Nimepata Tsh. Milioni 1.3, naomba ushauri wa aina ya biashara ninayoweza kufanya

Nimepata Tsh. Milioni 1.3, naomba ushauri wa aina ya biashara ninayoweza kufanya

Binafsi ningekushauri ufanye hiyo biashara ya kwanza;

Saloon na kuingiza Movies na nyimbo

Kwanini biashara hii?
~Inahitaji Mtaji kidogo
~Una uhakika wa kuzalisha zaidi ya shilingi 300,000 Kwa Mwezi
~Inahitaji usimamizi kidogo, ukifanikiwa Kufunga CCTV camera utajua Kila shilingi inayoingia
~Ni biashara yenye risk ndogo
~Ni biashara inayotumia fedha kidogo za Uendeshaji(O&M).
Nashukuru vip wazee wa TRA hawasumbui?
 
Toa maelezo utajuaje km unaibiwa na wewe kuja kuangalia ni mwezi mpaka mwezi?
Duka la nafaka, mfano umeagiza nafaka kilo 100 ukija kupiga hesabu unapima ulipo unajua uliouzw ani kiasi flani na bei kiasi flani na hata mafuta lita zinajulikana inshort vitu vya duka la mangi vinakuja kwa idadi na control ni rahisi hata kama hayupo
 
Hapo kazini kwako ndio mahali pazuri pa kuanzia , Anza kutoa mikopo midogo midogo kwa wafanyakazi wenzako isiyozidi 50k , weka mazingira mazuri kwa hr na watu wa accounts namna ya kupata rejesho. Factors nyingine kama majungu kazini watu wasiokopesheka nk ziweke kwenye mzani
Kazini kwetu marufuku biashara, hawezi kubali uwanja wake nafanyia plan B, ni taasisi binafsi. So haiwezekani, licha ya hivyo figisu zitaanza mkuu
 
Ukishapata Fremu ya kufanyia hiyo biashara yako

Nenda Halmashauri ukakate Leseni ya biashara ukiwa na Namba ya Mlipa Kodi(TIN number).

Kisha nenda TRA wakakukadirie Kodi kisha uanze kufanya biashara
Kwani vitambulisho vya ujasiriamali vip?
 
Nina hicho kiasi. Kichwani kwangu nina mawazo haya ya biashara lakini nasita ipi hasa na hizi zote nimezipata humu humu na kulingana na mazingira yangu.

1. Saloon na kuingiza movies na nyimbo.
2. Bodaboda ya million 1.2 dar napata nzuri.
3. Kinglion pikipiki dar ya lak 9. Then lak 4 nibebe balo la nguo za watoto mix nipite nayo vijijini.
4. Duka la mangi hususan biashara ya nafaka mchele, maharage na mafuta ya kula.
5. Niwekeze shambani huu msimu wa kilimo (hii ni option ya mwisho sababu sina skills)

NB: Boda nitampa mtu, salon mtu, maana mi sina muda. Asante karibu kwa ushauri.
Hiyo hela fungulua zipu maana akili huna!
 
Usifanye biashara ambayo hutoweza kui control kwa asilimia 100. Uhusika wako ni muhimu sana hadi pale utapotengeneza mifumo ya kuiendesha ndo unaweza ukamkabidhi mtu.
 
HAPO TAFUTA ODDS 1.32 WEKA ELF 50 KILA SIKU UNAKUA NA UWAKIKA WA KUINGIZA ELF 15 KILA SIKU UKU UKIWA KWNYE SOFA HAPO KWA SHEMEJI YAKO MKUU.
 
Kuna jamaa anaingiza movies, kasema kua aliambiwa alipe 80k kwa mwaka
Ndiyo maana Kuna haja na wewe uende waka-kukadirie

Mnaweza kufanya biashara aina Moja lakini mkapewa Kodi tofauti kutokana na eneo unalofanyia kazi na factors nyingine
 
Duka la nafaka, mfano umeagiza nafaka kilo 100 ukija kupiga hesabu unapima ulipo unajua uliouzw ani kiasi flani na bei kiasi flani na hata mafuta lita zinajulikana inshort vitu vya duka la mangi vinakuja kwa idadi na control ni rahisi hata kama hayupo
Hapa kidooogo umefafanua angalau
 
Nimefanya biashara January to June,nikapata asilimia 75%,kuitunza mpaka January ijayo nimeila yote hapa nilipo nasubiri bakora za wasiojulikana sababu nimeyatimba na January Iko mbali,biashara za msimu ni kipengele
Una familia?
 
Ndiyo maana Kuna haja na wewe uende waka-kukadirie

Mnaweza kufanya biashara aina Moja lakini mkapewa Kodi tofauti kutokana na eneo unalofanyia kazi na factors nyingine
Na vip kitatokea nini Endapo nitafanya bila kuwafata TRA maana jamaa adi Leo anakwepa
 
Back
Top Bottom