Soulja boy
JF-Expert Member
- Oct 3, 2015
- 4,052
- 7,375
Mkuu iv serikali wameitaifisha?Watu washatapeli Bandari huko.. alafu unakuja kusema UMENUSURIKA..
Watu tushapigwa mpk dakika hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu iv serikali wameitaifisha?Watu washatapeli Bandari huko.. alafu unakuja kusema UMENUSURIKA..
Watu tushapigwa mpk dakika hii
Pumbavu! Huu kwanza ni uongo. Tukio dogo namna hii unaeleza utafikiri ni kesi ya uhaini!Hata siku moja usiseme kwamba wewe ni mtoto wa mjini hivyo huwezi kutapeliwa, Hao matapeli kila siku wanakuja na mbinu mpya omba Mungu tu usikutane nao, Nawapa kisa hiki ili na wengine mjifunze pia hivyo jitahidi kusoma huu uzi hadi mwisho.
Jana siku ya jumanne nilipata cm ya jamaa aliejitambulisha kama mteja na kwamba ameona post zangu za mashuka na angependa kuniungisha kwa jumla (I don't know huyu mtu aliona tangazo langu hapa JF au kwenye social medias nyingine ila ni kawaida mimi kupokea simu za wateja kila wakati)
Jamaa; Bwana nahitaji mashuka size fulani idadi fulani naomba bei ya jumla maana nataka kuyaweka dukani kwangu niuze.
Mimi: Sawa nitakufanyia kwa bei fulani mkuu (malipo kwa utaratibu wangu kwa wateja walio ndani ya dar huwa ni baada ya kupokea mzigo ila baada ya hili tukio sasa nabadili utaratibu kwamba mzigo ukifika kiwango fulani kitachoonesha ni kikubwa basi mteja atapaswa kulipia advance ili mimi kuwa na asilimia 50 za uhakika)
Jamaa: Sawa, mimi nipo sehemu X kama una bodaboda muambie anifanyie delivery
Mimi: Sawa.
Maongezi hayo yalifanyika jana siku ya jumanne mchana... (ni kawaida kwangu kupokea simu kama hizi hivyo haikuwa big issue though jamaa aliagiza mzigo mkubwa kidogo maana alisema ni kwaajili ya biashara). Kiukweli kwa muda ambao alinicheki nilikuwa tight sana kutokana na ubusy wa kuhudumia wateja wengine ambao walimtangulia kabla hivyo nilishindwa kuwa ontime sana na kujikuta naanza ku-deal na order yake jioni mida ya saa kumi, Sikuwa na wasiwasi kwani nilikuwa na uhakika kwamba hatuwezi kupishana kwani Fast delivery ipo (Bolt), Mashuka yangu nayaaminia kwenye ubora n.k
Baada ya kupack mzigo wa jamaa na tayari nilisharequest usafiri ndipo nikampigia jamaa kumjilisha kwamba ndo natoka ili awe tayari kupokea mzigo wake, Kupiga mara tano zote simu haipokelewi alafu boda kashaanza kufunga mzigo kwenye chombo, Sikuwa na wasiwasi bado na nilihisi pengine jamaa huko alipo alikuwa mbali na cm hivyo sikuwaza kumkatisha jamaa wa bolt kuendelea kuufunga mzigo kwenye chombo, Baada ya jamaa kumaliza kuufungawakati navaa helmet nikaona nijaribu tena kumpigia jamaa kwa mara 6 huku nikimsindikiza na ujumbe kwamba ndo natoka, Ndipo baada ya kama dk 5 za Safari ujumbe ukajibiwa hivi⬇️
View attachment 2649180
Dah! Ukicheki tayari nipo robo ya safari, ikabidi nimpigie ili japo kumjuza kwamba nilishaanza safari na labda akihitaji ku-cancel kwa kuofia nitachelewa na mimi nikiwa na uhakika kwamba ndani ya 30mints ningekuwa nimemfikia aliponielekeza ila jamaa alisisitiza kwamba muda umemtupa mkono hivyo tufanye kesho tu ambayo ndiyo leo jumatano, Kwa kuwa nina experience ya Faida na hasara sikuona taabu bali nilimuelekeza jamaa wa bolt hali halisi na tukakubaliana anirudishe store... Baada ya kafanikisha yote yale mzigo sikutaka kuufungua kwenye package niliyoifunga bila kupata permission ya jamaa kwamba je, hiyo kesho ni uhakika kweli au kama anahisi order yake imeicancel mazima basi nifungue ile package ila jamaa akajibu nisiifungue kwani ni uhakika.
