Nimepata mshtuko mkubwa Ubungo Bus Terminal leo alfajiri!

Kwanza ubungo hayawez kaa mabasi 500-1000 kama ulivoandika mule basi nyingii saaana labda 80.
 
Nimetoka hapo asubuhi pako hivyo sana. Wakati nakaguliwa tiketi mkaguzi, basi na Mimi wote tulikuwa tumesimama kwenye maji na matope
 
Ilikuwa ni saa kumi na robo alfajiri ya leo, mlio wa simu yangu unanikurupusha toka usingizini, nakumbuka nina appointment ya kumfuata bibi yangu nyumbani alikokuwa amefikia na kumpeleka Ubungo bus terminal tayari kwa safari ya kurudi Kondoa.

Ile naingia pale getini tu, nikapigwa na butwaa nisijue ni wapi hapa nimeingia, nikajiuliza, hivi hii ndio stendi kubwa kabisa ya mabasi ya masafa marefu Afrika mashariki na kati?! Au ni stendi ya daladala ya mabasi ya Tandale kwa mfuga mbwa??!

Wingi na ukubwa wa mabasi ambayo kwa hesabu ya haraka haraka yanaweza kufika kati ya 500 - 1000 yaliyokuwa yamepaki iliniondolea shaka niliyokuwa nayo, hakika haya ni mabasi ya mikoani na si mabasi yaendayo Tandale kwa mfuga mbwa.

Wakati natafakari mshtuko nilioupata ghafla mbele nakutana na bwawa kubwa la maji kwenya parking ya magari binafsi, probably limetokana na mvua iliyonyesha usiku wa jana, yaani ni aibu, aibu, aibu, aibu! hata pakushukia hakuna, ikabidi nivue viatu na kukunja suruali ndio nikashuka, nikamfuata bibi upande wake na kumpa mgongo huku nikichutama kidogo, akapanda mgongoni na nikamvusha hadi kwenye sehemu kavu.

Kimbembe sasa kikawa kwenye kulitafuta basi lake la Kondoa, huku nikizongwa zongwa na wakaka wenye vitoroli vya ajabu ajabu vya matairi mawili wakijitolea kubeba mizigo, walini- harass mno; ni ajabu lakini ukweli ni kwamba hakuna kibao hata kimoja cha ku-guide abiria kwamba lot ipi ni ya mabasi ya wapi, mandhari ya kituo chenyewe ni kama soko la samaki, literally kituo hakina tofauti na Buguruni sokoni mule ndani, its absolute chaos and totally filthy, uchafu uchafu wa matope, hakuna shed za watu kusubiria wageni wao, yaani hakuna chochote, yaani ukisikia kurogwa ndio huku maana hakuna explanation nyingine.

Wakati naingia kulikuwa na foleni, lakini foleni ya kutoka ndio ilikuwa balaa, barabara kama vichochoro vya Vingunguti na mashimo kama tuko torabora, huu ni utani, mimi nawaambia ukweli haya ni matusi ya nguoni kwa wana Dar, hamtaamini kilichopo mule, jaribuni kama mmepotea njia muingie mule. Pale getini sasa kuna kadada kamekomaa kukusanya mapato, hata sijui wanazifanyia nini hizo hela, sijaona hata choo kimoja kwa ajili ya wageni, watu 15,000 wanaopitia hapo kila siku na hakuna choo, this is ridiculous!

Nilitokea kule kwa nyuma njia inayotokezea Shekilango, kule ndio kituko kabisa, huwezi amini ile ndio barabara inayotokea kituo kikubwa kama kile. Hivi ule mpango wa kuhama upo? Mbona mi sielewi?

Pole kwa mshituko mkuu.

Siku nyingine mpeleke akapande basi Morogoro pale Msamvu Bus Terminal. Ni ya kisasa zaid
pic+msamvu+airport.jpg

msamvu-4.jpg

imgs9339-jpg-jpeg.538458

img_20170707_124158-jpg.538465

msamvu-5.jpg

msamvu-10.jpg

msamvu-7.jpg

bcccb-Msamvu.jpg
 
Next time wapokee wageni wako wewe mwenyewe ili usishtuke wakati wa kuwarudisha.
Karibu Dar es Salaam, jiji la raha na karaha.
 
