Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,772
- 35,770
- Thread starter
-
- #61
Mbona kama sielewi? Una maanisha au unatania? Kwamba VAT uki deposit tu bank inakatwa juu kwa juu?Na kuna asilimia mbili ya kodi ya zuio (Withholding Tax) kama uliuza bidhaa au asilimia 5 kama uliuza huduma, ambayo imeshakatwa wakati unalipwa mwenye hundi yako.
Hivi kabla hujashinda hiyo tender wenye tender hawakuonyesha au kuweka kigezo hicho cha kuwa na VAT?
Mambo ni mengi sana, TRA Tanzania njooni mtoe msaada na elimu.
No, namaanisha kuwa kwenye hayo malipo uliyolipwa imeshakatwa na kodi ya zuio yaani Withholding tax, ambayo itakuja kupunguza corporate tax kama ni kampuni au provisional estimates tax kama ni individual (Withholding Tax ni tax paid in advance) kwenye hesabu za mizania mwisho wa mwaka.Mbona kama sielewi? Una maanisha au unatania? Kwamba VAT uki deposit tu bank inakatwa juu kwa juu?
Hakikisha una mtaji pembeni wa kuendeshea biashara Yako kwasababu unahitaji kusahau malipo kwa mda kwanza.Sasa mkuu una maanisha nini?
Mkuu mbona unanitishaUkitaka kufilisika Fanya KAZI na serikali
Hii ni taasisi ya serikali mkuuWewaambie unatoa risiti bila vat ila punguzo utawarudishia hiyovat iwe faida kwao ,hii ngoma haihitaji hasira wahindi ndivyowanavyotajirika anakupa huduma alafu anakwambia usilipie vat kwahyo unajikuta wewe unakua mtejawake sababu ya gharama yake ipo chini ila ukija kwa wabongo wanakujumlishia Hadi vat means gharama ya bidhaa lazma iwe juu nandipo tunapowakimbia nakwenda kwa wahindi
Bro, ulifanya makosa kusaini mkataba wenye thaman ya mkataba pamoja VAT Wakati unafaham kuwa hujafika kiasi cha kustahili kuwa VAT registered (hapa yaweza tastafsiriwa kama umefanya cheating).Kwa mujibu wa sheria, ili mfanyabiashara asajiliwe kama VAT unatakiwa either ufike makusanyo ua 200m kwa mwaka, au uwe mtoa ushauri wa kitaalamu au uwe na mikataba inayoonesha kazi uliyopata.
Sasa mimi naona nimeangukia hapo kundi la 3 maana japo ni kweli sijafika makusanyo ya 200m kwa mwaka ila nna mikataba ya Nest inayotaka ni supply vitu na mikataba ina VAT.
Nimejaribu kwenda ofisi ya TRA ili kuomba kusajiliwa lakini wamegoma! Je nafanyaje na nimeshalipwa natakiwa kutoa receipt?
Naombeni uzoefu wadau, je kama ulishapitia hii changamoto ulifanyaje kuvuka? Je nitoe recipt YA EFD isiyo na VAT?
way forward?Bro, ulifanya makosa kusaini mkataba wenye thaman ya mkataba pamoja VAT Wakati unafaham kuwa hujafika kiasi cha kustahili kuwa VAT registered (hapa yaweza tastafsiriwa kama umefanya cheating).
Wakati unapopewa mkataba uupitie ndio Wakati wa wewe kukiri kuwa sijawa VAT registered na taasisi hiyo ingerekebisha hiyo thaman ya mkataba kwa kuondoa VAT.
NeST huwa inaweka amount zote kwa kuziwekea VAT....bila kujali kama mzabuni hajafika kiasi cha kustahili kuwa VAT registered ama lah...na inafanya hivyo ili iwe rahisi kufanya ulinganivu wa bei Kati ya mzabuni na mzabuni...ila baadae unapopewa mkataba lazima ukiri kuwa sijasajiliwa ku collect VAT sababu sijafika kiwango cha mauzo kilichowekwa.
Kwa taarifa tu...hata ukitoa receipt ya amount hiyo...Jamaa watajua tu cz huwa wana updates kwa system...so wataona amount ni sawa ila system inakusoma kuwa hujasajiliwa ku collect VAT...hapo ndio itabidi wakuchek kuwa umewaibia.
Rekebisha uhuni uliofanya...warudishie pesa Yao (ambayo ilipaswa kuwa VAT)..toa risiti sahihi, declare kuwa nilisaini mkataba uliokuwa na makosa kwenye VAT na nimekuja kuona mwishoni.way forward?
Uwe na wekend njema mkuu.Rekebisha uhuni uliofanya...
Kama hujasajiliwa vat kuna baadhi ya unaofanya nao biashara hawatakubali maana ni hasara.Nachojua wakati unapata mashine unaulizwa VAT iwepo au isiwepo. Wakulungwa wanajibu isiwepo, haya madhara si ndo kama hayo?
Sidhani kama ni dhambi kisheria kutoa risiti bila VAT, we watolee. Unless mteja wako ndio akatae..
Toa risiti ya ulicholipwa, kwa siku za mbeleni mamlaka itakudai hiyo VAT.
Sidhani kama anaililia, ila biashara anazozifanya inaonekana inabidi asajiliwe,Hiyo VAT unaililia now,ukiioata utatamani utoke,na itakuwa ngumu
Anaweza kujitetea, mamlaka kuna vitu wanavikamilisha.Hao waliomlipa ndo watamsumbua na hiyi vat siyo Tra
Kumbuka unaposajiliwa vat, unakuwa wakala wa Tra kukusanya kodi
Nashukuru kwa kunielewaSidhani kama anaililia, ila biashara anazozifanya inaonekana inabidi asajiliwe,
Vat mziki wake sio mdogo kwa wafanyabiashara wadogo, inahitaji umakini na nidham sana
Sawa sawa mkuu