Nimepata msiba wa mwanangu wa pili, ana miaka 2

Nimepata msiba wa mwanangu wa pili, ana miaka 2

Magical power pole sana kama hizi habari ni za kweli ila kama ni za kuzusha JF inaweza kugeuka shubiri kwako
Binafsi nimepata ukakasi na hii taarifa. Msiba umetokea saa tisa usiku na saa kumi usiku ukaingia JF kupost!
Naamini kwanza umepata taharuki kubwa na kuna mengi ya kufanya kabla ya kutangazia watu msiba utakuwa wapi
Je marehemu aliugua? Kwa muda gani?
Je kafia hospital au nyumbani?
By the way tupe taarifa sahihi tutakushika mkono katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwanao ikithibitika ni kweli
Kuna Watu wanafiwa na dk hiyo hiyo wanapiga ukunga. Huyu kafiwa na kuwakumbuka watu wake humu JF. Turespect hii taarifa yake kwanza mengine yatafata.
 
Mungu akusimamie na akupe ujasiri wa kumsitiri Mtoto wetu! Pole kwako na Shemeji kwa msiba mzito. #WafuHawafiTenaBaliTulioHai Siku moja tutaungana na mwanetu
 
Kila mmoja ana namna yake ya kuomboleza, huyu hii ndiyo namna yake.

Huyu ni ndugu yetu hapa jukwaani, ametupa taarifa na eneo uliko msiba akitegemea faraja kutoka kwetu na sio haya uliyoandika.

Kama huna neno la faraja msibani ni vyema usizungumze kabisa.
Nimeipenda hii

Mfiwa pole sana,Mungu akufanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu
 
Pole sana Mdau! Mungu awafariji wapendwa! Mliopo Morogoro mshiriki jamani.
 
Habar ya usiku huu,

Nimepata msiba wa mtoto wangu wa pili ana miaka 2 amefariki usiku wa saa tisa.

Msiba upo Morogoro mjini forest KILEKA
Polee sana mkuu maelekezo vizuri nihudhurie kwa kijana wetu! Polee sana rafiki mungu akutie nguvu
 
Back
Top Bottom