Unathibitisho upi kwamba pumzi ilitengenezwa?
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimetengenezwa, Hata huyo Mungu lazima awe ametengenezwa.
Na kama huyo Mungu yupo tu bila kutengenezwa, Hata Pumzi ipo tu bila kutengenezwa.
Mungu huyo Alishindwaje kuumba dunia isiyo na mateso, magonjwa, vilema na njaa?
Kama Mungu aliumba kila kitu kwa ukamilifu. Magonjwa, mateso, njaa na vilema yalikujaje?
Kama magonjwa, mateso na njaa yaliweza kuja duniani, ilihali Mungu huyo aliumba dunia kwa ukamilifu. Huoni kwamba kazi yake ya uumbaji ina dosari na kasoro?
Huoni kwamba Mungu huyo ni Mdhaifu sana kwa kushindwa kuumba Dunia yenye ukamilifu milele yote?
Uwepo wa vipofu ni uthibitisho tosha kwamba kazi ya uumbaji ya huyo Mungu ina dosari na kasoro.
Ndio maana kuna watu wanazaliwa vipofu bila wao kupenda.