Tuje siku ya leo (Jumatano) siku ya tukio....
Kutokana na jamaa alisisitiza asubuhi basi saa moja juu ya alama nilikuwa macho tayari nikashtua mwili kiasi kisha nikamtumia jamaa ujumbe kumuuliza kama ratiba ipo sure kama tulivyopanga ila hadi kufika saa 3 sikupata majibu ndipo nikaamua kufungua ile percel kwa kuwa nilihisi labda jamaa ni mswahili tu ila ilipofika saa 4asbh simu ya jamaa iliita na akanipangilia kwamba baada ya nusu saa atanipanga wapi tukutane. Hakunicheki baada ya nusu saa bali baada ya lisaa na mara hii alibadili location na kunitajia sehemu nyingine ambayo alidai ni ofisini kwake. Sikuona taabu maana haikutofautiana sana na pale pa mwanzo kwani ilikuwa ninkutuo kinachofuata tu baada ya kile cha maelekezo ya mwanzo. (Kutokana na haraka na sikutaka kupishana na jamaa kwa mara hii basi mzigo sikuhangaika kuupack kwa mfuko tena bali niliufanga vizuri tu kwa kamba ukakaa poa kisha nikarequest usafiri na kumjuza jamaa kwamba nilishatoka)
Picha linaanza,
(Kwanza hii siku mvua ilikuwa inanyesha hivyo nimenyeshewa sana alafu nimefika destination husika kabla nimpigie jamaa simu kwamba nipo kituoni ile kamba niliyotumia kufungia mzigo ikakatika ila kwakuwa nilikuwa na kitambaa fulani cha kujifutafuta jasho kilinisaidia kuunganisha tena ile kamba ndipo mimi nilipata walau uwezo wa kujitwika ule mzigo ambao almost ulikuwa na thamani kama ya 500k)
Nilipompigia jamaa cm akapokea na kisha akanipa maelekezo fulani ya wapi nielekee baada ya kufika pale.
Jamaa: Kuna njia fulani ipo kwa mbele inaingia kushoto umeiona
Mimi: Ndiyo naiona mkuu.
Jamaa: Ingia nayo kuna kanisa unaliona kwa mbele sasa kwa nyuma kuna hospital ndo nipo nahudumia wagonjwa hivyo utanikuta tu.
Mimi: Sawa mkuu.
(Kiukweli ule mzigo ulikuwa mzito na aikuwa na jinsi japo jamaa aliniambia sio mbali na ni kama mita 100 kutoka nilipo na haina haja ya usafiri ila niliita boda) boda akanirusha chap sana pale hoapital.
Kufika kwa nje ya hospital nikakutana na majamaa wawili ambao baada ya kuona ule mzigo wa mashuka walionesha kutamani sana na wao walau waniungishe (kumbuka packages za mashuka ni transparent hivyo zilionesha dhahiri kilichopo ndani) so wakawa wananiuliza bei yake n.k ila niliwajibu kwamba ule ni mzigo wa watu niliagizwa hivyo kama wangehitaji na wao wachukue mawasiliano ili waweze kuagiza na wao muda wakihitaji, Nikawapatia namba ya cm... Ghafla simu ya jamaa ikaita na nikamjuza kwamba nipo nje ya hospital aliyonielekeza nifike.
Wakati huo bado nilikuwa kwenye boda, Jamaa akaniambia kashaniona na ameona mzigo ni mkubwa kidogo na asingeweza kuuhifadhi kwa pale ofisini hivyo akanipa maelekezo kwamba nirudi na boda nyuma kidogo kwenye njia niliyojia kwamba kuna frame fulani inauza keki basi kuna binti yupo pale anampa maelekezo yote na yeye ndo atampokelea ule mzigo.
Simu ilikuwa loudspeaker so sauti ilipenya masikioni kwa jamaa wa boda na kumfanya asitake kusubiri sana na akageza chombo na chap tukafika nilipoelekezwa nifike. Nikamlipa boda chake akaondoka zake nikabaki na dda wa frame ya bakery pale.
