Nimepata mshtuko mkubwa Ubungo Bus Terminal leo alfajiri!

yani kituo cha daladala cha mawasiliano kina international standards everything is just perfect hata wakora hamna
iyo bullshit ya ubungo terminal cjui kwanini wasiifanye soko la ndizi na kuku
ndo maana campany kubwa kama kilimanjaro wameanzisha office zao wenyew
 
Mkuu ulikuwa ukiishi nje ya nchi, umerudi hivi Karibuni kwa pipa au ni mkazi wa kawaida wa Dar? Mbona Dar yote iko hivyo hata Posta madimbwi tu. Miundombinu huko ni changamoto.
 
Hata mitaani madimbwi tu.

54F76ADF-8C2D-4BF8-8987-30EDD75FA452.jpeg
 
nilijua labda ulitaka kubakwa, au umekuta polisi anaibiwa na kibaka.
 
Hapana umhimu hapo,pesa nyingi zinatakiwa kutumika kulinda nchi kwa kuwalipa vizuri Polisi ili wapate moyo wa kuteka,kutesa na kuua wapinzani,hivyo pambana na hali yako.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
muongo mkubwa..kwani ilikua lazima upaki gari hapo kwenye maji tuu
 
Huko unakokuita tandale kwa mfugambwa kumbuka wanaishi watu ambao tumeridhika na maisha yetu
 
Ilikuwa ni saa kumi na robo alfajiri ya leo, mlio wa simu yangu unanikurupusha toka usingizini, nakumbuka nina appointment ya kumfuata bibi yangu nyumbani alikokuwa amefikia na kumpeleka Ubungo bus terminal tayari kwa safari ya kurudi Kondoa.

Ile naingia pale getini tu, nikapigwa na butwaa nisijue ni wapi hapa nimeingia, nikajiuliza, hivi hii ndio stendi kubwa kabisa ya mabasi ya masafa marefu Afrika mashariki na kati?! Au ni stendi ya daladala ya mabasi ya Tandale kwa mfuga mbwa??!

Wingi na ukubwa wa mabasi ambayo kwa hesabu ya haraka haraka yanaweza kufika kati ya 500 - 1000 yaliyokuwa yamepaki iliniondolea shaka niliyokuwa nayo, hakika haya ni mabasi ya mikoani na si mabasi yaendayo Tandale kwa mfuga mbwa.

Wakati natafakari mshtuko nilioupata ghafla mbele nakutana na bwawa kubwa la maji kwenya parking ya magari binafsi, probably limetokana na mvua iliyonyesha usiku wa jana, yaani ni aibu, aibu, aibu, aibu! hata pakushukia hakuna, ikabidi nivue viatu na kukunja suruali ndio nikashuka, nikamfuata bibi upande wake na kumpa mgongo huku nikichutama kidogo, akapanda mgongoni na nikamvusha hadi kwenye sehemu kavu.

Kimbembe sasa kikawa kwenye kulitafuta basi lake la Kondoa, huku nikizongwa zongwa na wakaka wenye vitoroli vya ajabu ajabu vya matairi mawili wakijitolea kubeba mizigo, walini- harass mno; ni ajabu lakini ukweli ni kwamba hakuna kibao hata kimoja cha ku-guide abiria kwamba lot ipi ni ya mabasi ya wapi, mandhari ya kituo chenyewe ni kama soko la samaki, literally kituo hakina tofauti na Buguruni sokoni mule ndani, its absolute chaos and totally filthy, uchafu uchafu wa matope, hakuna shed za watu kusubiria wageni wao, yaani hakuna chochote, yaani ukisikia kurogwa ndio huku maana hakuna explanation nyingine.

Wakati naingia kulikuwa na foleni, lakini foleni ya kutoka ndio ilikuwa balaa, barabara kama vichochoro vya Vingunguti na mashimo kama tuko torabora, huu ni utani, mimi nawaambia ukweli haya ni matusi ya nguoni kwa wana Dar, hamtaamini kilichopo mule, jaribuni kama mmepotea njia muingie mule. Pale getini sasa kuna kadada kamekomaa kukusanya mapato, hata sijui wanazifanyia nini hizo hela, sijaona hata choo kimoja kwa ajili ya wageni, watu 15,000 wanaopitia hapo kila siku na hakuna choo, this is ridiculous!

