#COVID19 Nimepata Chanjo ya Corona nchini Marekani, puuzeni uzushi

#COVID19 Nimepata Chanjo ya Corona nchini Marekani, puuzeni uzushi

Embu funguka mkuu kwa faida ya wengine


Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Unatesa mno...nililia...nilikua na maumiv makali sana ya mwili.kwa siku 4 mfululizo ..maumv kama umeanguka toka juu ...misuli inauma mno...na vichomi mafua makali na kukoa kikohiz kikavu.. nilifka hosp nikahis labda ndo nimeanza kusumbuliwa sukari.. nilijua sukari iko 0..hata kukaa kwa kiti huwez nilimwambia dk chek na ngoma nianze mara 1 dose ..majibu yanakuja toka jionii...dk ananiambia una corona...yaan ulimi ni kama unajikata na ubongo husikii kitu ..nilikua nabugia chumv nifeel wapi had leo nasugulia ulimi pilipili kama inasense hakuna kitu...huez simama even 4min .miguu inauma na kutetemeka mno..misuli ya shingon inauma mno ..ah hapa a corona naiheshm
 
Huyu kakariri sayansi ya kwenye kitabu hataki kwenda na wakati.
Ndiyo elimu ya Bongo hiyo. Hata ukimwamsha usiku wa manane atakutajia hizo hatua. Mwambie sasa hata ajaribu kutengeneza chajo ya kuku! Ila pengine siyo mbumbumbu kiasi tunachodhani. Anajitoa ufahamu ili kumfurahisha aliyemteua. Ni aibu kwa profesa kuongea hivi wakati maelezo yote kuhusu hizi chanjo yamefafanuliwa kwa kina.
 
Hii chanjo mwisho wa siku itakuwa haikwepeki epecially kwa wasafiri wanaovuka mipaka ya Nchi

Kitu ambacho watu hawataki kukisema ni kwamba hakuna ajuaje mpaka sasa kwamba ukishapata tu hizo chanjo hizo mbili baaaasi upo free kutamba huku na huko kwa sababu hutopata C19.
Huwezi kutamba huku na huko bila tahadhari hata kama umechanjwa. Sababu zake zimeshalezwa na zipo wazi. Unaweza ku-gogle.
 
Ndiyo elimu ya Bongo hiyo. Hata ukimwamsha usiku wa manane atakutajia hizo hatua. Mwambie sasa hata ajaribu kutengeneza chajo ya kuku! Ila pengine siyo mbumbumbu kiasi tunachodhani. Anajitoa ufahamu ili kumfurahisha aliyemteua. Ni aibu kwa profesa kuongea hivi wakati maelezo yote kuhusu hizi chanjo yamefafanuliwa kwa kina.
Mule mule mkuu.

Hata mimi nimeona pengine anajua somo, anazuga kutetea kibarua kisiote majani tu.
 
Mwananchi mbona una hasira Kali, chanjo hailazimishwi, hauna haja ya kua na hasira Kali

Lakini Siku ambayo utataka kusafiri nje ya nchi ndio utaona umuhimu wake unless labda kama hauna mpango was kusafiri au utazamia kwa meli, au uamue kubaki Tanzania maisha yako yote hadi kifo,

Tanzania kuna mahali tutabanwa kwenye kona tu, time will tell! Kwa sasahiv acha tuendelee kuwatukana na kuwakejeli ambao wana chanjo its our time, but itafika muda wetu.
Najibu kulingana na kauli za niliemjibu. Nikilazimika kuchanja nitachanja. Ila kwa hiari yangu sichanji. Hata huko zinapotoka wapo watu wasiotaka chanjo.
 
Chanjo sehemu nyingi duniani siyo lazima. Ila baada ya muda itakuja kukulazimu (kumbuka siyo lazima) kuchanjwa. Nahisi kwa watu wanaosafiri nje ya nchi/kwenda kwenye shughuli maalum wanaweza kukwama kama hawajachanjwa. Chukulia mfano wa Hija. Pia pengine kuna nchi zitataka uwe na cheti cha chanjo kabla hujaingia kwenye hizo nchi, kama ilivyo yellow fever. Siyo lazima, lakini unalazimika.
Nikilazimika nitachanja, kama silazimiki sichanji. Simple as that.
 
Huwezi kutamba huku na huko bila tahadhari hata kama umechanjwa. Sababu zake zimeshalezwa na zipo wazi. Unaweza ku-gogle.
Zipi hizo? Kwamba ukichanjwa uendelee kuvaa mask na kukeep distance?

Bottom line is there is a lot of unknown info about these vaccines. Hawasemi hizo dose mbili zitaishiwa nguvu lini au ukishachomwa basi hutohitaji kuchomwa tena
 
Mie natamani sana hao wanaokataa chanjo waugue....huu ugonjwa mie naweza kesha siku nzima nikihadithia jinsi unavyotesa... unanyong'onyeza mno kwa muda mrefu nowonder wazee inawaonda mapema sana..ni mateso makali sana
ilikuchukua mda gani hadi ukarecover?
 
