Nimepata Tender za Nest na TRA wanakataa kunisajili VAT, je nifanyaje?

Mzee,hiyo taasisi waambie tu huna VAT,then watolee tu risiti..mbona normal tunafanya hivyo always.
Hawez mkuu acha kupotosha, labda arudishe ile VAT aliyokusamya kutoka kwa client wake.
Alitakiwa aseme mapema ili alipwe bila VAT. Kama amelipwa anapaswa kupeleka hiyo kodi kwa mama Abdul
 
Nilivyoona mkataba unasema kuna 18% ya vat ndio nikapata shaka kidogo hasa ukizingatia niliyo lipwa ni kiasi chenye vat ndani. Ila nikiona ngoma ngumu itabidi nitoe risiti tu hamna namna!
Changamoto utakayo Kumbana nayo, huyo mteja wako (Nest) lazima atataka Risiti yenye VAT. Ikitokea Umempa risiti haina VAT akibaini anaweza Vunja Mkataba, maana yeye kwenye Mchanganuo wa Malipo yake kwako Kuna 18% ya VAT anakua amekulipa ambayo wewe unatakiwa kupeleka TRA.
 
Kwangu kupeleka sio tatizo, na mimi niko tayari kupeleka! Shida ni kwamba wapokea VAT hawataki kunisajili, je nifanye nini na nimeshalipwa?
 
Hawez mkuu acha kupotosha, labda arudishe ile VAT aliyokusamya kutoka kwa client wake.
Alitakiwa aseme mapema ili alipwe bila VAT. Kama amelipwa anapaswa kupeleka hiyo kodi kwa mama Abdul
Sasa naipelekaje ma hawataki nisajili?πŸ˜‡
 
Hawez mkuu acha kupotosha, labda arudishe ile VAT aliyokusamya kutoka kwa client wake.
Alitakiwa aseme mapema ili alipwe bila VAT. Kama amelipwa anapaswa kupeleka hiyo kodi kwa mama Abdul
Naongea kwa uzoefu mzee,unaweza ukawapa risiti sio ya VAT na unalipwa vizuri sana.
 
Sasa naipelekaje ma hawataki nisajili?πŸ˜‡
ingekua hujalipwa tungesema akulipe bila VAT. Sasa kama ameshakulipa kutompa risiti yenye VAT unaweza hata ukapewa kesi ya Uhujumu Uchumi. We saizi tunza hiyo VAT Yao ufuatilie Taratibu. Siku wakikubananisha unakua unayo kesi inakua ndogo.
 
Reactions: Nus
Naongea kwa uzoefu mzee,unaweza ukawapa risiti sio ya VAT na unalipwa vizuri sana.
Wakakulipa na ile amount ya VAT ikiwa inclusive au exclusive?
Yeye anafanya vipi return zake? Tax invoice ina VAT na imelipwa then ww utoe receipt bila VAT? Huyo Auditor wako yuko wap? Niunganishe nae anifundishe namna ya ku-reconsile hizo hesabu.
Huyo client wako anafanya vipi return zake boss?
 
Biashara Sina Siri mkuu Upepo wa Pesa
tafuta kijana wa stationary mzoefu na muaminifu wa mifumo ya nest akuelezee vizuri atakusaidie .
Mbona issue simple TU πŸ˜‚
 
The way huyo jamaa anajibu inaonekana uelewa wake juu ya mambo ya uhasibu na kodi (VAT in particular) ni mdogo. Watu wengi hufanya blunders kwa mazoea sababu hawajawahi shikwa basi wanaona ni utaratibu sahihi siku akibambwa ndio anaanza kuwaona TRA Tanzania waonevu.

Mtu anaposema VAT inatesa ni wazi hajui maana ya VAT, inaonekana in the first place anaamini VAT unalipa wewe mfanya biashara.
 
Nilivyoona mkataba unasema kuna 18% ya vat ndio nikapata shaka kidogo hasa ukizingatia niliyo lipwa ni kiasi chenye vat ndani. Ila nikiona ngoma ngumu itabidi nitoe risiti tu hamna namna!
Hiyo asilimia inakatwa automatically bank wewe peleka mzigo utaona hayo makato ukipewa hela yako..
 

Hivi kabla hujashinda hiyo tender wenye tender hawakuonyesha au kuweka kigezo hicho cha kuwa na VAT?

Mambo ni mengi sana, TRA Tanzania njooni mtoe msaada na elimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…