Saoka
JF-Expert Member
- Oct 23, 2018
- 468
- 682
Habari zenu ndugu zangu,
Mimi ni muhitimu wa chuo kikuu mwaka jana (2019) baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu niliamua kuja kutafuta maisha hapa Dar, kwakweli niliteseka mno kwa muda zaidi ya miezi 8 nipo tu nakula na kulala kwa aunt, sina hili wala lile,, kiukweli nilikuwa naumia sana.
Ndipo ikatokea nikapata mahali walikuwa wanahitaji msimamizi wa nyumba za kulala wageni (Guest house) hapa Dar.
Sasa ndugu zangu changamoto ninazozipata huku ni nyingi mno kwa kuwa mimi ndiye mfuaji wa mashuka na pia mimi ndiye kama mlinzi maana wakati mwingine mtu anaweza kukugongea umpe chumba hata saa 8 usiku na huku bado kipato ni kidogo mno japo nakula na kulala hapa hapa
Duh! Wadau nishaurini mana hata nikisema niache hii kazi inayoninyima usingizi sina popote pa kwenda mara nyingine najihisi mkiwa hasa ninapokumbuka nakujishangaa mno kama ni kweli mimi ndiye nimekuwa hivi
Eee Mungu Baba unitie nguvu kwa kweli