Uwingi wa spika sio ukubwa wa sauti na wala ukubwa wa watts wa redio sio ukubwa wa sauti.
Sauti ambayo inarekodiwa na wanamuziki ni stereo kwa maana ina njia mbili mithili ya masikio yetu yalivyo.Radio ambazo ni home theater sio kwa ajili ya kusikilizia muziki ila ni kwa ajili ya kutazamia muvi mana kwenye muvi kila spika moja hupewa sauti maalumu kwa mfano kuna spika zinatoa sauti ya mazungumzo tu, kuna ambazo zinatoa sauti ya effect za kwenye muvi, kuna ambazo zinatoa sauti ya saund track na mambo mengine mengi na ndio maana ukizitumia kwenye mziki sauti haziwi kubwa sana kwa sababu spika ambazo zinafanya kazi huwa ni tatu tu( 2.1)spika moja ya kulia, moja ya kushoto na subwoofer.
Kitu kingine ni kwamba nguvu ya spika haipimwi kwa watt.Watt inaonyesha kiwango cha umeme ambao redio itatumia kwa muda fulani.Kiwango cha sauti kinapimwa na SPL yaani Sound pressure level.
Kadri Spl inavyokuwa kubwa ndo sauti nayo inakuwa kubwa. Kwahiyo redio kubwa ambayo ina watt kubwa na spl ndogo inazidiwa mdundo na radio ndogo ambayo inawatt ndogo ila spl kubwa.Kama shida yako ni sauti basi zingatia spl ila kama shida yako ni kujua redio inakula umeme kiasi gani basi zingatia watt.