Nimeona yote; CCM haitaondoka madarakani kwa kura

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Kwa uwekezaji na mali inazomiliki CCM nchi hii hakuna siku hiki chama kitakubali kuondoa madarakani kwa kura katika uchaguzi.

CCM kukubali kuondoka madarakani ina maana ni kupoteza ukwasi wake wote wa mali kuanzia viwanja, majengo mpaka migodi, sio kupoteza dola tu.
 
Kwa uwezkezaji wa mali inazomiliki CCM nchi hii hakuna siku hiki chama kitakubali kuondoa madarakani kwa kura katika uchaguzi.

Binadamu huwa haishiwi mbinu mbadala za kupambana na hila.Ipo na itapatikana namna tu.Labda siyo binadamu.
 
Kwa uwezkezaji wa mali inazomiliki CCM nchi hii hakuna siku hiki chama kitakubali kuondoa madarakani kwa kura katika uchaguzi.

CCM kukubali kuondoka madarakani ina maana ni kupoteza ukwasi wake wote wa mali kuanzia viwanja, majengo mpaka migodi, sio kupoteza dola tu.
Kwani hivo vitu ni mali binafsi za watu au ni mali za Chama?
Kama ni mali binafsi basi upo sawa ila kama ni mali za Taasisi hawana sababu ya kuwa na hofu
 
CCM ikipoteza madaraka itapoteza udhibiti wa mali zake pia, CCM kinaweza kudhibiti mali zake kupitia dola, chama cha kawaida cha siasa hakiwezi kuwa na mali za biashara au kuzalisha mali, kinaweza kumiliki Ofisi tu. Kuna mali nyingine pia zina utata mkubwa sana kwa sababu zilipatikana enzi za za chama kimoja kwa hiyo zinahesabika kama za umma, hizi zinaweza kunyang'anywa na kurudishiwa serikalini, kuna viwanja vilikuwa vya umma vikaenda CCM kwa njia zisizoeleweka navyo vitarudishwa serikalini CCM ikipoteza dola.
 
Kwa uwezkezaji wa mali inazomiliki CCM nchi hii hakuna siku hiki chama kitakubali kuondoa madarakani kwa kura katika uchaguzi.

CCM kukubali kuondoka madarakani ina maana ni kupoteza ukwasi wake wote wa mali kuanzia viwanja, majengo mpaka migodi, sio kupoteza dola tu.
CCM kukubali kuondoka madarakani ina maana ni kupoteza ukwasi wake wote wa mali kuanzia viwanja, majengo mpaka migodi, sio kupoteza dola tu.
 
CCM ikipoteza madaraka itapoteza udhibiti wa mali zake pia, CCM kinaweza kudhibiti mali zake kupitia dola, chama cha kawaida cha siasa hakiwezi kuwa na mali za biashara au kuzalisha mali, kinaweza kumiliki Ofisi tu. Kuna mali nyingine pia zina utata mkubwa sana kwa sababu zilipatikana enzi za za chama kimoja kwa hiyo zinahesabika kama za umma, hizi zinaweza kunyang'anywa na kurudishiwa serikalini, kuna viwanja vilikuwa vya umma vikaenda CCM kwa njia zisizoeleweka navyo vitarudishwa serikalini CCK ikipoteza dola.
Hayo yote nayajua. Issue ni kwamba hizo mali zipo kwa maslahi ya chama au maslahi ya watu binafsi ndani ya Chama.

Unachokisema ni hofu ya watu binafsi wanaofaidika kupitia mgongo wa Chama. Otherwise hakuna sababu ya kuwa na hofu hata kama hizo mali zitarudishwa chini ya umilki wa serikali. Na in fact bado beneficiary watabaki watu wa mifumo ya Ccm wataendelea kuwepo Serikalini maana sio kwamba CCM wakifukuzwa madarakani, chama kipya kitaajiriwa watu wote maeneo yote.
 
Kwa uwezkezaji wa mali inazomiliki CCM nchi hii hakuna siku hiki chama kitakubali kuondoa madarakani kwa kura katika uchaguzi.

CCM kukubali kuondoka madarakani ina maana ni kupoteza ukwasi wake wote wa mali kuanzia viwanja, majengo mpaka migodi, sio kupoteza dola tu.
Museveni alishasema hadharani kabisa kuwa hawezi kutoka kwa njia ya makaratsi bali atatoka kwa nyundo maana yeye ni kotapini.
 
CCM kukubali kuondoka madarakani ina maana ni kupoteza ukwasi wake wote wa mali kuanzia viwanja, majengo mpaka migodi, sio kupoteza dola tu.
Mali zote zilizokiwepo kabla ya mwaka 1992 ni mali za watanzania wote bila kujali itikadi za chama kwani kipindi kile kila mradi wa chama ulikuwa unategemea nguvu za wananchi.

Kama kingekuwa na uwanja sawa kutoka kwa WATAWALA basi kwa nia njema hizo mali libidi zirudishwe kwenye umiliki wa serikali.
 
CCM ikipoteza madaraka itapoteza udhibiti wa mali zake pia, CCM kinaweza kudhibiti mali zake kupitia dola, chama cha kawaida cha siasa hakiwezi kuwa na mali za biashara au kuzalisha mali, kinaweza kumiliki Ofisi tu. Kuna mali nyingine pia zina utata mkubwa sana kwa sababu zilipatikana enzi za za chama kimoja kwa hiyo zinahesabika kama za umma, hizi zinaweza kunyang'anywa na kurudishiwa serikalini, kuna viwanja vilikuwa vya umma vikaenda CCM kwa njia zisizoeleweka navyo vitarudishwa serikalini CCK ikipoteza dola.
Uko sahihi, na wengi wanaofaidika na hivyo vitega uchumi vya ccm hawana ujanja nje ya mbeleko ya dola. Ccm ikipoteza dola vingi vitafubaa ama hata kufa kama vilivyokufa viwanda na mashirika ya umma.
 
Kwa uwezkezaji wa mali inazomiliki CCM nchi hii hakuna siku hiki chama kitakubali kuondoa madarakani kwa kura katika uchaguzi.

CCM kukubali kuondoka madarakani ina maana ni kupoteza ukwasi wake wote wa mali kuanzia viwanja, majengo mpaka migodi, sio kupoteza dola tu.
Haina mali,ila mali za taifa yaani zakwangu na wewe na yule wamezipa jina feki kama mali za ccm.
 
Ndio,but only after 39 years in power and immense internal pressure. Na wakati wa kuondoka, walikuwa wamechoka na walikuwa wamegawanyika.
KANU pia haikuwahi kumiliki mali kama inazomiliki CCM, Jomo Kenyatta alikuwa busy zaidi kuimarisha utajiri wa familia yake kuliko wa chama.
 
Uko sahihi, na wengi wanaofaidika na hivyo vitega uchumi vya ccm hawana ujanja nje ya mbeleko ya dola. Ccm ikipoteza dola vingi vitafubaa ama hata kufa kama vilivyokufa viwanda na mashirika ya umma.
Watu binafsi pia watajizolea mali zake na hakuna kitu watafanywa, sasa hivi wana cha kuwafanya kwa sababu ya dola kama Rostam alivyony'ang'anywa Magic FM na Channel 10.
 
Back
Top Bottom