Hatari sana man, yani ukiamua kubadili maisha yako unakuwa mtu mwingine kabisa mfano mimi zile shobo nilizokuwanazo kila nikimuona demu anaevutia sahizi sina kabisa, yani hata manzi awe mkali kiasi gani mimi namuona kama nyani tu yuko juu ya mti.
Juzi nimeingia mgahawa flani wa mshkaji wangu uko jirani na chuo flani hivi hapa town nikaagiza msosi mara wakaja madem flani wa mjini wale wanaojionaga top in town.
Walivyoingia hawakusalimia mtu hata mmoja ila wadau mule ndani wakaanza kuwashobokea kwa salamu kibao mixa kuwachekea chekea mimi nimecool tu sina habari na mtu tena mmoja akaja kukaa karibu yangu bila kusalimia namimi sikumsemesha mpaka naondoka pale nikamuaga mchizi kisha mimi yuleeee nikapotea.
Naona kitendo nilichofanya yule demu hakuamini alijiona yeye ni mzuri na wakushobokewa na kila mwanaume.
Sasa jana yule mshkaji wangu akanipigia anasema nilivyoondoka pale wale madem wakaanza kunisema eti huyu kaka alietoka anaonekana anadharau hata sijui anaringia nini.
Mimi nikacheka saaana hahahahah.