Wanabodi,
Nimemsikiliza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika bandiko hili
Mbowe: Najutia kumuamini Rais Samia
View: https://youtu.be/Xjao83Ghy04?si=qSQTeSxIx_8B5a-L
Kiukweli kabisa mimi nimemwelewa sana Mwenyekiti Freeman Mbowe hapa, na hata ningekuwa mimi!, I would have felt the same, but not done the same, I would have done something worthwhile but not maandamano!.
Namuomba sana Mhe. Mbowe, please usipoteze imani na Rais Samia!, kwasababu Rais Samia ninaye mfahamu mimi, sio mtu mwenye ndimi mbili!, namfahamu fika Rais Samia kwa kauli na matendo, yeye kama yeye, hawezi kabisa kusema hivi haiafu akaja kutenda vile!. She is straightforward person and firm, tena usikute yeye kwa intellect yake, japo ndie aliyeongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichopitisha miswada hiyo lazima ukakuta yeye wala hajui kuwa mswada sheria ya uchaguzi una ubatili ulioshabatilishwa na Mahakama Kuu kwasababu yeye sio mwanasheria!.
Japo miswada yote ya serikali, lazima ipite Baraza la Mawaziri ijadiliwe, wakati mswada huu wa sheria ya uchaguzi unajadiliwa, hakuna mtu yeyote mule akiwemo AG, aliyemwambia ukweli Rais Samia kuwa muswada huo una ubatili!, hivyo mtu ambaye sii mwanasheria hawezi kuujua ubatili wa kisheria kwenye vipengele vya miswada mpaka aelezwe na wanasheria!. Hivyo kwa intellect ya Rais Samia, kumlaumu kwa kutoyajua haya ni kumuonea bure!.
Kwa bahati nzuri, mimi ni miongoni wa watu wanaomfahamu Rais Samia sio tuu kwa kauli na matendo, bali kwa kufanya nae mahojiano ya ana kwa ana mara mbili. Mara ya kwanza akiwa Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais na mara ya pili akiwa Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.
Wakati akiwa VP nilimfanyia uchambuzi mara mbili
Mara ya kwanza ni hapa
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na mara ya pili ni hapa
"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Na baada ya kuwa Rais wa JMT, pia nilimfanyia uchambuzi mara mbili
Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... na
Ili kupata Viongozi Bora baadae, Watanzania tujifunze kuwasoma watu kwa asili zao. Mjue Samia alivyo kwa asili yake
Hivyo kwa kauli na matendo, ya Rais Samia, hiki kinachofanyika kwenye miswada hii, naamini kabisa sio yeye, bali waonayafanya haya ni wanasheria, waojua fika ubatili wa muswada huu, lakini wametake advantage ya intellect yake Rais Samia kumsokomezea ubatili tena, ikapelekwa Bungeni, itapitishwa, na kutungwa sheria batili, kisha Rais Samia ataisaini kuanza kutumika, kwa excuse kuwa batili hiyo kwa vile iko kwenye katiba yetu!, then ni batili halali!. Kisheria, batili ni batili, hata ikichomekewa kwenye katiba kiubatili, bado inabaki ni batili, na badala ya kuihalalisha haramu kwa kuichomekea kwenye katiba, haramu hiyo inaiharimisha katiba na kuibatilisha katiba kwa kuifanya kuwa na unajisi!.
Mimi naamini kabisa kwa haya yanayofanyika kuhusu Muswada huu, huyu sio Rais Samia ninaye mfahamu mimi, na naamini kabisa yeye wala hajui kuwa muswada wa sheria ya uchaguzi ni muswada wenye ubatili unaokiuka ibara ya 11 ya katiba ya JMT na kuathiri ibara ya 5, ibara ya 21, ibara ya 39 na ibara ya 67.
Kwa vile yeye sio mwanasheria, hajui kuwa katiba yetu ina ubatili, uliochomekewa kiubatili na awamu zilizopita na Bunge lilolopita unakokwenda kinyume cha Ibara ya 5, ibara 21, ibara ya 39 na ibara ya 67 za Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Nimesema ninaamini kabisa Rais Samia hayajui haya na hapa niliandika
Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.
Hivyo kitendo cha Freeman Mbowe Kutomwamini Rais Samia, ni kumuonea bure, niliwahi kushauri
Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda, ila kama Freeman Mbowe anaona muda aliompa kwenye vikao vya maridhiano unatosha, sasa ndio aanzishe maandamano, huku sio kumtendea haki, namshauri Mbowe, aichukulie miswada hii kama fursa, afanye uhamasishaji na uelimishaji umma wa kufa mtu kwa Watanzania kwa ku invest in people, grassroot people kuhusu haki zao, ili Watanzania kwa mamilioni wajitokeze wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, na 2025 wajitokeze kwa wingi wawapumzishe watu kwa amani kupitia sanduku la kura na sii kupitia maandamano!.
Bahati nzuri sana na mimi nimehudhuria vikao vyote vitatu vya kukusanya maoni ya wadau na mara zote 3 nilipata bahati ya kuchangia.
Mchango wangu kikao cha kwanza ni huu
View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=9dtqZ-1-ZkzWo69t
Mkutano wa pili maoni yangu ni haya
View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=98HTkiMGNsmlLBGz
Na Mkutano wa tatu wa Kamati ya Bunge pia nilitoa maoni.
Nimeandika makala zifutazo kuhusu sheria hizi
Mbowe kutangaza maandamano nimetoa ushauri issues za kisiasa zitatuliwe kisiasa, halafu issues za kisheria zitatuliwe kisheria, utungaji miswada ni issue ya kisheria, baada ya watu kutoa maoni yetu, Bunge likitutungia sheria batili, this time around, we'll have to do something!.
Tangu Rais Samia ameingia madarakani ile March 21, 2021, mimi tuu mwenyewe, nimelisemea jambo hili la katiba, sheria na haki zaidi ya mara 100!,
Mhe. Freeman, rudisha moyo, applies zile 4R za Rais Samia tulisongeshe mbele kwa mbele.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali.