Nimepata Tsh. Milioni 1.3, naomba ushauri wa aina ya biashara ninayoweza kufanya

FUNGUA STATIONARY............. but zingatia location.....
 
1.3m (huna muda)

Watu wanauza viwanja kila ukipita spika zinatangaza viwanja.

Kanunue PLOT (mashamba) yako ya laki 3 x 4 = 1.2m (hiyo 100k ilobaki itumie kama matumizi)

Tunza mashamba yako au viwanja vyako mpk utakapokuja kupata muda na pesa zaidi kisha itauza yale mashamba yako kwa bei ya juu Utarudsha pesa yako utaunganisha na uliyonayo wakat huo utafanya jambo.

Au

Yote 1.3m tafuta Kiwanja cha 1.3m nunua kiache hapo kitulie kwakua hauna muda nadhani ndio jambo pekee ambalo hutopoteza pesa yako ukilifanya.

Ungekua na MUDA ningekushauri vinginevyo as long as ushasema muda huna wa kuwa katika biashara utayofungua basi wewe Hela imvest yote kwenye KIWANJA.

Kiwanja vina panda bei kila mwaka,usijifikirie eneo hilo ingia mzima.mzima na 1.3m yako mwaka 2027 rudi itafute hio comment yangu, unishukuru.
 
Tafuta dogo umtengeneze genge la matunda
 
Shukrani mkuu, muda ninao ila sio full time ndio maana natamani nijikite katika biashara fulan fulani
 
Wewe sio mfanyabiashara na hichi kitu ndicho kinachowatesa waajiriwa.
Siri ya biashara ni uthubutu basi
Maana kwenye uthubutu ndipo utakapo jifunza vingi
Na kama anaanza tu na anafikiria kuweka mtu basi hana uthubutu unaohitajika.

Hio hela bora afanyie starehe maana hata ikiisha atakua ameyaona ya dunia kuliko kuipoteza kwenye biashara.
 
List ya biashara zote ni fresh tu, kasolo hiyo namba 5.kilimo inachanga moto hasa kama hauna ABC za kilimo. Hizo zingine risk ya kupoteza mtaji sio kubwa ila tafuta wazoefu wakupe maujanja maisha ni atua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…