Nimenunua home theater LHD657 Model, lakini cha ajabu ina Sauti ya kawaida sana

Nimenunua home theater LHD657 Model, lakini cha ajabu ina Sauti ya kawaida sana

mkuu utoke mziki mzuri uliochujwa base yenye mkito. sasa cha ajabu base ipo chini hata ukiongeza hamna chochoke kinachobadilika. mfano volium ipo 100 ni ya kawaida sana ukipunguza mpaka 40 ndio imeisha hiyo
Umepigwa
 
Kama ulitaka mziki, nenda na music system sio home theatre, home theatre is for surround sound kama dt dobbie nk ambazo utaskia souti ya movies vzr kwanye hizo channel 5 za sauti, hakuna mziki una channel 5, mziki ni sterio ya channel 2 tu.

Ukitaka mziki, chukua music system hii, andaa milioni zako kadhaa
[emoji2956]
img_3_1685851883129.jpg
 
"Habari, watu wangu! Karibu Rahisi Point, mahali pa kujipatia TV na SABUFA kwa bei poa kabisa!
Tunakuletea ofa za kusisimua na huduma bora kabisa. Piga kambi nasi kwenye safari hii ya ununuzi smart! [emoji342][emoji91]

[emoji419][emoji419] Pia unaweza kupata OFFER YA Blender au jiko la umeme la Plate 2

OFFICE ZIPO TANDIKA ROUND ABOUT YA MAJARIBIO au
[emoji338]Piga 0686 886 507

[emoji419][emoji419]MIKOANI TUNATUMA KWA UAMINIFU MKUBWA [emoji120][emoji106]

IG - @Rahisi_Point
FB - @RahisiPoint
#RahisiPoint #TV #SABUFA #BiasharaSmart"
 
Hizi radio nyingi huwa ni issue ya setting, cheza na remote vizuri, cheki bass, check noise, mwisho cheki connection za waya kama zipo sawa.
Kuna rafiki yangu mmoja alinunua subwofer la aina ya Seapiano, akiwasha inaongea kama sauti ya simu ya kitochi, nikakutanaye naye yupo kwenye bajaji ameibeba nairudisha.

Nikamwambia rudisha radio nyumbani, kisha nikamwambia aunganishe kama alivyounganisha mwanzo. Kwanza kule nyuma zile speaker alikosea kuunganisha, nikaweka sawa. pia ukiangalia kwenye remote especial ya Seapiano sijui kwa LG, kuna sehemu ya bass imeandikwa - na +, bonyeza + mpaka mwisho. Nenda sehemu ya noise weka on, kuna sehemu nyingine tena ina alama za - na + ponyeza plus usikilize mdundo utakao toka.

Hizi radio zimekuwa designed unaweza kata kabisa bass ikawa stereo tupo na hiyo hiyo ukaweka busy na usiamini kama hiyo ni radio ile ile.
Unasema unaweza kata base ikawa "stereo tupu"?

Stereo unajua ni nini mkuu?
Stereo SIO Treble/mchicha.

Stereo ni 2 channels kwenye sound/audio.
 
Me natumia edifier. Hii kitu ni zaidi ya speaker. Haziharibiki wala hazichuji mziki wake ni balaa
Kwa Edifier hapa sasa tunazungumzia mziki.

It's a good entry level set inayokupa mziki halisi. I hope Edifier uliyonayo ni Active Speakers.

Inashangaza M'bongo anataka mziki halafu anaenda kununua Homethearte au soundbar(soundbar ni home thearte pia, in a bar)!!
 
Uwingi wa spika sio ukubwa wa sauti na wala ukubwa wa watts wa redio sio ukubwa wa sauti.
Sauti ambayo inarekodiwa na wanamuziki ni stereo kwa maana ina njia mbili mithili ya masikio yetu yalivyo.Radio ambazo ni home theater sio kwa ajili ya kusikilizia muziki ila ni kwa ajili ya kutazamia muvi mana kwenye muvi kila spika moja hupewa sauti maalumu kwa mfano kuna spika zinatoa sauti ya mazungumzo tu, kuna ambazo zinatoa sauti ya effect za kwenye muvi, kuna ambazo zinatoa sauti ya saund track na mambo mengine mengi na ndio maana ukizitumia kwenye mziki sauti haziwi kubwa sana kwa sababu spika ambazo zinafanya kazi huwa ni tatu tu( 2.1)spika moja ya kulia, moja ya kushoto na subwoofer.
Kitu kingine ni kwamba nguvu ya spika haipimwi kwa watt.Watt inaonyesha kiwango cha umeme ambao redio itatumia kwa muda fulani.Kiwango cha sauti kinapimwa na SPL yaani Sound pressure level.
Kadri Spl inavyokuwa kubwa ndo sauti nayo inakuwa kubwa. Kwahiyo redio kubwa ambayo ina watt kubwa na spl ndogo inazidiwa mdundo na radio ndogo ambayo inawatt ndogo ila spl kubwa.Kama shida yako ni sauti basi zingatia spl ila kama shida yako ni kujua redio inakula umeme kiasi gani basi zingatia watt.
Well
 
Back
Top Bottom