Nimenisurika mara nyingi kupigwa na utapeli wa mitandaoni kwa kutumia mbinu hii

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Habari za muda huu wana JF

Nimesikia vilio watu kupigwa kwenye Kalyinda nimeamua kuwaletea mbinu yangu niliyopata mwaka wa mwisho wakati namaliza kozi za Uwabata nchini Cuba (joking)

Mimi siamini kabisa katika pesa za kudownload yaani umekaa kiboya pesa zije kirahisi bila kutolea jasho naona kama changalamacho hivi na kutokana na mtizamo marafiki baadhi wamenichukulia kama mshamba hivi kwa sababu kila dili nikiletewa sitoki ushirikiano barabara.

Mbinu ninayotumia: Nikipewa mchongo na mtu kama kuna dili la fedha za kudownload mimi huwa namsikiliza na simpingi bali namwambia "Si biashara inakupa faida na una uhakika kutoboa kupo? basi nikopeshe na mimi nikipata faida ya kwanza nakulipa deni maana mimi kuna michongo bado naisikilizia"

Hapo napewa konakona na Kiswahili kingi basi naona magumashi maana kama kitu kingekuwa na faida ya haraka yenye uhakika na yeye akimleta mtu mpya kupitia link malipo yake yanongezeka sasa kwa nini ashindwe kumkopesha mtu anayemuamini kamtaji kadogo wakati yeye kapata faida na ana uhakika anayetaka kumkopesha atapata faida?

Juzi Kati nilitumia mbinu hii kuepuka Kalyanda maana kuna rafiki zangu kama wawili ninao waamini walinihakikishia ni kweli na kuna faida ila mimi nikasimamia misimamo yangu


Tukaendelea

Baadae


Nb: Tuchapeni Kazi tuache janja janja...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…