Nimepanga nisome open university degree ya ICT, Lakini malalamiko ya watu humu ni Mengi je ni uhalisia?

Utakuja kujuta, katafute chuo kingine chenye walimu wa kueleweka
 
Ukisoma kitu kingine tofauti na fani uliyoajiriwa nayo toka mwanzo, unapoteza mda bure kwa sababu, ukimaliza lazima utachagua moja Kati ya mbili, Kuajiriwa kama mtumishi upya au uendelee na kazi ile ile ya zamani ( means hapa unakuwa umepoteza mda wako bure kabisa for nothing) , soma kwanza sheria za utumishi na shirikisha HRO na katibu wako kabla hujatumbukia kwenye chumba cha vibwengo, vinginevyo labda kama unasoma kwa matumizi yako binafsi.
 
Usijaribu utapotezewa muda , wanasahisha vibayaaaaa uki appeal hakuna lolote, wengi wamefika mahala wame drop
Lasivyo utasoma mpaka ukate tamaaa πŸ˜‚πŸ™ŒπŸΎπŸ˜…
 
Kwa hiyo ulishaanza masomo au ulikuwa unaturusha tu.
 
Kwani mkuu hauwezi kweda chuo kingine tofaut na OUT?
Azingatie huu ushauri, lasivyo tutamsahau, watu wanasoma miaka 5 mpaka 6 pale Bachelor's degree na poa labda kama yuko tayari kutoa pesa.

Malecturer wa pale wana njaa sana, nahisi mishahara yao ni kiduchu au mazoea tu.Chuo cha hovyo sana
 
kusoma soma huku ni uoga maisha, kwa hiyo kazi we tafuta mtaji fanya biashara.
 
Ulichoandika ni kitu sahihi kabisa, ila kwenye upande wa "cheap and easy to access degree" inategemea na nani na nani, ukitaka kunyooka hawashindwi kukuweka miaka 5 mpaka 7 kwa programme ya miaka 3.

Niko pale naongea ninachojua. Usione wanasiasa wanamaliza ndani ya miaka 3 first degree, au miwili Masters kwa wanafunzi wa kawaida vitu haviko hivyo, kuna walimu wanafelisha wazi kabisa, kupewa REPEAT kwao ni kawaida na wanafundisha masomo ya kawaida tu. Ukikoswa kwenye masomo utakaziwa kwenye RESEARCH watahakikisha kama hujiongezi utakaa sana pale chuo, supervisor wako atafuta sababu tu wa kukufanya urudie kazi yako mwaka hadi mwaka unaisha
 
Open University, ni chuo kinachotoa Elimu ya hapa na pale na Elimu mbali mbali.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hakuna shule pale nakuambia niko pale kwa zaidi ya miaka mitano, ningejua ningerisiti paper nichukue D yangu moja niapply vyuo vya kueleweka.

Ni vile tu huwezi kurudisha muda nyuma ila ni moja ya kitu najilaumu, wenzangu walioenda UDOM wamemaliza mwaka juzi, na wao course yao ilikuwa ya miaka 4, yangu pale Open ilikuwa miaka 3
 
Miaka 5 yote unasubiri nini?? Ondoka hapo haraka sana.
 
Usijaribu utapotezewa muda , wanasahisha vibayaaaaa uki appeal hakuna lolote, wengi wamefika mahala wame drop
Lasivyo utasoma mpaka ukate tamaaa πŸ˜‚πŸ™ŒπŸΎπŸ˜…
Wewe unakijua vizuri hiki chuo na kuna swala la kupotea mitihani, swala la uchelewesha matokeo, kiufupi siwezi mshauri mtu yoyote kukisogelea
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…