Nimepata mshtuko mkubwa Ubungo Bus Terminal leo alfajiri!

Nimepata mshtuko mkubwa Ubungo Bus Terminal leo alfajiri!

Nilienda hapo jana mdada ananikingia mikono nitoe kiingilio, niliwaza sana nalipia kitu gani hapo! Niliamua kumwambia huyo dada nasafiri na nikapitiliza bila cha kuonyesha tiketi wala nini, hivi pale mtu unalipia nini? Na wanaotoza hela hawaoni hata aibu!!!!
Aibu mbele ya pesa?
 
 
Ilikuwa ni saa kumi na robo alfajiri ya leo, mlio wa simu yangu unanikurupusha toka usingizini, nakumbuka nina appointment ya kumfuata bibi yangu nyumbani alikokuwa amefikia na kumpeleka Ubungo bus terminal tayari kwa safari ya kurudi Kondoa.

Ile naingia pale getini tu, nikapigwa na butwaa nisijue ni wapi hapa nimeingia, nikajiuliza, hivi hii ndio stendi kubwa kabisa ya mabasi ya masafa marefu Afrika mashariki na kati?! Au ni stendi ya daladala ya mabasi ya Tandale kwa mfuga mbwa??!

Wingi na ukubwa wa mabasi ambayo kwa hesabu ya haraka haraka yanaweza kufika kati ya 500 - 1000 yaliyokuwa yamepaki iliniondolea shaka niliyokuwa nayo, hakika haya ni mabasi ya mikoani na si mabasi yaendayo Tandale kwa mfuga mbwa.

Wakati natafakari mshtuko nilioupata ghafla mbele nakutana na bwawa kubwa la maji kwenya parking ya magari binafsi, probably limetokana na mvua iliyonyesha usiku wa jana, yaani ni aibu, aibu, aibu, aibu! hata pakushukia hakuna, ikabidi nivue viatu na kukunja suruali ndio nikashuka, nikamfuata bibi upande wake na kumpa mgongo huku nikichutama kidogo, akapanda mgongoni na nikamvusha hadi kwenye sehemu kavu.

Kimbembe sasa kikawa kwenye kulitafuta basi lake la Kondoa, huku nikizongwa zongwa na wakaka wenye vitoroli vya ajabu ajabu vya matairi mawili wakijitolea kubeba mizigo, walini- harass mno; ni ajabu lakini ukweli ni kwamba hakuna kibao hata kimoja cha ku-guide abiria kwamba lot ipi ni ya mabasi ya wapi, mandhari ya kituo chenyewe ni kama soko la samaki, literally kituo hakina tofauti na Buguruni sokoni mule ndani, its absolute chaos and totally filthy, uchafu uchafu wa matope, hakuna shed za watu kusubiria wageni wao, yaani hakuna chochote, yaani ukisikia kurogwa ndio huku maana hakuna explanation nyingine.

Wakati naingia kulikuwa na foleni, lakini foleni ya kutoka ndio ilikuwa balaa, barabara kama vichochoro vya Vingunguti na mashimo kama tuko torabora, huu ni utani, mimi nawaambia ukweli haya ni matusi ya nguoni kwa wana Dar, hamtaamini kilichopo mule, jaribuni kama mmepotea njia muingie mule. Pale getini sasa kuna kadada kamekomaa kukusanya mapato, hata sijui wanazifanyia nini hizo hela, sijaona hata choo kimoja kwa ajili ya wageni, watu 15,000 wanaopitia hapo kila siku na hakuna choo, this is ridiculous!

Nilitokea kule kwa nyuma njia inayotokezea Shekilango, kule ndio kituko kabisa, huwezi amini ile ndio barabara inayotokea kituo kikubwa kama kile. Hivi ule mpango wa kuhama upo? Mbona mi sielewi?
=================================
Update: 21/02/2019
Kilio cha bibi kimesikika.
Hatimaye ujenzi wa stendi umeanza mbezi.
Hatimaye ujenzi wa stendi ya mabasi (Mbezi Luis) yaendayo mikoani yaanza kujengwa - JamiiForums


=================================
Update: 29/06/2019


________________________________

UNGEENDA NA BAJAJI HIZI KELEEE ZISINGEKUWEPO
 
 
Stand ya ubungo ni takataka kabisa sijui watawala wanawaza nini
 
Back
Top Bottom