Nimepata kazi ya millioni 10, nifanyeje kuutoroka umasikini?

Bunge linaandaa bajeti ya mwakani kwa kutumia forecast ya misaada au mapato wanayotarajia kupata .
In business, planning ni kitu cha muhimu sana kuliko hata hela.
 
Chukua ushauri huu muhimu sana utakujenga.
Wekeza kwenye ardhi nje ya hapo ni kilio tu.
Nunua mashamba panda miti, kesho utauza miti utauza viwanja,Jenga nyumba za kupangisha self self achana na nyumba nzima mtihani kumpata mpangaj,Jenga hostel,guest.
Simamia mwenyewe Kama huna mda zijichimbie hizo pesa bank fixed hadi ukipata mda yaani likizo au mkataba ukiisha.
 
Duly noted. Na hii ndiyo ilikuwa plan yangu ila hao wadau walionishauri bonds, hisq na UTT and the like wamenishawishi kuachana na nyumba.

Au mkuu unaonaje?
 
Duly noted. Na hii ndiyo ilikuwa plan yangu ila hao wadau walionishauri bonds, hisq na UTT and the like wamenishawishi kuachana na nyumba.

Au mkuu unaonaje?
Nyumba Inaongezeka thamani daily huku unakula Kodi,ni dhamana ya kukopea ili ufanye biashara,pili unaweza itia sokoni ukapata mtaji baada ya mkataba kuisha.
Kama huna mda wa kusimamia sikushauri kufanya biashara,kazi za wazungu Huwa zipo bize sana plus ma safari kibao semina kibao,mbongo,ndugu lazima akupige tu.
 
Hakuna kazi ya million kumi kenge wewe tena huna hata uzoefu wazungu gani hao wakulipe pesa ndefu hivyo na kwa skills gani ulizonazo.
Ni heri ungeniuliza ni skills gani nilizodemonstrate kwa hawa wazungu kuwashawishi kunipa hii kazi. Huenda ingekusaidia na wewe kunoa skill zako.
Lakini kwakuwa wabongo mnafocus na vitu negative tu. Namimi nakuwa negative, sitakuambia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…