Nimenunua home theater LHD657 Model, lakini cha ajabu ina Sauti ya kawaida sana

Nimenunua home theater LHD657 Model, lakini cha ajabu ina Sauti ya kawaida sana

Duh sasa kama ni hvyo ht mbona bei kubwa sana halafu hamna cha maana zaidi?
Mi nilikosa wakati natafuta,wahuni wakaniambia we weka hela ununue Home Theatre tu utapata kile unachotaka lakini nikiwastukia maana wajinga wengi bei ikiwa kubwa ndio wanaamini kitu ni kizuri.
 
Ninayo LG ya hivi 1000 watts mziki wake nikifungulia 30 tu.ndani hukai.kitanda,dali,kabati,vyombo vyote vinatetetema.na ina volume mpaka 100.ila niliwahi kufika 50 tu.[emoji95][emoji95][emoji95]
JamiiForums-623056523.jpg
 
Shida hapo ni hiyo deki kanunue deki ya singsang toa hiyo iliyoijiapo mziki wa hapo hutasahau
 
Wengi wao hawazijui coz kupatikana ni ishu lakini trust me ukiipata Edfier umepata kila kitu unachokiitaji kwny mziki na movie. Hii niliyonayo inazaidi ya miaka 8 na mziki wake ni uleulee
ya kuanzia shilingi ngapi ndio iko fresh?
 
Uwingi wa spika sio ukubwa wa sauti na wala ukubwa wa watts wa redio sio ukubwa wa sauti.
Sauti ambayo inarekodiwa na wanamuziki ni stereo kwa maana ina njia mbili mithili ya masikio yetu yalivyo.Radio ambazo ni home theater sio kwa ajili ya kusikilizia muziki ila ni kwa ajili ya kutazamia muvi mana kwenye muvi kila spika moja hupewa sauti maalumu kwa mfano kuna spika zinatoa sauti ya mazungumzo tu, kuna ambazo zinatoa sauti ya effect za kwenye muvi, kuna ambazo zinatoa sauti ya saund track na mambo mengine mengi na ndio maana ukizitumia kwenye mziki sauti haziwi kubwa sana kwa sababu spika ambazo zinafanya kazi huwa ni tatu tu( 2.1)spika moja ya kulia, moja ya kushoto na subwoofer.
Kitu kingine ni kwamba nguvu ya spika haipimwi kwa watt.Watt inaonyesha kiwango cha umeme ambao redio itatumia kwa muda fulani.Kiwango cha sauti kinapimwa na SPL yaani Sound pressure level.
Kadri Spl inavyokuwa kubwa ndo sauti nayo inakuwa kubwa. Kwahiyo redio kubwa ambayo ina watt kubwa na spl ndogo inazidiwa mdundo na radio ndogo ambayo inawatt ndogo ila spl kubwa.Kama shida yako ni sauti basi zingatia spl ila kama shida yako ni kujua redio inakula umeme kiasi gani basi zingatia watt.
Somo kubwa sana hili
 
Ni kampuni ya LG. Kuna maandishi yanasomeka lhd657 january 2023. Nimeifunga ndani kwangu cha ajabu inazidiwa mkito na hizi sabufa za kichina spiano

Nimeinunua 700k. Pesa yangu inaniuma sana kwa hiki nilichokutana nacho

Nimeagiza mwanza sijafata mwenyewe. Je, hii sio fake kweli wakuu?
LG Home theatre haina bass kubwa ila ina sound quality ambayo hakuna subwoofer ya mchina inaweza kufikia. Pili, hiyo home theatre inadumu milele. Subwoofer za kichina zina bass kubwa ndiyo lakini baada ya muda mfupi zitaanza kukoroma na hata kufa kabisa. Hiyo LG yako hautajutia kabisa. Time will tell…
 
Back
Top Bottom