Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!

Kwanini mnamlaumu tu Freeman Mbowe?

Nadhani tunahitaji kuwashauri CHADEMA the way forward. Kwamba, maamuzi yao ya sasa yako sahihi? Tuyaunga mkono hata kama yamekuja kwa kuchelewa?

Hata hivyo, binafsi naweza kusema, kuwa, hata ktk siasa zipo ajali pia a k.a ajali za kisiasa, zipo imperfections za kutosha..

Freeman Mbowe & CHADEMA hawawezi kuwa na maamuzi sahihi siku zote na muda wote. Kwa hili bila shaka ndiyo tunaona wazi kuwa they made wrong decisions..

No matter what happened...

No matter ni makosa gani wamefanya..

The fact remains kuwa CHADEMA bado ndicho chama tegemeo shindani pekee kuliko vingine vyote kuinyang'anya CCM dola..

Na bado uwezekano huu upo kwa zaidi ya 100% . Tuwashauri kuangalia mbele badala ya kuangalia wapi wamejikwaa..

Ni Ukweli kuwa hata Freeman Mbowe mwenyewe anajuta kwa hili kwa sababu amepoteza miaka zaidi ya miwili kwa ulaghai wa CCM..

Ndugu Nguruvi3, nini unawashauri CHADEMA? Tuendelee kulaumu tu kwa makosa yaliyokwisha kufanyika?
 
Mkuu Mayor Quimby , kwanza asante for being mchangiaji most objective kwa kuja na vifungu. Ibara ya 5 inahusu tuu haki ya kupiga kura, the right to vote, the right to choose.

Ili haki hii ya kuchagua iwe absolutely ni lazima kuwepo choice to choose from.
Japo haki ya kila Mtanzania upon the attainment the age of majority is free to vote, but freedom hiyo to vote is jeopardised by ibara ya 21 ambayo ili mgombea agombee lazima adhaminiwe na chama cha siasa.

Kwa lugha nyingine ni Watanzania wote wana haki ya kuwachagua sio viongozi wao wanaowapenda bali viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa!.

The right to vote but no right to be voted!
Mfano mimi naishi Kawe, wapiga kura wengi wa Kawe wako two classes, the haves and the have not, wale the have not ndio wengi, maeneo ya Ukwamani, vijiweni, standi za boda boda, bajaji, magoli ya jobless na wale dada zetu wale, Goba, Tegeta, Bunju na wote wa hali ya chini with nothing, mimi ndio mtu wao, ndie chaguo lao. Nilipojaza fomu kupitia CCM, nikakutana na Akofu, mkono mrefu, wajumbe wameangaliwa vizuri, vikao vya uteuzi vikampitisha Askofu mkono mrefu. Mimi nikakatwa,!. Hivyo wale wapiga kura wangu wote, they are denied their right to choose the leader of their choice!. Ilitakiwa baada ya CCM kuniona sifai, haki yangu kugombea ibaki pale pale, hatima ya peoples right to choose imekuwa forfeited na udhamini wa chama cha siasa. Mwananchi ndie the most important kuliko kitu chochote!. Ndiye mwenye nchi, ndiye mwenye katiba, ndiye the big boss anayemuajiri Rais, Serikali, Bunge na Mahakama na kuwalipa mishahara kwa kodi yake, huyu mwananchi mwenye nchi, haki yake ya kumchagua kiongozi anayemtaka umeporwa na kinyangarika fulani kinachoitwa chama cha siasa!. This is no right!.
kulazimisha mtu kuchaguliwa ni lazima adhaminiwe na chama cha siasa, ni kinyume cha Ibara ya 11 ya katiba!. Huu ni ubaguzi kuwabagua watu wote wasio na vyama, na ili kugombea unalazimishwa lazima ujiunge na chama cha siasa!.
Shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni shurti batili kinyume cha katiba.
Hapa ndio kwenye mtihani mkubwa kabisa wa kujua mtunga katiba ilidhamiria nini, mtunga katiba alikuwa na dhima ya kila Mtanzania kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa. Nimejitolea kuendesha darasa la dhima ya mtunga katiba. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?
Uwezi kutoa tu kichwani kwako kwa sababu umesoma sheria na kudhani hiyo ndio sheria.
Kwenye issues za katiba, mfano hapa Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? I might be right, Serikali, Bunge, Mahakama, they may all be wrong!.
JPM alikuwa ni habari ingine!, usikute huu ulikuwa ni utekelezaji wa ushauri huu Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'! angalia ulitolewa lini!.
Ukiwasikiliza wanasheria wa Tanzania hakuna kesi ya kushinda ulaya, labda yule jamaa au sijui taasisi iliyokuwa na website ya ‘Jaba-Shadrack’ waliobaki hamna kitu.
Kwenye hili nakubaliana kabisa na wewe.
P
 
