Satisfy
Senior Member
- Jun 25, 2022
- 147
- 237
Baada ya kupitia misukosuko mingi kwenye ndoa yangu nimeamua kuja kupumzika nyumbani. Moyo unauma sana mpaka sitamani hata kuinuka kitandani natamani kulala tu, nikilala usiku nikisikia adhana ya saa 11 asubuh moyo unauma nataman kuwe usiku tu tulale tusiamke. Sina namna siwezi kumlazimisha anipende, hanipendi, haoni umuhimu wangu wala hisia na mimi hana.
Kinachoniuma zaidi vitu yangu vyote nimeiacha,, nyumba yangu, biashara yangu nimerudi O ninamtoto mdogo
Sijajua kwa ambao wameshapitia hili walifanyaje wakasahau machungu maisha yakaendelea.
Dada acha kuhuzunika sana japokuwa ni ngumu.
The matter is,jaribu kukaa na familia yako then uwasikilize wana mawazo gani then kama kuna uwezekano pia kaa na familia ya upande wa mmeo.
Mwisho wa siku if possible mnaweza pata suluhu ikishindikana basi take easy ww sio wa kwanza kukutokea.
Kingine thread yako haina nyama za kuweza mtu kukupa ushauri ulio sahihi coz humu jf hatujui sababu iliyopelekea adi kuachana.
Suluhu yoyote lazima usikilize pande zote mbili then you come up with a better decisions.
Kwa hiyo inatakiwa tu kuyamaliza kifamilia zaidi lkn sio humu,coz sisi hatujui nan mbaya wa mwenzake.
Dada kaza moyo yataisha tena kiroho safi kabisa mm nna imani iyo, ww sio wa kwanza.