Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

[UllMkuu nakupongeza sana kwa ku save hiyo hela mkuu, itabidi uongeza hapo milion 30 ili ununue Scania Mende mkuu ,kwa Arusha unalaza milion 5 au nne kwa mwezi na gari haiendi mbali ni Korongoni au pale Kia kubeba chipping kaka ,ni 114 ,360 manual mkuu mimi najua mzungu mmoja anauzaga yuko Uingereza mkuu, inalipa sana kaka .
Ttzo ni ushuru
 
Wastaafu wote wameweza kuishi kwa kutegemea kilimo
Unajua kilimo cha kusoma na kufanya ni tofauti kabisa.Ni kweli kilimo kinafaida kuu lakini lazima ukubali kuwa si faida ya fasta kama unavyo sisitiza.
Mi naendelea kulima na kufuga na faida kubwa naisubiri kwa kitambo sasa
 
Kama umeweka huu uzi na ukarudi kupata mrejesho nakushauri usipite tena hapa na utulie Kama mwaka maana kila mdau Ana lake mi mwenyewe sina hii hela ila wqnanichanganya
 
Heshima zenu wakuu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, ni Mtanzania nnae ishi nchini ufaransa.

Nimebahatika kupata shillingi mil 50 za kitanzania na nahitaji kuwekeza nchini Tanzania.

Je ni fursa zipi nnazo weza kuzipata Tanzania kuweza ili kuimaximize hii pesa ili niweze kuwa Millionaire ndani ya miaka 10 kutoka sasa.?

Asanteni.

Nunua kiwanya wekeza fensi ili kata manyasi weka kibanda kidogo ili wasiseme hauja kiendeleza. alafu subiria baada ya mwaka mmoja ukiuze kikipanda bei.
 
Heshima zenu wakuu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, ni Mtanzania nnae ishi nchini ufaransa.

Nimebahatika kupata shillingi mil 50 za kitanzania na nahitaji kuwekeza nchini Tanzania.

Je ni fursa zipi nnazo weza kuzipata Tanzania kuweza ili kuimaximize hii pesa ili niweze kuwa Millionaire ndani ya miaka 10 kutoka sasa.?

Asanteni.
Milionea au bilionea?
 
[UllMkuu nakupongeza sana kwa ku save hiyo hela mkuu, itabidi uongeza hapo milion 30 ili ununue Scania Mende mkuu ,kwa Arusha unalaza milion 5 au nne kwa mwezi na gari haiendi mbali ni Korongoni au pale Kia kubeba chipping kaka ,ni 114 ,360 manual mkuu mimi najua mzungu mmoja anauzaga yuko Uingereza mkuu, inalipa sana kaka .
Likipata ajali je si ndo mpunga wote utakua umeishia chini
 
Shule ya bure/bila ada[emoji116]
_________________________

Milionea= Millionaire ~having millions of dollars in cash +assets

Bilionea= Billionaire ~ " billion " " " " + "

hata ukiwa na madafu yetu inatakiwa u- convert to USD then utaingia kwenye hizo rank, virtually sidhani km kuna billionaire Tanzania.
Mohammed Dewji ni Billionare. As at 08-jan-2017 his net worth is $1.42 Billion (source: Forbes)

Mohammed Dewji
 
unataka kuwa milionea au bilionea kama lengo lako ni kuwa bilionea badilisha heading ila kama ni kuwa milionea tayari lengo lako limetimia kuwa na milion 50 wewe tayari ni milionea........Nitarudi na wazo baadae kama unataka kuwa bilionea
 
Kwan kuwa millionaire inabid uwe na million ngap?

Kwa definition ya haraka ya maths.. ni zaidi tu ya milioni moja kwenda juu..

Yaani ukiwa na 1,000,000.0001 tayari ww ni milionear..!!

So, Milioni 1, 2, 3, 4......bilioni 1, 2, 3, 4.... Trillioni 1, 2, 3 ... na kuendelea

Pesa haina mwisho..
 
chukua milion tisa fanya biashara ya viwanja kwa kununua na kuuza, kanunue viwanja vya milion tatu vitatu kisha uza kwa milion tano. then chukua milion tano kalime tangawizi eka tatu. zilizobaki ziache bank kwanza mpaka ukomae na ujifunze zaidi ndo uongeze mtaji.
 
Njoo tuwekeze kwenye biashara ya miti kaka... Unanunua shamba lako ekari kadhaa, tunapanda pines kila ekari miti 600.. baada ya miaka kumi na mbili wewe unagongagonga mguu chini na kupiga kamluzi kwa mbali.. ikikomaa kwa sasa mti mmoja si chini ya 20,000.. na mashamba yapo hadi shilingi 100,000 kwa eka Njombe. Mimi nina eka 10 tayari.. Muhimu kuweka fire breaks na kufanya prunning kwa wakati.. huhitaji kugombana na mtu
 
1) Wekeza kwenye mashamba ya miti ukipata ekari zako 30 - 50 za miti, baada ya miaka kumi utakuwa na 35, ukivuna utakuwa milionea
2) Nunua shamba eneo la jirani na mjini kama ekari 5 au 10, weka maji shambani na mifumo ya maji kwa kilimo cha umwagiliaji na fanya kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga, matunda n,k mwaka mzima, pesa yako itazunguka vizuri kabisa.
 
Back
Top Bottom