Ubungo Bus Terminal,
Hiyo ni moja tu, Kati ya sehemu nyingi za hovyo za Dar Ninayoifahamu.
Nimezaliwa Dar,
Nimekulia Dar,
Nimesoma na Kuhitimu Dar,
Buguruni, Mbagala,Kiwalani,Vingunguti,Kilungule,Mzinga,Temeke,Kwa Azizi Ally, Ubungo,Tabata, Posts,Kimara,Mbezi,Kibamba, Kkoo, Kongowe, Msasani, Kinondoni, Sinza, M,burahati, Manzese,Jangwani, Kigogo, Magomeni, Mwenge, Mikocheni,Kawe, Makonde, Mbezi Beach, Tegeta, Bunju, Mbweni, Hadi Nyumbani Ununio kote nimeishi na kupita kwa namna moja au nyingine.
Kiukweli Dar ni zaidi ya uchafu,
Dar ni zaidi ya Jehannamu,
Dar ni zaidi ya Kaburi,
Jiji la hovyo sana,
Inashangaza linavyosifiwa sana, Inashangaza zaidi watu wa mikoani wanavyolilia kuja Dar.
Rate ya magonjwa ya milipuko na kuambukizana Kwa Dar ni kubwa,
Moshi wa magari, Hewa chafu, Taka taka na uvundo, Wingi wa watu, Imefanya hewa izidi kuwa nzito hasa katikati ya jiji.
Hata Yote nimekuja kugundua baada ya kutoka nje ya dar kwa Mara ya kwanza, Kuna sehemu nzuri sana Tanzania hii,
Nimeajiriwa Mkoa wa Rukwa, Hewa Safi, Miti ya kutosha, Ubaridi mzuri, Maisha Nafuu, Kuna kila aina ya vyakula.
Sikuwahi kuijua Chinese, Mboga tamu kuliko mchicha,
Sikuwahi kuona karanga zikichanganywa kwenye Mboga ila huku ni zaidi.
Kiukweli mikoani kuna Maisha mazuri zaidi, Hii ni kwa wale watu wanaojitambua.
Ardhi safi yenye rutuba imenishawishi ninunue shamba nilimishe, ingawa sijui kulima.
Tanzania ni Kubwa,
Tanzania ni zaidi ya Dar,
Ni wakati wa Mikoa mingine kuinuliwa kiuchumi, Wa Dar waachieni Dar yao.