Nakumbuka enzi zetu kuwa na pasi ya mkaa tu ilikuwa anasa, mara nyingi ili kunyoosha nguo tulikuwa tunazipeleka kwa dobi.
Kinyume na hapo unazikunja nguo vizui, unaziweka chini ya godoro, unalalia, ukiamka zimenyooka vizuri.
Kuhusu maharage, tulikuwa tunayaloweka ile usiku, asubuhi unaenda kazini, jioni ukirudi unayachemsha kwa muda wa dakika 20 au nusu saa tayari yanakuwa yameshaiva. Ukijisahau ukaendelea kuyaacha yamelowekwa hadi siku ya pii unakuta maji yameshakolea rangi ya mchuzi wa maharage, halafu maharage yenyewe yameshaanza kuota humo kwenye sufuria