Nimeombwa hela ya kusukia

Nimeombwa hela ya kusukia

Huyu dada nimekutana nae juzi kwenye gari kuja Iringa, nikamtongoza akajishaua shaua mwisho akaniambia nimpe namba ya simu atanijibu tukishaachana stand, nikampa.

Jana akanipigia na kudai amekubali ombi langu ila alishindwa kunijibu uso kwa uso kwa madai ana aibu sana. Sasa wakuu jana hiyo hiyo usiku wakati namtafutia usingizi na vidakika vyangu vya ofa mara akaniomba elfu 30 ya kusukia. Nikaeskutiiiiiiiii, yaani leo leo tu?? Nikaona haina shida, nikamwambia nakutumia kesho, yaani leo.

Sasa tangu saa 3 asubuhi anapiga simu mfululizo kuulizia! Kwani deni? Calls zishafika 67 hapa, nimemblock namba sasa anatumia namba tofauti tofauti eti "bebi mbona kimya sasa?!", mimi huyo????

Sjamuelewa kwakweli
calls 67 mbavu zangu mie
 
Wanaume wa siku hizi majangaaaa sana....Sasa unalalamika nn..usikute ulijinadi saaana ...ooih nipo TRA ooh nimo kwenye list ya ma DC wapya.. Unavyojiweka ndo utakavyochukuliwaaa...Unataka mambo makubwa kumbe Hata ya kodi huna... si ajabu anakuenjoy tu..Maana nujuavyo mwanamke serious hawezi omba pesa haraka ivyoo..Yaani Anakyenjoy Na pesa yako ataila Na humpati
 
Sasa hivi simu yake ya 89 inaita hapa bado niamini ananienjoy???
 
Sorry.. Ivi kutongoza bado ipo..? Mi najua siku hizi baada ya salamu na story mbili tatu mnapanga mkutane lini tena.. Then shughuli inaishia hapo.. Mnamalizana kiutu uzima ati..!!
 
hahaha ao wanaitwa njaa kali mkuu nikum-block tu
 
Ndio leo leo unapofungua account siku hiyo uanza kutumika tuma usiitwe mwanamme suruali
 
Sorry.. Ivi kutongoza bado ipo..? Mi najua siku hizi baada ya salamu na story mbili tatu mnapanga mkutane lini tena.. Then shughuli inaishia hapo.. Mnamalizana kiutu uzima ati..!!
Nilimuingia kikubwakubwa sasa hata hatujapanga kukutana krshaomba pesa!!hivi kweli mademu wa iringa wamekuwa hivi?....hapana,huyu atakuwa miongoni mwa mademu wa dar!!
 
Sasa hivi simu yake ya 89 inaita hapa bado niamini ananienjoy???
Sasa si umpee..kumpenda unampenda ila kutoa fungu ndo balaaa..halafu wanaume wa hivi MNA wivuuu balaaa...kama ulivyowai kutokea nae kawai kukuomba ngoma Droo.Ushauri..bado kiza kuingia nenda.M-pesa Tuma..then ulete mrejesho..Ubahili tu.
 
Bora niwe bahili!
 
mkuu mwambie aibu aliyonayo kwenye kukubali kutongozwa aitumie hiyo hiyo aibu kwenye kuomba omba fedha, kuanzia sasa asione aibu kuitikia ombi LA kutongozwa na awekeze nguvu kwenye kuijenga aibu ya kuomba omba ela, maana ilivyongu ni bora awekeze nguvu hizo za kuomba kwenye kutafuta
 
Sasa si umpee..kumpenda unampenda ila kutoa fungu ndo balaaa..halafu wanaume wa hivi MNA wivuuu balaaa...kama ulivyowai kutokea nae kawai kukuomba ngoma Droo.Ushauri..bado kiza kuingia nenda.M-pesa Tuma..then ulete mrejesho..Ubahili tu.
Halafu sijui kanataka kusukwa au kushonwa!maana kana tunywele tudogo tudogooo
 
Back
Top Bottom