Nimenyoosha mikono juu

Nimenyoosha mikono juu

Unasikia maumivu sasa ni kwa sababu ndio umetoka kwenye hayo matatizo. Ila jipe muda maumivu yataisha tu na akili itatulia utakaa chini we mwenyewe utajua ni maamuzi gani sahihi utatakiwa kufanya ili kuendelea na maisha kwa amani
 
Ila mwanamke mwenye majukumu yake Hana Muda wa kuchat humu. Wewe unashughuli Gani??
 
Mahusiano yenu yalikuaje mwanzo? je ni hali imekuja tu baada ya kuingia kwenye ndoa au redflag zilikuwepo toka mwanzo ila uka ignore?
 
Baada ya kupitia misukosuko mingi kwenye ndoa yangu nimeamua kuja kupumzika nyumbani. Moyo unauma sana mpaka sitamani hata kuinuka kitandani natamani kulala tu, nikilala usiku nikisikia adhana ya saa 11 asubuh moyo unauma nataman kuwe usiku tu tulale tusiamke. Sina namna siwezi kumlazimisha anipende, hanipendi, haoni umuhimu wangu wala hisia na mimi hana.

Kinachoniuma zaidi vitu yangu vyote nimeiacha,, nyumba yangu, biashara yangu nimerudi O ninamtoto mdogo
Sijajua kwa ambao wameshapitia hili walifanyaje wakasahau machungu maisha yakaendelea.
Mpigie huyu Mwanasaikolojia anaitwa
Said Kasege. Atakusaidia sana kukujenga kimawazo na utakuwa mpya
0766862579 na 0622414991
 
Na huo ndio ukweli. Wanawake wanaopenda kuonewa huruma hugawa nyuchi zao hovyo kwa wanaume baki kama shukrani wanapofarijiwa. wakidhani ndio faraja,wanapendwa,wazuri,warembo,hawababaishwi kuna wengine wanawahitaji na kumkomoa mwanaume.

Na hapo ndipo wanapozidisha jeuri na kiburi ndani ya ndoa na mwisho ni muendelezo wa migogoro na mwisho kupewa talaka ua mahusiano kufa. Na wale wafariji hukimbia kukwepa mizigo!

Wanapoambiwa kurekebisha mienendo au tabia zao, huja na madai eti 'wananyanyaswa' katika ndoa au mahusiano. Wanajenga dhana ya kutopendwa na manyanyaso. Wanashindwa kuelewa kuwa mwanaume ndio kiongozi ndani.

Kuna tatizo la kauli na kujiheshimu kwa dada yetu, kumdhihaki mwanaume kwenye tendo la ndoa ni dharau kubwa na kumuondolea uanaume wake. Pole kwake bado kuna cha kujifunza hapa.
 
Unasikia maumivu sasa ni kwa sababu ndio umetoka kwenye hayo matatizo. Ila jipe muda maumivu yataisha tu na akili itatulia utakaa chini we mwenyewe utajua ni maamuzi gani sahihi utatakiwa kufanya ili kuendelea na maisha kwa amani
Kweli
 
Nyanyuka simama jifute vumbi na usonge mbele ni mungu pekee hawezi kukuacha kipindi hiki.....by mwizukulu mgikuru a.k.a mwizukulu babuuuuu
 
Wapendao ni wahanga wakubwa wa mahusiano hasa wanawake.
Hupenda kujifanya wamemove on kumbe moyoni wana vinyongo.

Dada pole sana ila kama alikua hakupend huo si ndio uamuzi mzuri zaidi.?
 
Mahusiano yenu yalikuaje mwanzo? je ni hali imekuja tu baada ya kuingia kwenye ndoa au redflag zilikuwepo toka mwanzo ila uka ignore?
Zilikiwepo ila ndio mtu unataka mume.tu
 
Wewe nawe kilasiku unalalamika wewe tu, nyuzi nyingi umefungua humu kumlalamikia mumeo... Wewe utakua una matatizo tena sana ndiyo maana umeshindwa kuishi na mumeo... Usijione upo perfect sana, na usione watu wanakupa ushauri humu ukadhani umewazidi matatizo ktk ndoa, wanakuchora tu na upuuzi wako... Haya umeondoka umerudi kwenu ukae kwa kutulia mumeo aoe mke mwingine aingize ndani...
 
Siwezi ninawatoto 2
1) miaka 7 baba yake alishafariki
2) ana mwaka 1 wote wananitegemea siwezi fanya chochote kibaya Mungu anisaidie
Pole sana! Jitahidi sana kuomba mno Mungu atakupitisha salama. Najua unapitia wakati mgumu. Putting one foot in front of other.... Keep trying utaona mabadiliko.
 
Siwezi ninawatoto 2
1) miaka 7 baba yake alishafariki
2) ana mwaka 1 wote wananitegemea siwezi fanya chochote kibaya Mungu anisaidie
Mwenyewe kama wewe,nahisi una kheri kidogo,mi alikuwa ananiacha Kwa miez 6 bila huduma ukimuuliza anasema ndo maana nilioa mwalimu....nimeishi nae miaka miwili nimeona nae mara 5.Nilivumilia Kuogopa watu wataongea Nini...but moyo ulivyochoka niligeuka jumla na sikurudi nyuma.Mali zinapita tu,embu jikaze anza 1 na utafika panapostahili ...nilitamani kufa ila nilipowaza watoto na utamu wa debolo....nikasema 🤪.....just move on baby....ninao wawili watoto..miaka 7 na 2 yrs old.Naganga🤜 kazaaa😉😉😉
 
Back
Top Bottom