Nimefanikiwa kupata chanjo ya Corona hapa napoishi na kufanya kazi Dallas, Texas. Nimepata dose mbili za sindano kwenye bega ya kwanza tarehe 5 mwezi wa pili na ya pili tarehe 4 mwezi wa tatu. Nimepata chanjo kutoka kampuni ya Moderna. Nilivimba kidogo kwenye bega kwa mara zote lakini sijapata homa kama watu wengine wanapata homa kwenye sindano ya pili.

Chanjo ni muhimu na zinaokoa maisha hasa kwa wale wenye au ambao waliwahi kuwa na pumu, kisukari, wazee, wenye magojwa ya moyo na wamegundua pia wenye type A ya damu nao wanaumwa sana wakipata corona. Asilimia 90% ya watu wakipata hawazidiwi hivyo inawezekana hata wewe umeshapata Corona bila kujua. Lakini baada ya siku 90 unaweza kupata tena na inaweza kuwa mbaya zaidi maana mwili unakuwa hauna nguvu sana. Kwasababu kirusi cha corona kimekaa zaidi ya mwaka kinabadilika ili kiweze kuingia kirahisi kwenye miili yetu hii kitaalamu wanaita variant. Hivyo mpaka sasa kuna variant ya South Africa, England, Brazil na ili ya China. Ya South Africa ndiyo kali kuliko zote na ndiyo imeingia Tanzania kwa sasa na kusababisha watu kufa na kuumwa sana kulinganisha na ile ya mwanzo.

Kwenye kinga kuna kinga nyingi sana cha maana ni upatikanaji, usalama na chanjo kufanya kazi. Kuna vipimo vikubwa viwili vya kuzingatia cha kwanza ni kinga ya chanjo yaani ambayo inazuia mtu kupata Corona lakini cha pili je mtu akipata corona ambaye ana chanjo ataumwa kiasi cha kulazwa au kuzidiwa?. Hii ya south Africa inaonyesha kinga haifanyi kazi vizuri hasa kwa hii chanjo ambayo nchi za Africa inauziwa za Oxford Astrazenica au AZD1222. Hawajatoa data kuonyesha je mtu akiumwa inakuwaje au kinga inakuwaje. Lakini chanjo ya Johnson and Johnson imeonyesha inakinga ya corona ya south Africa kwa asilimia 57% lakini hata ukipata corona ni karibu 100% hautazidiwa. Lakini mpaka sasa HAKUNA MTU ALIYEPATA CHANJO YEYOTE POPOTE NA KUUMWA NA KUZIDIWA KIASI CHA KULAZWA. Hii ina maana gani ni kwamba inawezekana kinga ikawa ndogo lakini watu nhawatapoteza maisha ambao wana chanjo

Tanzania wanaogopa chanjo kama hii niliyopewa kwasababu inatumia technologia ya mRNA ambayo ni ya DNA na wanaogopa eti DNA zetu wazungu watabadilisha. Wakati nimeenda kupata chanjo kulikuwa na wazungu wengi wamepewa chanjo kama yangu sasa sijui hizi habari ni za wapi?!!!. Lakini kuna chanjo ambazo zina technologia kama chanjo za zamani mfano Sputnik V ambayo ni ya Urusi inatumia technologia ya zamani ya chanjo na sasa wamefanya utafiti unaonyesha inakinga aslimia 90%. Lakini hii ina order nyingi hasa huko South America itachukua muda kuipata.

Hivyo ushauri wangu ni kwa serikali kutumia chanjo yeyote kasoro ile ya China ambayo haina data ambazo watu wamezionana kusema zipo sawa. Lakini hii wenzetu wa Kenya, Nigeria, Ghana wamepata chanjo yenyewe inawezekana kinga ni ndogo kwa hii ya south Africa lakini ukipata chanjo corona itakuwa kama mafua ya kawaida haitakuuwa kama sasa hivi. Hivyo nashauri bado ni bora sana kuliko kukaa na kutokufanya maamuzi yeyote. Tukiweza kuweka order hii ya J&J ni zuri kwasababu ni sindano mmoja na inahitaji jokofu la kawaidia kuifadhi.

Tatizo serikali inaweza kusema wataalamu wanachukungaza lakini mpaka sasa hakuna habari yeyote uchunguzi umefika wapi, nani yupo kwenye hiyo team inawezekana ni maneno tu.
Asante sana mkuu kwa kututoa matongotongo.
 
Anahoji kwanini serikali haitaki chanjo huku watu wanapoteza maisha.

Ulivyo na Ego mbaya huoni tunavyopoteza maprof, padres, doctors, lawyers etc kwa mijitu mibinafsi kama nyie.

Black is misfortune, I can agree.
Sua imepoteza wasomi had unakaa chini na kusema Eh Mungu nini hiki...
 
Mimi na ukoo wangu mpana wa huko Mwanza, Mbeya, na marafiki zangu wote waishio mikoa mbalimbali hapa nchini wote tupo salama kabisa wala hatuna wasi, kuumwa mafua hatujaanza leo ni ugonjwa ambao unatushika wakati wa vumbi na pale hali ya hewa inapobadilika (baridi). Hatuhitaji chanjo na maisha yanaendelea kama kawaida, wala hatuhitaji ushauri wa kutumia hayo madude yenu
 
Back
Top Bottom