Kwa maelezo yako ni wazi uwezo wa rais ni mdogo Ila Mbowe naye akishindwa.kutumia fursa zilizokuwa zinajitokeza kwa kujifanya na yeye ni sehemu ya uongozi wa nchi kwa kifupi amepoteza nguvu kubwa ya ushawishi.
Baadhi ya Mambo yaliyompotezea ushawishi
1. Kukataa kuunga mkono waliokuwa wanapinga mkatba wa Do world kids Chadema haikupewa nafasi.
2. Kukaa kimya wakati mfumkowa Bei ikiwemo kupanda mafuta, kupanda gharama za maisha ikiwemo kupanda kwa Bei za vyakula, mafuta ya kupikia, umeme, sukari na nauli halafu leo unarudi kwa watu walewale uliokataa kuwasemee ukitaka wakuunge mkono kisa Sheria za uchaguzi ni wazi wataona unajali zaidi Mambo yanayokugusa kuliko Mambo yanayowagusa.
 
Utasongaje mbele wakati Samia 4R hazitekelezi ila ni gheresha tu?
No 4R za Rais Samia is real, ila Utekelezaji wake ndio issue!.
Think deep, you shuld no think while anticipating to please samia for a nomination!...... unatafuta uteuzi tu.
Duh...!. Naomba niheshimu mawazo yako, ila pia karibu hapa Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza! kisha fungus link HII kisha uniambie mtu anayetafuta uteuzi kwa mteuzi anaweza kuandika hivyo?.
Mtu anakudanganya na wewe unakuwa zuzu eti kuna R4 ambazo ni cosmetic tu na mwenye kuzipendekeza hazitekelezi. Unaona kabisa kuwa huyu anataka kuwatoa kwenye reli..
Mbona they are working perfectly!.
SWALI: SAMIA ANAONA UGUMU GANI KULETA KATIBA MPYA? KUANDIKA MISWADA KAMA WADAU WALIVYOSHAURI? ANAOGOPA NINI? KUNA MADHARA GANI? Mpelekee maswali hayo akupe majibu utuletee hapa Pascal Mayalla
OK nitamtafuta na kukuletea mujibu hapa!.
P
 
Umeongea uongo. Process za kutunga miswada lazima zipite kweñye Baraza la mawaziri. Sasa utasemaje Rais hajui wakati ndio mwenyekiti wa Baraza la mawaziri.
Kuna vitu technical hata wajuzi hawavijui, kama wanasheria ma nguli wabobezi na wabobevu wameshindwa kubaini kuwa wametunga muswada batili, wakapeleka bungeni kwenye wanasheria manguli wabobezi na wabobevu nao wakishindwa kubaini ubatili wake, Bunge likatunga sheria batili!, so what are the chances kwa a layman kama Rais Samia?.

