Nimeolewa ama nimeoa? Naombeni ushauri

Nakuombea utaratibu wako wa talaka uwende vema Kisha urudi sokoni

Kama mwanaume namuombea mwanaume mwenzangu kuwa utakapo pata talaka tu.

Milango ya mafanikio imfungukie huyo jamaa.

Kuna muda Mungu kabla ya kukupa mafanikio makubwa sana, anaondoka egemeo na tegemeo lako katika maisha

Ili katika ufukara na kukosa upate kujua uhalisia wa watu ili pindi atakapokuinua na kukufanikisha Tena, ujue yupi wa kuishia getini , yupo mwisho jikoni na yupi anapaswa kuingia chumbani
 
Mbona wao huweza kutu hudumia vizuri hata kama hatuna kazi. Mvumilie tu ipo siku atafanikiwa. Unaweza ukaondoka na mambo yasiende vizuri.
 
Fungua mafaili yako ya kumbukumbu. Huku mwekea limbwata ili akupende sana ? Siku zote madhara yake ndiyo hayo hataki kufanya kazi. Rudisha mrejesho ndiyo tupate pakuanzia
 
msaidie kumlea siku nae akipata atakusaidia, kwani kipindi cha nyuma alivokuwa anakuhudumia aliwaza kukuacha kisa wewe ni mzigo kwake?
 
Badae ukisha tafunwa sana, utarudi kwamtaraka wako "Ohoo Mme wangu nisamehe turudi tulee watoto"
 
Pole sana mkuu...
Yasije yakageuka kama yaliyompata mwenzako kwenye movie ya crimony" (2018)
 
I stand for the DEFENCE of our fellow man

Je, haukuwahi kumchezesha michezo ya kupeleka nywele zake kwa fundi?
Hujawahi kumtajia fundi jina la mama yake?
Je, umewahi kukaa naye mkashauriana kama familia au ndo ile mwanamke akishakuwa na financial muscles basi anaweza hata kulinda sungusungu?
 
😆😆 Happy nyu yia
 
Mtego huo,,ruka kojo ukakanyage mavi,,na usikute ulimroga mwenyewe ili asichepuke,dawa zimemzidia unataka mkimbia.
 
Ukimtema tu kesho yake anapata lottery ya bilioni mbili na kazi anaitwa. Utaomba mrudiane. Haki sawa komaa
 
Wewe sio mwanamke Bora! Alikosea kukuoa.
Wanawake wenye upendo wa kweli huwa wanaangaika nae na wanaume zao hadi kieleweke!
Iko hivi wanaume wengi wanapitia changamoto mbali mbali hasa changamoto za kiroho. Ningekuona wa maana sana kama ungeandika umehangaika nae kwenye upande wa rohoni kama kwenda kanisani kwenye maombezi, au wewe mwenyew kumuombea.
Huyo jamaa siku akija kupata msaada wa kiroho na akapona na ukishamwacha huwa wanafanikiwa sana.
Huenda Kalogwa e.t.c mwanaume sio rahisi kukataa kazi tu au kuacha kazi pasipo sababu.
 
👏🏾
 
Hivi Kumbe limbwata ni siriazi mkuu maana Ata mimi kuna yan nashindwa kumsahau
 
Mtego huo,,ruka kojo ukakanyage mavi,,na usikute ulimroga mwenyewe ili asichepuke,dawa zimemzidia unataka mkimbia.
Ndo nimemwambia hapo wanaume wanapitia changamoto mbalimbali zinahitaji mwanamke shupavu ambae anajua pia mambo ya Rohoni sio mwanamke anafurahia kuletewa hela tu! Jamaa pengine kachezewa huko kazini, mizungukoni, ndugu au wanawake/michepuko..e.t.c

Huyo jamaa akipata mtu wa kumsaidia mambo ya rohoni iwe kwenye maombezi au vyovyote kutokana na imani yake atarudi kwenye mstari na Mungu huwa anawainua maradufu watu kama hao.
Huyo jamaa Kalogwa! Tatizo lake ni la rohoni.
 
Muache mtafute mwenye kazi
 
Wewe umeshaamua tayari,ila tatizo lenu ni pesa.Bila shaka uliolewa na mwanamume ambaye hukumpenda kwa dhati,pengine ulipenda kazi yake ama kipato chake.Wanawake wa sampuli hii wanavimelea vya ukahaba ndani yao.wanaweza kufanya chochote mradi wapate pesa.Yupo radhi hata kutoa rushwa ya ngono kwa bosi ili ampatie Fursa Fulani ya kimaisha.Kwenye haya maisha Mungu ndiye hupanga hatma ya Kila jambo,ishi kwa kufanya wema hufahamu ni lini pengine utapata ajali na kupoteza uwezo wako wa kufanya kazi.Fikiria kama ni wewe ndio ungekuwa unafanyiwa hivyo na mwanamume wako?siku akifanikiwa utarudi? Au akijiua unajisikiaje!,nakushauri utafute njia halali za kutafuta kipato ,hata kama utaomba talaka bado utaolewa na kuachika kwa sababu kama hizo
 
lakini ni vema hata huyu dada kaja kuomba ushauri kabla ya maamuzi magumu zaidi, ingawa yapo ambayo ameyaamua tayari.

Naamini akipitia comments kuna kitu atapata,huenda hata yeye alikua gizani pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…