Nimepata kazi ya millioni 10, nifanyeje kuutoroka umasikini?

Anza kwa kuweka akiba kwanza, huku ukitafakari nini cha kufanya. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa, daima ukijituma na kujiongeza. Ishi kama fukara kwa kipindi cha mwanzo, uhakikishe una kama milioni 100 benki, hapo uufanye uamuzi wa busara tunaanza kupambana vipi kuutokomeza umasikini na ujinga ili ccm wasikuburule tena!!
 
Hao wazungu kutoka UN waliopo pale kambi ya ukimbizi nyarugusu wanalipwa $4500 Kwa mwezi Sasa wewe ni NGO gani kigoma ikulipe million kumi Kwa mwezi? Labda ya wachawi na mizimu
Unajua aje naye yuko kiwango cha wazungu? Sidhani kama UN inaangalia mzungu na MTz hasa kama kazi na wajibu ni huo huo.
 
Hv na ww una Amin jobless kapata Kazi ya mil 10, au. Seriously [emoji23]
 
Milioni 10 unaomba Ushauri Mtandaoni jinsi ya Kutoka Umasikini ?? Una Akili kweli Wewe ?
Anza na Kutoomba Ushauri Mitandaoni wa Jinsi ya Kutumia Milioni 10....Kama Kweli Umazipata na Sio just Wishful thinking...!!!

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Agreed 100% . Hata mimi nilikuwa kama ningetoa ushauri basi ningecheza kwenye angle hizi hizi.
ile ya kuingiza BOT-Bond , yes ila mpaka ukiwa na pesa ya kutosha.
 
Bro kweli ww mzima wa akili sio punguani unapata zali la mentali unaleta huo mchongo wako ili iweje hujui binadamu kama wabaya wewe kauzu nini .Omba dua hiyo kazi uipate kwanza na uiweze ,mambo hayo ya kazi ni siri yako usimwage mchele kwenye kuku wengi haya kila la kheri .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…