Ilikuwa ni saa kumi na robo alfajiri ya leo, mlio wa simu yangu unanikurupusha toka usingizini, nakumbuka nina appointment ya kumfuata bibi yangu nyumbani alikokuwa amefikia na kumpeleka Ubungo bus terminal tayari kwa safari ya kurudi Kondoa.

Ile naingia pale getini tu, nikapigwa na butwaa nisijue ni wapi hapa nimeingia, nikajiuliza, hivi hii ndio stendi kubwa kabisa ya mabasi ya masafa marefu Afrika mashariki na kati?! Au ni stendi ya daladala ya mabasi ya Tandale kwa mfuga mbwa??!

Wingi na ukubwa wa mabasi ambayo kwa hesabu ya haraka haraka yanaweza kufika kati ya 500 - 1000 yaliyokuwa yamepaki iliniondolea shaka niliyokuwa nayo, hakika haya ni mabasi ya mikoani na si mabasi yaendayo Tandale kwa mfuga mbwa.

Wakati natafakari mshtuko nilioupata ghafla mbele nakutana na bwawa kubwa la maji kwenya parking ya magari binafsi, probably limetokana na mvua iliyonyesha usiku wa jana, yaani ni aibu, aibu, aibu, aibu! hata pakushukia hakuna, ikabidi nivue viatu na kukunja suruali ndio nikashuka, nikamfuata bibi upande wake na kumpa mgongo huku nikichutama kidogo, akapanda mgongoni na nikamvusha hadi kwenye sehemu kavu.

Kimbembe sasa kikawa kwenye kulitafuta basi lake la Kondoa, huku nikizongwa zongwa na wakaka wenye vitoroli vya ajabu ajabu vya matairi mawili wakijitolea kubeba mizigo, walini- harass mno; ni ajabu lakini ukweli ni kwamba hakuna kibao hata kimoja cha ku-guide abiria kwamba lot ipi ni ya mabasi ya wapi, mandhari ya kituo chenyewe ni kama soko la samaki, literally kituo hakina tofauti na Buguruni sokoni mule ndani, its absolute chaos and totally filthy, uchafu uchafu wa matope, hakuna shed za watu kusubiria wageni wao, yaani hakuna chochote, yaani ukisikia kurogwa ndio huku maana hakuna explanation nyingine.

Wakati naingia kulikuwa na foleni, lakini foleni ya kutoka ndio ilikuwa balaa, barabara kama vichochoro vya Vingunguti na mashimo kama tuko torabora, huu ni utani, mimi nawaambia ukweli haya ni matusi ya nguoni kwa wana Dar, hamtaamini kilichopo mule, jaribuni kama mmepotea njia muingie mule. Pale getini sasa kuna kadada kamekomaa kukusanya mapato, hata sijui wanazifanyia nini hizo hela, sijaona hata choo kimoja kwa ajili ya wageni, watu 15,000 wanaopitia hapo kila siku na hakuna choo, this is ridiculous!

Nilitokea kule kwa nyuma njia inayotokezea Shekilango, kule ndio kituko kabisa, huwezi amini ile ndio barabara inayotokea kituo kikubwa kama kile. Hivi ule mpango wa kuhama upo? Mbona mi sielewi?
Ninaamini kwamba chama cha kutetea haki za abiria kimekusikia.
 
Hahaha maskini bibi wa watu hadi hurumaa..... sasa zile mia mbili wanazichaji kwa ajili ya nini au siku hizi wameacha kuchaji??
 
meya wa ubungo boniphace jacob hili linakuhusu.
Wengi walikuwa hawataki kunijibu hili, Asante mkuu. Mimi ni wa mkoani huku, halmashauri za Dar sizijui. Ila huku halmashauri yetu inajipanga kujenga stendi yetu ili kuiongezea mapato halmashauri.
 
Back
Top Bottom