Pompey
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 399
- 241
There you are mkuu, ukiwa humo ndani maisha yanaenda vizuri sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
There you are mkuu, ukiwa humo ndani maisha yanaenda vizuri sana
Hapo utamlaumu Magufuli, utafikiri ndio aliyekusababishia mshtuko mkubwa leo asubuhi.
Hii itakuwa Morogoro
Hauna tofauti na uwanja wa mnada wa ng'ombe, kuna haja gani ya kuchukua ushuru sehemu isipo na maboreshi hata wageni utushangaa sehemu ambayo inabeba Magari yenye thamani zaidi ya bilioni 200 kwa siku. Inakosa stand ya kisasa ambayo hata gharama yake haifiki bilioni 100.Tupambane na maendeleo tuache kupambana na watu.Ipo haja ya kuugeuza uwanjwa wa mpira wa miguu kuwa stendi kuu ya mabasi ya mikoani... Itakuwa ni manufaa makubwa kuliko ulivyo kaa kaa kihasara sasa hivi.
Yaani mtu anaenda Kondoa apande Ndege ya Mbeya? Utakuwa hujui Jogorafia wewe!Next time, mpandishe bibi kwenye bombardier mpaka Mbeya then aendelee kwa bus!
[emoji39] [emoji39] [emoji39]
"Dreva wa lori"Hapo utamlaumu Magufuli, utafikiri ndio aliyekusababishia mshtuko mkubwa leo asubuhi.
Atapanda bus la mbeya arushakondoa unapitia mbeya;;; weita ongeza balimi nakuja kulipa
Ifike pahala tuwe sehemu ya suluhusho na sio kulalama tu. Ushauri wako ni upi kwa mamlaka husika?Ilikuwa ni saa kumi na robo alfajiri ya leo, mlio wa simu yangu unanikurupusha toka usingizini, nakumbuka nina appointment ya kumfuata bibi yangu nyumbani alikokuwa amefikia na kumpeleka Ubungo bus terminal tayari kwa safari ya kurudi Kondoa.
Ile naingia pale getini tu, nikapigwa na butwaa nisijue ni wapi hapa nimeingia, nikajiuliza, hivi hii ndio stendi kubwa kabisa ya mabasi ya masafa marefu Afrika mashariki na kati?! Au ni stendi ya daladala ya mabasi ya Tandale kwa mfuga mbwa??!
Wingi na ukubwa wa mabasi ambayo kwa hesabu ya haraka haraka yanaweza kufika kati ya 500 - 1000 yaliyokuwa yamepaki iliniondolea shaka niliyokuwa nayo, hakika haya ni mabasi ya mikoani na si mabasi yaendayo Tandale kwa mfuga mbwa.
Wakati natafakari mshtuko nilioupata ghafla mbele nakutana na bwawa kubwa la maji kwenya parking ya magari binafsi, probably limetokana na mvua iliyonyesha usiku wa jana, yaani ni aibu, aibu, aibu, aibu! hata pakushukia hakuna, ikabidi nivue viatu na kukunja suruali ndio nikashuka, nikamfuata bibi upande wake na kumpa mgongo huku nikichutama kidogo, akapanda mgongoni na nikamvusha hadi kwenye sehemu kavu.
Kimbembe sasa kikawa kwenye kulitafuta basi lake la Kondoa, huku nikizongwa zongwa na wakaka wenye vitoroli vya ajabu ajabu vya matairi mawili wakijitolea kubeba mizigo, walini- harass mno; ni ajabu lakini ukweli ni kwamba hakuna kibao hata kimoja cha ku-guide abiria kwamba lot ipi ni ya mabasi ya wapi, mandhari ya kituo chenyewe ni kama soko la samaki, literally kituo hakina tofauti na Buguruni sokoni mule ndani, its absolute chaos and totally filthy, uchafu uchafu wa matope, hakuna shed za watu kusubiria wageni wao, yaani hakuna chochote, yaani ukisikia kurogwa ndio huku maana hakuna explanation nyingine.
Wakati naingia kulikuwa na foleni, lakini foleni ya kutoka ndio ilikuwa balaa, barabara kama vichochoro vya Vingunguti na mashimo kama tuko torabora, huu ni utani, mimi nawaambia ukweli haya ni matusi ya nguoni kwa wana Dar, hamtaamini kilichopo mule, jaribuni kama mmepotea njia muingie mule. Pale getini sasa kuna kadada kamekomaa kukusanya mapato, hata sijui wanazifanyia nini hizo hela, sijaona hata choo kimoja kwa ajili ya wageni, watu 15,000 wanaopitia hapo kila siku na hakuna choo, this is ridiculous!
Nilitokea kule kwa nyuma njia inayotokezea Shekilango, kule ndio kituko kabisa, huwezi amini ile ndio barabara inayotokea kituo kikubwa kama kile. Hivi ule mpango wa kuhama upo? Mbona mi sielewi?
Hivi Kwa nini kusiwe na terminal tatu za wilayani Temeke, Ilala na Kinondoni? Ubungo imekuwa ganzi kwenye akili za wahusika miaka nenda-rudi na watu hawana ubunifu, wanatesa abiria bure tu!Ilikuwa ni saa kumi na robo alfajiri ya leo, mlio wa simu yangu unanikurupusha toka usingizini, nakumbuka nina appointment ya kumfuata bibi yangu nyumbani alikokuwa amefikia na kumpeleka Ubungo bus terminal tayari kwa safari ya kurudi Kondoa.