Pole sana mkuu, nadhani shida imeanzia hapa. Je mmeshawekana wazi kuhusu mahusiano yenu?, Je unapowasiliana na hizo namba ngeni una behave vipi?. Huenda ananuna kwa sababu anapopokea hizo simu unamkaripia/unamgombeza, kama ndivyo kaeni muelekezane vizuri kwa upendo, mtaelewana tu na maisha yatasonga mbele. Miongoni mwa taasisi zenye migogoro mikubwa katika dunia ya leo ni taasisi ya ndoa, ndoa nyingi zina migogoro, huenda humu ndani wanaokupa ushauri ya kuachana na huyo mkeo pia wana migogoro kwenye ndoa zao. So tumia hekima kufanya maamuzi badala ya mihemko.
Jiulize kwanza:
1. Chanzo cha tatizo ni nini?
2. Nani chanzo cha tatizo?
3. Je nini kifanyike ili kuondoa mzizi/chanzo cha tatizo?
Ukishapata majibu ya maswali hayo, basi suluhu itakuwa ndani ya uwezo wako.
Wanawake wengi tabia zao zinafanana, kama zipo tofauti ni ndogo sana. Leo utamuacha huyo kesho utampata ambaye ni tatizo zaidi ya huyo.
N.B. Tunapoingia kwenye ndoa tujitahidi kuwa wawazi kwa wenza wetu ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.