Nimepata mfadhili wa mradi mmoja mkubwa unaoweza kugharimu Tsh billioni 116. Ni mradi gani unaweza kugharimu hizo pesa?

Bro, wanakuchota kisha wanasepa zao, wanajua uko desparate (kimuhemuhe) cha kushika hela plus na njaa kali. Principal za biashara ni sawa kote duniani. Huwezi kuweka hela nyingi sehemu ambayo haina uhakika wa kurudisha pesa. Makampuni yote makubwa yalianza kidogo kidogo.
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri boss, Ila badilisha huo mtazamo. Kesho na kesho kutwa wewe ndio utakua kiongozi wetu. Sasa sijui kama utaweza pata hela za kutekeleza mradi hata mmoja.
 
Nunua boti 2 kubwa za uvuvi baharini, na eneo karibu na pwani unafungua kiwanda cha kuchakata mazao ya samaki minofu, mifupa, mafuta ya samaki. Boti 2 nyingine ziwa Tanganyika kule hakuna zana za kisasa na samaki au dagaa ukikausha unauza DRC uhitaji mkubwa sana.
 
Saizi kwenye makaa ya mawe kuna uhitaji mkubwa wa gari za kubeba makaa ya mawe kutoka Mbinga kwenda Mtwara, Mbinga kwenda Uganda,Rwanda na Kenya.

Nunua trucks zako na trailer za tipper (chinese tractor truck per unit inarange usd 56000 mpaka 57000 na tipper trailer za CIMC Qingdao ni usd 28500 kwa trailer, ukiwa na fleet yako ya truck 20+ utakuwa na project nzuri). Mpaka sasa gari za makaa ya mawe ni shida na wateja kutoka nje wanaongezeka
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri boss, Ila badilisha huo mtazamo. Kesho na kesho kutwa wewe ndio utakua kiongozi wetu. Sasa sijui kama utaweza pata hela za kutekeleza mradi hata mmoja.
Nimesema hayo kwa experience ya miaka 6. Kabla akili haijakaa sawa nilipitia njia hiyo hiyo. Sikatai wafadhili wapo wa projects or investments za dollar million 5-10 ila lazima kuwe na background work kuonyesha umeshaanza na faida ipo.

Kuwa makini tu lakini. Ni maoni yangu sio chuki
 
Huyo mfadhili ni mjinga kiasi gani hadi aahidi hela hizo bila kujua anazipeleka kwenye mradi gani au bila business plan.
Inawezekana mfadhili akawa anataka partnership, na yeye atumike kama mzawa, na amempata kwa njia ambazo ni friendly. Its better kuuliza kuliko ku condemn mkuu. Pia amekwambia aliandika baadhi ya miradi.
Kuna miradi kama ya kuzalisha umeme inaweza kubali lakini kwa nchi zetu na political connect.
Mfano issue kama ya kuzalisha umeme wa nyuklia kama itawezekana kuandaa project itakayokuwa ndani ya limit hiyo. Ingawa miradi hiyo huwa inahitaji hela nyingi zaidi ya hiyo. Kama proposal inafanyika, na wataalamu wakaweza kumtengenezea mtambowa ku fit 40 feet container, uhakika wa soko kuwauzia Tanesco ni mkubwa sanaaa
 
Hongera mkuu Kwa bahati hiyo,
Kwa muda niliyokufutilia nimeona una mawazo mazuri na na makubwa sana
So siwezi kushangaa kuweza kupata watu wa kufinance mawazo yako,
Maana kwa wenzetu wanaangalia uwezo mkubwa wa kufikiri
Kwa upande wangu ningekushauri kuwekeza kwenye sekta
Nishati haswa kwenye Gas Asilia

ambayo naona
-unaipenda na
-Una uzoefu nayo na unailewa
-lakini pia baadhi ya material yake yanapatikana hapa nchini
-Pia Ina uhitaji mkubwa
-vile vile I think was cheap after process
-Lakini pia unaweza kuifanyia ubunifu mkubwa ambao Bado haupo nchini Kwa wingi na Africa na
-Hivyo kukuza uchumi wako na kutoa fursa kwa maelfu ya watu
-na ukakuza uchumi wa nchi yetu