P
 
Ikiwa unaamini Mh Raisi aliweka Saini katika muswada ambalo haujui ndani yake ulivyo, huku mawaziri wakijua kilichopo, basi hakuna budi kuamini kwamba nchi haina kiongozi.
Yes that has happened not once not twice, several times!, ila sio Rais Samia. Kama Bunge litaendelea kuitunga sheria batili hii, Rais Samia ataisaini faster, kisha tutakuja kukutana Mahakamani!.
P
 
Eti Tundu Lissu anamtukana Samia. Kipi alichotukanwa!? Kuambiwa ukweli ni kutukanwa!? Hii Katiba ya kipuuzi ya ccm imefanya Rais aonekane mungu mtu fulani hivi na akikosolewa inakuwa katukanwa. Acheni unafiki.
 
Safi sana kwa kuliona hili. Hii nchi ina wajinga wengi sana Aisee! Mazuri yananasibishwa na Rais ila mabaya wanasukumiwa wasaidizi, Hawa wapuuzi sijui wanatuonaje!?
 
Ukweli utatuweka huru;hivi katika hii nchi ni kweli Samia ana uhuru wa kufanya uamuzi mgumu unao husu nchi au Kuna state machinery tusiyo ijua ndiyo inafanya decisions na yeye ni mtekelezaji tu!!
Marais waliomtangulia walikuwa na all powers at their disposal lakini huyu Kuna kundi linamdhibiti ingawa hawezi kusema!
 
Mimi mnanishanagaza watu wa Tanzania hii. Sifa nzuri nzuri anayepongezwa ni rais. Mfano utasikia, TRA imevuka lengo la makusanyo. Rais Samia apewe sifa. Mara sijui umeme wa uhakika, rais apewe sifa.
Watumishi wote wa umma, muajiri wao ni rais wa JMT na kila wachofanya wanafanya kwa niaba ya rais.
Ila zikika sifa mbaya za serikali mnataka kumtenganisha na sifa hizo.
Ndivyo katiba yetu inavyoelekeza, rais hakosei na hashitakiwi!.
Kwangu ukisema yeye si mwanasheria anaweza kuwa hajui ubatūili wa katiba si utetezi maana rais hatutegemei ajue kila kitu ila kazungukwa na wataa ambao inapaswa awatumie.
yes ila waliomzunguka, hawamwambii ukweli kuwa muswada huo una ubatili.
Mbowe kavuna alichopanda taingia mwanzo yale maridhiano yalikuwa ni janja janja tu.
Duh...!
Maridhiano ilikuwa ni marekebisho ya katiba si kuitwa ikulu upewe fadhila.
Duh ...!
Mtu akikupa fadhila kesho anaweza zichukua kama ambavyo wana ccm mnadai kuruhusu mikutano ya kisiasa ni huruma ya rais Samia kwa wapinzani
Hili neno!. Nimelizungumza hapa Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
P
 
Punguza ujinga. Miaka yote ccm inaongoza wameiba fedha kiasi Gani na wamechukuliwa hatua Gani!? Unakuja kulaumu wapinzani waliofanya kazi kubwa ya kuonesha wezi wa ccm wanavyoitafuna nchi.! Akili Yako itakuwa ina matatizo. Kapambane kwanza na wale wanaosema "wema hawafi"
 
Ninavyofahamu mimi ni kwamba hata kwenye mataifa makubwa kama Marekani na mengineyo Kiongozi Mkuu huwa anao wanasheria wake binafsi katika kumshauri katika mambo yote yanayohusu sheria
I mean personal lawyers !
Je kwenye Nchi changa zinazoendelea hivi vitu haviruhusiwi ?
 
Chama chetu kiko Imara sana, sisiemu si kidude kidogo hivi kiasi kwamba waweza kichezea chezea
 
Aisee! Nimeshangaa sana Mayalla na hizi hoja zake. Eti watu wakapige kura!? Hivi huyu mtu ni mgeni nchi hii!? I'm very disappointed na huyu jamaa. Ni kama amesahau ya Zanzibar na yale aliyofanya Magufuli 2020.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…