Mimi; Mambo
Dada: Pow, Karibu.
Mimi: Asante kuna jamaa ana mzigo wake hapa nadhani amekupa maelekezo
Dada: Ndiyo, ameniambia nihakiki idadi kwanza. (Yule dada akahakiki na ghafla jamaa akapiga cm)
Jamaa; Vp umeonana na dada huyo?
Mimi: Ndiyo
Jamaa: Haya mpe simu.
Nakuja kuendelea wakuu...
Mapema tu watu washaweka Bandari begani.. wamepita hivii..Mkuu iv serikali wameitaifisha?
Komenti yako menikumbusha luminous and non luminous flame enzi hizo kwenye kemia.cc: non-luminous _Flames
Tunashukuru na tunasubiri hapa ..yah nipo kuelezea ili mwingine ajifunze
Mi nilipigwa mbezi Kwa msuguri Kwa style hii kama ya kwako, nilipigwa mzigo wa thamani ya 350000, nilitumiwa malipo Kwa njia ya bank kumbe muamala siyo aisee , sema mi skuwa na bahati kama yako ya kutokea vikwazo vidog vidog ili kuchelewesha mzigo usitembee haraka , Yani Ile kwenda Kwa wakala kuhakiki pesa na kuambiwa huu muamala siyo tayar mzigo ushatembea , boda niliyekuwa naye alinisaidia kumfukuzia jamaa lakini akatupotea kwenye Mataa na ilikuwa night , nouma Sana , mpak sa hv nikiona mteja oda yake ina usumbufu hata sihangaiki huyo ni tapeliNaendelea....
Wakati yule dada anaongea na yule jamaa mimi nilikumbuka kitambaa changu nilichotumia kufunga ule mzigo na kuanza kukifungua, Kitendo nimemaliza kufungua kile kitambaa na yule dada akawa amamemaliza kuongea na jamaa na akanipa simu yangu nami nikaiweka sikioni kumaikiliza jamaa hatma yake ni nini.
Jamaa: Sasa dada kasema mzigo upo sawa, sasa naomba acha huo mzigo hapo kisha njoo hapa hospital utanikuta nije nikupe hela yako.
Mimi: Sawa mkuu (Nikamuaga yule dada, Nikauacha ule mzigo ukiwa haujafungwa upande mmoja na kuanza Safari ya haraka kuelekea pale hospital aliponielekeza jamaa)
Kufika pale hospital jamaa akaniambia niingie nimsubiri pale reception anakuja.
Kweli nimesubiri kama dk tano ila machale yakanicheza na nikajiuliza ni kwanini hii order ya jamaa imekuwa na changamoto sana, Na imekuwaje mzigo nimeacha kwa madada ambae simjui na hadi muda huu sijalipwa hata advance? Ndipo akili ikaniambia "Wewe ebu toka hapo reception kimbia upesi rudi kwa yule dada kaweke uhakika wa mzigo usiondoke bila wewe kutoa permit" Sikujiuliza mara mbili ghafla mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio nami nikaamka chap na kuanza kukimbia kuelekea kwenye ile frame niliyoacha mzigo (huku naona simu ya jamaa inaita ila sikutaka kuipokea na nisijue ni kwanini niliipuuza). Ndipo natokea barabarani hivi kwa mbali naona kuna bodaboda anafika na abiria alafu abiria yule akashuka haihai kuingia pale na mimi huku speed nikiongeza na sasa nikaanza kukaribia ile frame ndipo nikashuudia yule abiria amerudi kwenye bodaboda alaiyokuja nayo kwa upesi sana na boda akawasha chuma wakaondoka. Ila kwa mimi ile action ilinipa wasiwasi kwamba hawa vipi mbona wako fasta sana na kama ni kuchukua mzigo wangu mbona wameondoka mikono mitupu? Sikujiuliza sana nikajikongoja na kuingia kwenye ile frame niliyoacha mzigo wangu, Nikamkuta yule dada yupo normal tu... Kuchungulia nilipoacha mzigo nikauona ndipo nikapumua kidogo kwa afadhali na nikamuuliza yule dada.
Mimi: Nimerudi maana nimehisi kama kuna kamchezo hapa (kabla sijaendelea yule dada akanikatisha)
Dada: Ehee, umeona hao uliopishana nao na bodaboda?