Kufungua kampuni kubwa ktk
Sekta ya Gas Asilia
hapa napendekeza miradi ifuatayo ambayo itabidi iandane
1.Viiwanda vya kubadilisha mifumo ya magari ya petroleum kutumia gas, hapa itabidi ujenge angalau Kila mkoa Kwa kuanzia Ili kiharakisha zoezi

2.Vituo vya kujaza Gas kwenye magari yenye huo mfumo ,hapa itabidi ujenge angalua Kila halmashauri kituo kimoja kikubwa kwa kuanzia,
small project
a)Magari ya kusambaza gas
b)Maeneo au store za kuhifadhi gas kila halmashauri
-but unaweza ukatufuta wauzaji wa jumla kila halmashauri then wao wakusupply kwenye vituo vidogo

Kama mtaji utatosha nashauri pia kuwa na miradi hii
3. Kuwa na eneo kubwa la kuhifadhi akiba ya Gas (I think was Gas hub sijui vizuri ) kutoka Kwa kampuni za uchimbaji au import, ambayo utakuwa na uhakika wa supply ya wateja wako angalau mwenzi mmoja bila kuwakwamisha, pia itkusaidia kuagiza nje endapo uzalishaji wa nchini utasusua

4.Kuwa na kiwanda Cha kuconvert gas yetu mpaka ifikie Hali ya kutumika na kusafirishwa kirahisi (hapa nimeshindwa kutumia ile misamiati yenu but I believe ya understand that process)

5. For the future Kuingia ubia na viwanda mbalimbali vya magari kuja kuasembelly magari yao hapa nchini but kwa sharti la mifumo ya Gas


6.For the future of many years after your co grow global and be stable, unaweza kuanzisha kampuni ya magari ya Gas moja kwa Moja au have two option Gas and electric (hapa kwenye electric unaweza kuingia ubia na magari ya umeme like Tesla endapo umeme utakuja kuwa stable hapa kwetu)
Uwe na utulivu wa kutosha na umakini mkubwa Kwa hao wafadhili na kujiepusha na wanasiasa uchwara
Ni mvivu wa kuandika but kama ushauri na ushieikiano utahitajika zaidi Niko tayari
Nikutakie mafanikio mema mkuu
 
Wazo lako ni zuri sana mkuu, but sera za umeme kwetu zinabadilika sana kulingana na kiongozi aliyepo, serikali Ina mpango wa kuzalisha na ziada so itakapofikia lengo mradi wako unaweza kufa so biashara na wanasiasa ni ngumu
 
Mkuu nashauri pia usikubali kupokewa kwanza ruzuku bila kujua masharti na vigezo vyake na mikataba yake clearly ,
ni muhimu sana kujua namna ya kulinda uhuru wako na umiliki wako kwenye Hilo

Ni Bora upate mkopo wa muda mrefu wenye riba ndogo ambao utalinda uhuru wako na umiliki wako,
Kuna watu wanapotezaga umiliki na uhuru wao kwenye kampuni walizoanzisha wenyewe
So ogeza umakini kwenye Hilo mkuu,
Vinginevyo nazidi kukutakia Kila na la heri
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri boss
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri naahidi kuufanyia kazi ushauri huu kwa asilimia zote 100.
 
Nipo makini boss, yote hayo unayoyasema nayafahamu vizuri. Lakini swala la kutafuta fund ndilo hata viongozi wetu wanafanya, miradi yote unayoona inaendelea ni wao wanatafuta hizo pesa.
 
Nipo makini boss, yote hayo unayoyasema nayafahamu vizuri. Lakini swala la kutafuta fund ndilo hata viongozi wetu wanafanya, miradi yote unayoona inaendelea ni wao wanatafuta hizo pesa.
na ndio kipengele kilipo hapo kwenye kupata funds na watz wengi uwezo wa kushawishi ni mdogo au hatuna elimu ya kutosha kueleza hasa nini tunakusudia kufanya..
 
Kuwa makini isije ikawa wale jamaa wa miradi unapambana unafungua kampuni, wananunua shea, wanataka uweke down payment, ukiweka wanapotea au wanakuja na stolen credit card kudeposit kwenye account yako...nina experience sana na hao jamaa wa hvo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…