Tuanzie hapa,
una umri gani?
Una familia inyokutegemea kwa maana ya mke na watoto?
Unachoenda kusomea unahisi kina mantiki ukimaliza?
Una ndoto ya kuishi ulaya?
Sio kwa dharau lakini mshahara wa laki5 ni wa kima cha chini sana kukufanya uache kufuatilia ndoto zako, huo mshahara hata muuza genge anaepata faida ya 20k kwa siku au boda anaingiza kipato zaidi.
Bila kupepesa, ikiwa umejiridhisha, nenda kasome tena kasome kitu cha maana ukimaliza upate kazi huko huko ufanyr vitu vya maana na kuliingizia taifa fedha za kigeni.
Kama umri wako ni chini ya 35, ni sahihi kuchukua risk hiyo hata ukiachana na kazi ya serikali bado una muda wa kupigania ndoto zako....
Tofauti kubwa ya tanzania na majirani, wenzetu wanapeleka sana nguvu kazi nje ya nchi na inawasaidia sana mfano kenya, uganda, nigeria, ghana n.k ifike mahali badala ya vijana kusubiri ajira waende huko magharibi kwenye kazi na fursa fedha wanazopata wawekeze nyumbani.