Nimepata accident mapema asubuhi ya leo

New bumper 400,000
New bonnet 600,000
Wing 200,000
Taa 250,000
Vikorokoro vingine 300,000
Haraka haraka 1,750,000
 
Boda boda ni mapepo kama mapepo mengine....lori limesimama kwenye kivuko, na mimi nikasimama ili tumruhusu dada flani avuke...yule dada akasita...nikamuonyesha ishara avuke, kuna bodaboda ikatoka ilipotoka, mwendo wa shetani...ikanipita kwa upande wa kushoto...tunashukuru yule dada alinusurika...wengine waliokuwa wanataka kuvuka wakaahirisha kwa muda..tukaondoka...

Nawachukia boda boda siyo siri....
Na asubuhi wakitupeleka kazini, wanakuwa wananuka midomo..[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
Pole sana mkuu
 
Kuna siku hizi dual carriageway tumesimama mtu avuke, wakati anavuka bodaboda inakuja mbio kutoka wrong side basi mimi naiona jinsi inavyoenda kumgonga mtu tuliemruhusu avuke aisee nilipiga honi yule mtembea kwa miguu akawa ananishangaa huyu ana kichaa nini, basi kule kushangaa kwake sekunde kadhaa ndio ile boda ikapita alinishukuru sana yule mtu ndio akaelewa kwanini nilikuwa napiga honi! Bodaboda ni janga halafu polisi ni kama wamekubali wamewashindwa!
 
Kusema ukweli boada boda ninawachukia....hala akishagonga mtu kwenye zebra, anakimbia anajichanganya kwenye kijiwe cha wenzake...anasikilizia kama kuna noma...

Kama kuna mazingira yasiyo na ushahidi, boda boda ni wakusukumia tu mtaroni
 
Acha upuuzi
 
Nnayo mkuu nimewapigia simu na kuwatumia picha ila walichonieleza itanipasa nisubiri kwa mwezi mmoja mimi mipango yangu mingi inategemea niwe na gari nasafiri mara kwa mara.
Kwani kabla ya kununua gari hilo ulikuwa unasafirije katika hiyo mipango yako. Sema una bima ya Premier badala ya Comprehensive!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…