Nilitokea kule kwa nyuma njia inayotokezea Shekilango, kule ndio kituko kabisa, huwezi amini ile ndio barabara inayotokea kituo kikubwa kama kile. Hivi ule mpango wa kuhama upo? Mbona mi sielewi?
Choo kipo, ila ww inaonekana sio mtumiaji mzuri wa hii stend ya ubungo....ndio maana umepata huo mshtuko. Ila naungana na ww stend haieleweki yaan kwa mgeni anapata tabu sana kujua wapi pa kutokea na kama amefuatwa mfano ww hukujua mabasi ya kondoa wapi yalipo... Kingine ndio hiko pa kukosekana kwa mahali pa kupumzikia hakuna hata vibanda vya kupumzika au kujikinga na jua au mvua.....wale mawakala wa magar nao wanaboa sana yaan stend inashindwa na ile ya dodoma au mbeya au morogoro
 
Ilikuwa ni saa kumi na robo alfajiri ya leo, mlio wa simu yangu unanikurupusha toka usingizini, nakumbuka nina appointment ya kumfuata bibi yangu nyumbani alikokuwa amefikia na kumpeleka Ubungo bus terminal tayari kwa safari ya kurudi Kondoa.

Ile naingia pale getini tu, nikapigwa na butwaa nisijue ni wapi hapa nimeingia, nikajiuliza, hivi hii ndio stendi kubwa kabisa ya mabasi ya masafa marefu Afrika mashariki na kati?! Au ni stendi ya daladala ya mabasi ya Tandale kwa mfuga mbwa??!

Wingi na ukubwa wa mabasi ambayo kwa hesabu ya haraka haraka yanaweza kufika kati ya 500 - 1000 yaliyokuwa yamepaki iliniondolea shaka niliyokuwa nayo, hakika haya ni mabasi ya mikoani na si mabasi yaendayo Tandale kwa mfuga mbwa.

Wakati natafakari mshtuko nilioupata ghafla mbele nakutana na bwawa kubwa la maji kwenya parking ya magari binafsi, probably limetokana na mvua iliyonyesha usiku wa jana, yaani ni aibu, aibu, aibu, aibu! hata pakushukia hakuna, ikabidi nivue viatu na kukunja suruali ndio nikashuka, nikamfuata bibi upande wake na kumpa mgongo huku nikichutama kidogo, akapanda mgongoni na nikamvusha hadi kwenye sehemu kavu.

Kimbembe sasa kikawa kwenye kulitafuta basi lake la Kondoa, huku nikizongwa zongwa na wakaka wenye vitoroli vya ajabu ajabu vya matairi mawili wakijitolea kubeba mizigo, walini- harass mno; ni ajabu lakini ukweli ni kwamba hakuna kibao hata kimoja cha ku-guide abiria kwamba lot ipi ni ya mabasi ya wapi, mandhari ya kituo chenyewe ni kama soko la samaki, literally kituo hakina tofauti na Buguruni sokoni mule ndani, its absolute chaos and totally filthy, uchafu uchafu wa matope, hakuna shed za watu kusubiria wageni wao, yaani hakuna chochote, yaani ukisikia kurogwa ndio huku maana hakuna explanation nyingine.

Wakati naingia kulikuwa na foleni, lakini foleni ya kutoka ndio ilikuwa balaa, barabara kama vichochoro vya Vingunguti na mashimo kama tuko torabora, huu ni utani, mimi nawaambia ukweli haya ni matusi ya nguoni kwa wana Dar, hamtaamini kilichopo mule, jaribuni kama mmepotea njia muingie mule. Pale getini sasa kuna kadada kamekomaa kukusanya mapato, hata sijui wanazifanyia nini hizo hela, sijaona hata choo kimoja kwa ajili ya wageni, watu 15,000 wanaopitia hapo kila siku na hakuna choo, this is ridiculous!

Nilitokea kule kwa nyuma njia inayotokezea Shekilango, kule ndio kituko kabisa, huwezi amini ile ndio barabara inayotokea kituo kikubwa kama kile. Hivi ule mpango wa kuhama upo? Mbona mi sielewi?
mkuu stend ya ubungo haiwezi kukarabatiwa kwasababu inatakiwa iondoke
 
choo kipo bwana na sehemu ya kupumzikia/kusubiria abiria pia ipo, labda kama limevunjwa. hapo kwenye mazingira ndio nakubaliana na wewe hasa kama unatafuta basi ukiwa umechelewa ndio kasheshe. utaloa jasho kwa kuzunguka kutafuta basi
 
na omba sana maana mle ndani kuna miti miti hiyo ndio huwa inatumika kama ramani ya kuonyeshea gari unalotaka kupanda,maana utaambiwa aaah sai baba anapak karibu na ule mwembe nenda kwa hivi kidogo,sasa siku wakikata na hiyo miti ndio kimbembe zaid,kikubwa kuku si anataga mayai ya nini watawala waangaike na wapi na jinsi gani anaishi
 
Back
Top Bottom