Mimi: Ndiyo, niliwaona ila nilikuwa kwa mbali kidogo ila niliona kama wapo fasta sana ila sikuwajali maana na mimi nilikuwa na mawazo pengine kwa muda niliopoteza reception pale labda huku nazungukwa.
Dada; Yaani ni kweli kaka yangu, hawa wtu ndo walikuwa wamejia huu mzigo, Mara ya kwanza alikuja mmoja ambae ndo yule tuliekuwa tumewasiliana nae akaniambia ameshamalizana na wewe na akautoa mzigo nje akitaka kuondoka nao ila kutokana na itilafu ya ile kamba akashindwa kuubeba ndipo akaaga kwenda kuita bodaboda, Wakati amendoka mimi pia machale yakanicheza nikaurudisha huu mzigo ndani maana alikuwa kauweka pale nje barazani na ndipo baada ya muda ndo wakaja wawili kama ulivyowaona, Ila awamu hii ikabidi nimchallenge kwamba ngoja nikupigie wewe ulieniachia kwanza kama wameshakupa hela sasa wakati ndo tunabishana ndo yule mwenzake amabae ni bodaboda akawa anamuita kama anamshtua kwamba waondoke ndo wakatoka kwa haraka hata nisielewe shida ni nini.
(kwanza nikapumua kama sekunde 50 nisimjibu kitu yule dada ndipo nikamjibu)
Mimi: Dada hao wamekimbia kwa kuwa yule wa nje aliniona ninavyokuja kwa kasi pengine alihisi nimewashtukia ila sio kesi dada asante sana kwa kuwawekea kikwazo kidogo na pia kingine ile kamba kukatika imekuwa msaada mwingine.
Yule dada alinipa pole sana ila kwa muda huo mimi nilikuwa tu nikiumia ni kwanini wanadanu tumekuwa na roho za kikatili kiasi hiki, Imagine watu wazima kabisa wanaunda timu kuja kutaka kuniumiza mimi mtoto wa kimaskini ninaejitafuta kweli? sh.500,000 mimi si ningekonda kwa mawazo nifie gheto wakuu? Ni hela ambayo nikiwatumia wazazi wangu wananibariki hadi nshangaa asee ila watu hata hawajali.
Basi niliishia tu kumshukuru Mungu wangu ambae nimekuwa nikimuomba kila wakati na haniachi, Na pia baada ya lile tukio wala sijahangaika kumcheki tena yule jamaa kwa kumuonesha nimechukia au nimemdharau bali sinimeamua tu kuupack ule mzigo na kuurudisha store.
Jamaa amenipa loss ya 15k kwaajili ya usafiri pamoja na muda wangu na pia nimenyeshewa sana na mvua ila ni heri kuliko ningepata loss ya vyote.
Mwisho: Wewe ukijaribu kunitapeli kama upo humu au kama utauona huu uzi ama hakika Mimi nimekusame ila nimekuachia Mungu adeal na wewe.
Ambao mnakubali nini nafanya naombeni muendelee ku-support biashara yangu.
Ahsanteni sana kwa kuusoma uzi wangu hadi mwisho kama kuna some corrections za spelling and stuff like mnivumilie tu 🤝
Pole sana mwanangu, Changamoto ni za kawaida so, ukiumia ni vyema ukawa mwalimu kwa wengine ili wajifunze kuepuka, so mimi kupoteza Muda wangu kuandika uzi mrefu huu nina hakika nimeokoa watu 50+Mi nilipigwa mbezi Kwa msuguri Kwa style hii kama ya kwako, nilipigwa mzigo wa thamani ya 350000, nilitumiwa malipo Kwa njia ya bank kumbe muamala siyo aisee , sema mi skuwa na bahati kama yako ya kutokea vikwazo vidog vidog ili kuchelewesha mzigo usitembee haraka , Yani Ile kwenda Kwa wakala kuhakiki pesa na kuambiwa huu muamala siyo tayar mzigo ushatembea , boda niliyekuwa naye alinisaidia kumfukuzia jamaa lakini akatupotea kwenye Mataa na ilikuwa night , nouma Sana , mpak sa hv nikiona mteja oda yake ina usumbufu hata sihangaiki huyo ni tapeli