Nimepata Tsh. Milioni 1.3, naomba ushauri wa aina ya biashara ninayoweza kufanya

Nimepata Tsh. Milioni 1.3, naomba ushauri wa aina ya biashara ninayoweza kufanya

Kuwekeza na mtanzania ni suicide dive,kama watu wanaiba Hadi Kodi waliyotoa maskini unafikiri kuna zaidi wanaogopa,Hadi kura zinaibwa.Tz kila mtu ana vina saba vuba wizi.
Mimi ni shahidi wa matukio ya partners kupigana na vitu vizito,mtu anaiba anakuacha kama mkiwa,nadhani taifa hili Lina vita ya mtu kwa mtu.
Mfano akaunti ya kampuni inaitaji signatures zenu nyote kama ni partiners na pesa yote inalipwa kwenye akaunti moja mnaibianaje?
 
Nimefanya biashara January to June,nikapata asilimia 75%,kuitunza mpaka January ijayo nimeila yote hapa nilipo nasubiri bakora za wasiojulikana sababu nimeyatimba na January Iko mbali,biashara za msimu ni kipengele
Wakulima wa korosho huko ni neema tu yaan kwa waliootea sasa hivi wanakula pension msimshangae yule mmakonde mgawa range rover 2 kwa mkupuo na kuzitupia kwenye mashimo matatu ya shangazi fulani
 
Hizo za nampa mtu utatupa pesa yako ndgu.

Bora biashara ile ambayo walau una muda nayo, vijana wanaunguza sana mitaji aisee.

Hiyo ya belo la nguo na kusepa nazo bush nimeipenda ila ukiifanya mwenyewe na iyo bonda ikusaidie chaka to chaka na kufata minada.
 
Binafsi ningekushauri ufanye hiyo biashara ya kwanza;

Saloon na kuingiza Movies na nyimbo

Kwanini biashara hii?
~Inahitaji Mtaji kidogo
~Una uhakika wa kuzalisha zaidi ya shilingi 300,000 Kwa Mwezi
~Inahitaji usimamizi kidogo, ukifanikiwa Kufunga CCTV camera utajua Kila shilingi inayoingia
~Ni biashara yenye risk ndogo
~Ni biashara inayotumia fedha kidogo za Uendeshaji(O&M).
 
Hizo za nampa mtu utatupa pesa yako ndgu.

Bora biashara ile ambayo walau una muda nayo, vijana wanaunguza sana mitaji aisee.

Hiyo ya belo la nguo na kusepa nazo bush nimeipenda ila ukiifanya mwenyewe na iyo bonda ikusaidie chaka to chaka na kufata minada.
Hii ya nguo nitaifanya mwenyewe kwa mikono yangu mkuu
 
Hizo za nampa mtu utatupa pesa yako ndgu.

Bora biashara ile ambayo walau una muda nayo, vijana wanaunguza sana mitaji aisee.

Hiyo ya belo la nguo na kusepa nazo bush nimeipenda ila ukiifanya mwenyewe na iyo bonda ikusaidie chaka to chaka na kufata minada.
Hivi utaratibu wa kufuata minada ukoje?
 
Nina hicho kiasi. Kichwani kwangu nina mawazo haya ya biashara lakini nasita ipi hasa na hizi zote nimezipata humu humu na kulingana na mazingira yangu.

1. Saloon na kuingiza movies na nyimbo.
2. Bodaboda ya million 1.2 dar napata nzuri.
3. Kinglion pikipiki dar ya lak 9. Then lak 4 nibebe balo la nguo za watoto mix nipite nayo vijijini.
4. Duka la mangi hususan biashara ya nafaka mchele, maharage na mafuta ya kula.
5. Niwekeze shambani huu msimu wa kilimo (hii ni option ya mwisho sababu sina skills)

NB: Boda nitampa mtu, salon mtu, maana mi sina muda. Asante karibu kwa ushauri.
Hapo kazini kwako ndio mahali pazuri pa kuanzia , Anza kutoa mikopo midogo midogo kwa wafanyakazi wenzako isiyozidi 50k , weka mazingira mazuri kwa hr na watu wa accounts namna ya kupata rejesho. Factors nyingine kama majungu kazini watu wasiokopesheka nk ziweke kwenye mzani
 
Back
Top Bottom