Baada ya takribani siku 35 Nimepata relapse moja Kali Sana nikajichukulia Sheria mkononi,
Mwanzo niliamua kuacha porn na puli kwanza Ila sex niendelee na nakumbuka nilisex Kama Mara sita au Saba hivi Basi, baadae nikahamasika nayo niiache, nikaazimia kufanya sperm retention Kabisa na nikaacha rasmi vyote porn, puli na sex.
Faida nilizopata
Kwangu Mimi nilijona Kabisa nimebadilika hata kazi zangu nilifanya kwa bidii na morali na mafaniko makubwa sana tofauti na mwanzo, kujiamini kwangu kuliongezeka sana Tena sana yaani hadi najishangaa mwenyewe, hata nikipishana na mwanamke sijishauri kumgeukia kumuangalia kwa tamaa za kumpigia puli baadae pia nimegundua kuwa Kumbe MTU unaweza Kabisa Kuishi bila kufanya mapenzi kabisa. Hii inawezekana sana maana nimepata muda wa kuusoma mwili wangu.
Kuanguka kwangu kumetokana na
haka ka ujasiri ka kipumbavu. Niliona nimewin najiamini sana aisee Kumbe napotea nikajisahau nikawa naperuzi mitandaoni bila utaratibu mzuri hasa Instagram naingia page zile mbovu mbovu kule nikiamini siwezi rudia maana najiamini sana maana naona hata iweje puli nilishaachana nayo na hainiwezi tena, Kumbe kiburi kinanipoteza sasa majuzi Tu Hapo, nikaingia page moja nikakutana na picha moja ya utata Kabisa shetani akatabasamu na Mimi nami nikamtabasamia akanisihi nijichujulie Sheria mkononi Basi nikamuitikia kwa kumpigia bao moja la mkono aisee sikutosheka nikapiga tena baade Tena nikarudia hadi siku nne mfululizo, nimejilaumu Sana na nimeumia Sana ,nikaona sina maana kabisa jitahada zangu zote zile nimerudia ushetani,nikajikuta roho inaniuma sana kibaya zaidi maumivu makali ya kichwa, magoti, kiuno na uchovu wa mwili wote na hasira muda wote.
Uamuzi niliochukua
Nimeamua nianze upya baada ya kubaini tatizo ambalo Ni kujiachia sana insta kule nimeamua kujipangia saa na wakati wa kuperuzi, Sitaki kujiachia Tena.
Naamini mwenyezi Mungu yupo nami Tena ktk mwanzo mpya.
Kama nikishindwa pia Hapo Basi nimedhamiria Kabisa Kabisa kufuta Instagram Mara moja baada ya kushindwa Tena.
Wajumbe naomba tuungane tena
Hongera pia mnaoendeleza challenge