Canada uta enjoy ukiwa na watoto, maana jamaa wana kodi ndefu sana, ukiwa na watoto unaweza usihisi maumivu sababu ya universal health care system yao, pia elimu yao.
Huduma zao za elimu na afya ni standard nchi nzima na ni 'bure' (hakuna cha bure ndiyo maana ya ile kodi ndefu).
Unaenda hospital, unahudumiwa 'bure', mziki upo kwenye parking na fine zao, unaweza ukahisi ni gharama ya kufanyiwa operation ya kubadirishwa kichwa😀.
Ukizamia hakuna namna utaweza hata kuita kulipia uber, or chakula, yaani ukizamia ujue upo nje ya system hautapata huduma yoyote ile wala hawabishani na wew. Ndiyo maana walimwengu wanapagwaya, wanabaki wanajazana New York na Seattle.
Wa Seattle anakua anaisikia tu Vancouver kuwa ipo just across the border huku wa Minnesota, Michigan, Ohio, Pennsylvania, na New York wanakua wanaichungulia tu Ontarior lakini kamwe hawatamani kuvuka ili kwenda,