Mkuu tiririka walikua wanaonekaneje ujue mimi hua siamini sana hii makitu ulikua unaona nini?
 
Sasa nimeanza kuami JF inapoteza credibility ...Kisa nilichokiwasilisha ni cha kweli na nahitaji msaada ajabu ...nimepitia michango yote na asilimia 95 watu wanechangua utani,masihara kejeli nk!
Inashangaza kidogo kwa Forum kama hii!
Ni kama vile kuna majibu unayo tayari kichwani ambayo unatamani kuyapata kutoka kwa wadau, we hiyo ndoto unawaza nini kwani? Kwamba ni mchawi?kwamba amekukula? Au?
 
Hiyo ni ndoto tu. Usipoteze muda na fedha zako kwenda kwa waganga na waganguzi. Ninavyoandika hivi wanakusubiri kwa hamu sana na wanalaumu kwa kuwapeperushia ndege wao. Chukua tahadhari kabla ya hatari.
 
Feedback... Hii kitu haijawi kunitokea tena! Ila huyu Binti bado ni jirani yangu! Tumeendelea kufahamiana , ambapo baadaye niligundua ameolewa .. ndoa za Masafa. Mume yupo mkoa wa mbali!
 
Kama unaishi na mtu nyumbani kwako awe mwanao,Ndugu,mke,mine au mtu yeyote akikuambia jambo kama aliloandika hapa mtoa mada,usimpuuze,fanya utafiti.

Katika utafiti utagundua mengi,na hata kama sio kweli utagundua kua huyo aliokuambia habari Hiyo Ana matatizo makubwa na anahitaji kusaidiwa.

Pengine anaumwa,ameanza kuchanganyikiwa au vinginevyo.

Unaweza kugundua kuwa anafuatwa na wachawi,au wachawi wanaisumbua familia yako na Yeye kapewa nguvu na Mungu ya kuwaona.

Zaidi ya hapo unaweza kugundua Mambo mengine yasiyo ya kawaida.

Watu makini huwa hawadharau kitu.

Na Hiyo ndio akili.
ni nini cha kufanya baada ya kugundua?
 
Back
Top Bottom