Nimenyang'anywa Watoto wangu na moyo unaniuma maana nawataka sanaa

 


Duh🤔🤔
 
Na wewe. Embu acha kutabiri mabaya
Hayo mabaya yaliyomtokea nilimtabiria mimi? Mimi sio mtabiri na neno ninalosema sio lazima litokee. Ni mawazo yangu tu
 
Wewe ndio una shida jichunguze tafta mke uone maana naona utakuja kuishia pabaya kuliko baba diamond
 
Mhmm kweli umepatwa na majanga. Na mbona unapapara ya kupata mtoto Bila kuwajua wazazi au dini za umpendae?Kuhusu Mpenzi wako wa awali wa dini ya kiislamu. Nadhani itakua ngumu kwa ww kutambulika kama mzazi halali wa mtoto kama toka mwanzo ujajitbulisha kabla hajajifungua au kupata ujauzito. Kwa mujibu wa Dini ya kiislamu Mtoto ni wa mama. Hata ungekua mwislamu ni bado sio mtoto wako hawezi kurithi wala ww kutoa idhni ya kumuozesha. Hata ungekua ww ndio mwislamu na mke wako ndo mkristo. Ni bado mtoto ni wa mama akifariki ni lazma mtoto azikwe kwa dini ya mama. Yao ni kwa mujibu na msimamo wa dini ya kiislamu...
 
Dilek mbona nimechangia[emoji3].
Ha haaa sijaona ngoja nitafute. Ila lazima umemuonea huruma na kumtia moyo..ingekuwa ni mimi nimepost shida zangu nimezaa watoto wa4 kila mmoja baba yake...my friend, ningebanwa humu bila huruma hadi nijinyonge.
 
Ha haaa sijaona ngoja nitafute. Ila lazima umemuonea huruma na kumtia moyo..ingekuwa ni mimi nimepost shida zangu nimezaa watoto wa4 kila mmoja baba yake...my friend, ningebanwa humu bila huruma hadi nijinyonge.

Hapana, ningekutetea bhana.
 
Damu ni Nzito kuliko Maji, km kweli ni wako watakutafuta tu someday..inaweza kua sio leo wala kesho ila watakutafuta tu. Otherwise km una guts nenda kadai watoto wako..wapigie hesabu wakifika 7yrs nenda kawadai.
Anaanzaje kudai kwa haki ipi aliyonayo? Akute tu mume wa bidada akubali kumwachia mtoto, mwingine hamuachii hata kama atahakikisha sio wa kwake wa kumzaa. Mtu kalea mimba, kaoa, kalea mtoto amekuwa mkubwa tayari wametengeneza bond...kwa mtu anayejitambua huyo mtoto hamuachii. Kisheria mtoto ni wa mume.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23] hapo sasa
 
Miaka 31 tu malaya mzoefu hivyo,utapataje sasa mwanamke wa kumuoa,hao uliotusimulia tu wengine si unajaza fuso zima,punguza zinaa ndugu
 
Nadhani mkuu hapa ulipofika shida ni wewe.
Kwanza kuzaa zaa ovyo, na kila mwanamke unayekutana nae sio sawa.

Pili, kila mtu unayezaa naye sjui ninkama unachukulia jambo dogo sana hulipi uzito wake...yani mwanamke familia hazijuani, hakuna nini wala nini...mnadate na kuachana kama viboyfriend na vigirlfriend vya A level wakati hao ni wazazi wenzako...

Sorry to be harsh, but truth gotta be said.

My only advise ni kuwa goig forward usizae zae tu na yeyote unayekutana nae.

Sex does not have to lead to babies all the time. Otherwise tungekuwa tuna watoto kila sehemu kwa idadi isiyomakinika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…