Nimemwachia mali zote, naanza upya

Nimemwachia mali zote, naanza upya

Me yamenikuta sana haya mambo, nikaona isiwe shida nikaoa mke wa pili.

Akaanza kulalama ooh utachelewa sana kupata maendeleo nikamwambia sina shida ya hayo maendeleo.

Sasa hv heshima na adabu, tena akiona kesho ni zamu ya mwenzie anatoa show ya kibabe ili nikifika kule nichemke
Mi Mkristo Mkatoliki... Siezi oa tena ...
 
Mkuu usijari kuhusu mali mimi nina baba angu mdogo aliacha kila kitu na akaenda kuanza maisha mbali huko mkoa wa ruvuma na amepambana na sasahv ana maisha mengine tena mazuri zaidi ya yale ya kwanza cha muhimu muombe mungu tuu afya mali hutafutwa tuu...hawa wanawake wa sasa ni wasumbufu sana
Wengi wanalaumu ..ila mwanau akishakudharau... Sio mke ..
 
Stori isiwe ndefu.

Mke wangu mtumishi na mimi mtumishi. Anatiwa ujinga na wenzake kila siku, tuna viwanja viwili na kimoja tumejenga. Leo nimempelekea hati za viwanja vyote na a akae navyo.

Na nimemwambia nakuachia mali zote usiliwe KIZEMBE liwa ukiwa na hamu. Naondoka wasikilize hao marafiki zako. Simu nazopigiwa sio za dunia hii.

Nimeamua kumuachia mali zote, nianze upya. Wanawake Mungu anawaona. Sasa naombwa vikao kusululisha wakati ana nionea kijinsia hakutafuta ndugu. Nimekaa miezi hanipi mzigo kwa ustaarabu sikutaka kumuingilia kinguvu.

Leo namuachia kila kitu nilichopambania ameita familia kutatua na kujadili nirudi kwenye ndoa ambayo hajaihudumu zaidi ya mwaka. Mimi Mkristo Mkatoliki ila huu ujinga sitaki

Nimempa kila kitu nianze upya.
Kwa hiyo unahitaji kupewa msaada gani ?
 
Kauli ya kijinga sana na yenye Udhaifu wa hali ya Juu...

Nani alikuambia huo ujinga ndio urijali....na kufa kisa mwanamke ndio ushujaa..???

Umekuwa MANIPULATED na hawa feminist na ukaaminishwa ujinga,, Grow up
Katika maisha yangu duniani... Nimempiga dada yangu tu.
.... Mke wangu nilimuwamba Kofi sikumpiga....
Akili zikae sawa.... Kwa maisha niliyokulia .. siwezi.. ndio maana nimemwambia ushanizalia watoto watatu wakiume 2 ma kike 1 ... .na ndio MSINGI wa wa kuamuachia Mali zangu...
 
Nakusapoti mkuu. Mi nakaribia mwaka wa pili nilimuachia kila kitu nikaanza upya.
Iko hivi mwaka 2019/2020 ndio nimemaliza chuo nilipanga na mke wangu hapa centa yetu, msimu ukafika nililima mpunga majuruba ya kwetu nusu ekari, kwao tulipewa ekari moja na nusu, tukavuna kama gunia 25, majuruba ya kwao tulipata gunia 18. Nilianza kusimangwa kwa hivyo vigunia kulivyolima kwao.

Ikafika nikawa naambiwa sina lolote, siwezi hata kuajiriwa. Nilichofanya niliuza gunia 7 za mpunga tulizopata kutoka majaruba ya kwetu, vingine vyote nilimwachia, vitu vya ndani, mpunga na gunia za mahindi tano. Nilianza upya sahiv afadhali, yeye akauza mpunga akapewa kiwanja hapohapo kwao akajenga slopu mbili chumba na sebule.

Saa hivi naambiwa tujenge tuwe wamoja hapo alipo amepachoka, maana alipojenga kuna mkubwa wake pia single mother na watoto watano, jumlisha kwao, msongamano unamsumbua.
Kaka .usijenge ukweni..
 
Umeliona hilo...!!? Karibu ...
 
Mbona hazitaki ... Kamuita Mama yangu na mama mkwe ..baba yangu kafariki 2002, baba yake kafariki 2020 .... Anachoomba nirudi nyumbani atabarika ... Anajua jinsi navyopambana ... Nimemwambia baki navyo ... Ameomba mpaka Misa ya kubariki ndoa ....
wazee wetu walikua wanafukuza wanawake zao waende kwao wakajifunze na baadae huitishwa vikao na mwanamke kuonywa na kurudishwa kwa mume. sijui kama hii mbinu bado ipo legit kwa maisha haya ya kisasa .
 
Unajua ni Rafiki yangu kinyama... Nimesoma nae na tumeishi kitaa kimoja .... Namjua vizuri Ananijua vizuri ...ndio maana mpaka sasa anahangaika kulimaliza nirudi nyumbani .... Tangu majuzi nilikuwa nahangaika kutafuta makazi .. nimetulia sasa ndio najibu ... Keshawapia mama na mama yake wapo nyumbani (nilipoondoka) .... Niende tukayajenge .... Nimewaambia tu awahadithie madhila yote aliyonifanyia mpaka Mimi kuondoka .... Mkiyaelewa ndio tukae tunaaamuaje kuhusu malezi ya watoto sio kurudi Hapo.
Issue kwamba umemfanya awe rafiki yako?????
 
wazee wetu walikua wanafukuza wanawake zao waende kwao wakajifunze na baadae huitishwa vikao na mwanmke kuonywa na kurudiahwa kwa mume. sijui kama hii mbinu bado ipo legit kwa maisha haya ya kisasa .
Utandawazi Mzee...nimeondoka Mimi ..anahangaika yeye...
 
Utandawazi Mzee...nimeondoka Mimi ..anahangaika yeye...
sawa mkuu songa mbele bana usirudi nyuma as long as watoto wako pia ndio watakaofaidi hizo mali zako. sisi vijana ngoja tuendelee kujifunza kwenu mabro
 
Back
Top Bottom