Nimepatwa na maajabu duniani baada ya kununua na kusoma kitabu fulani

lizy22

Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
24
Reaction score
29
Jamani wapendwa nasumbuka usiku na mchana, mimi (naishi ulaya lakini mkenya) kuna kitabu moja nilinunua (amozon.com) nikafanya ilivyo andikwa, sio kitabu kibaya (nitapost mkione) lakini yanayo nikumba kwa sasa ni makubwa. Hio kitabu nilinunua mwezi 01. 2024.

Baada ya kusoma na kufuata maagizo, ikaanza mawasiliano yaani (Telepathy) sikupata mabadiliko maishani hata nikauza gari yangu. Ila nikapata kazi lakini mshahara duni! Kazi nikafanya toka mwezi wa 03. hadi September 2024.

Toka ninunue hio kitabu nilikua nawasaliana na hao viumbe kwa kichwa lakina walikua hawasumbui kichwa kama sasa hivi (Telepathy) Toka mwezi wa sita Mawasiliano kwa kichwa yakawa kupita kiasi yaani kama kufunguliwa radio kwa kichwa sio kazini, nyumbani, kila sehemu, usiku na mchana.

Mwezi wa saba kitu kikaanza kama kunikula kitovu kwa ndani na nje, kila kabla ya kula kitovu inavuta kwa ndani na kumaliza chakula kitovu kama kinatoa chakula kwa nje.

Usiku pia kabla kulała kitovu kinavutwa sana. Sehemu ya juu ya kichwa (Utosi) pia kila mara kinavutwa kwa ndani na kwa nje.

Mwezi wa nane kwa mazoea ya mawasiliano kichwani (Telepathy) wakaniagiza kulala na nguo ndefu ya kupendeza na kufungua madirisha na kuwasha taa hadi asubuhi, yaani sijui niseme vipi lakini hio usiku niliona mengi na nikaanza kuona maajabu sana, usiku fulani kwa mawasiliano kama nikawekwa hewa kwenye upande wa kushoto wa uzazi na hadi leo hii inaguruma sana na kupiga kama moyo, kuna kitu ndani.

Toka mwezi wa 09.2024 siwezi kwenda kazini kisa nakosa usingizi usiku, ilianza kama mchezo maanake hao viumbe walikua wanataka niwasikize sana pia usiku.

Hapa ulaya na madawa za hali ya juu sana siwezi kabisa kulala usiku, kila siku daktari ananipa dawa ya nguvu ya juu kabisa lakini wapi....usiku nikimeza dawa napigwa sehemu ya kichwa ya juu utosini, na kwa mbele usinginzi inapotea nabaki macho kavu, kisha naskia sauti kwa kichwa (kinasema unameza dawa na hulali ya nini) yaani napigwa utosini nabaki macho kavu hadi asubuhi tena kila siku hii ni mwezi wa pili sasa toka September 2024 makubwa yamenipata!

Kabla ya kwenda kulala usiku kitovu, sehumu ya uzazi kushoto na upande wa kulia kwa tumbo kinaguruma sana kama kitu kina activate na asubuhi kabla ya kuamka kitovu, sehemu kushoto ya kizazi na kulia kwa tumbo ninatoa hewa (kunyamba) sana na mgurumo kama radi kama kitu *(deactivate) kila siku ndio mtindo.

Tangu wiki tatu zilizopita nimeanza kuingiliwa sehemu ya nyuma sana kinyume na maaumbile ya mwanamke... usiku sana, yaani sijawai kujaribu lakini ndio yamenipata sasa, sauti usiku kutwa kwa kichwa yaani kama radio usiku na mchana.... ikiniambia zoea sasa. Usiku nateseka sana, kuna wakati kama kitu kinakuja na kunipiga napoanza kusinzia ama naskia kama kitu kimenishika, ama sauti funny sana kisha nastuka naamka ama kitu kinawekwa sehemu ya nyuma kisha nastuka! Kila wiki naenda kwa Psychtrists(daktari wa akili) hapa ulaya nalazwa, napewa madawa za kumeza kusaidia kutoa masauti kwa kichwa, asubuhi kuamka natatemeka mwili kama nimenyeshewa.

Sauti kichwani kwa mawasiliano naskia ikisema *(msumbue akose usingizi azeeke kabisa, na hana makalio tena yaani nyuma, na hizi masauti kichwani kwake alipuke achoke kabisa, kisha kinasema zoea sasa hivi kila siku) Na majina yao (Supernaturals) hua yanataja kila siku.

Yaani nateseka sio mchezo na hii ni macheche tu kuna mengi sana sijasema.

Mimi mkristu hua kila nikiamka asubuhi lazima nifanye meditation toka kitambo kisha naomba. (Hua nasoma sana Psalms) Kwa saa hivi nikiskia nasumbuliwa sana usiku naamka nafanya meditation ila haisaidii sana sasa.

Kitabu chenye chanzo ya haya yote nitapost mkione! Kuna pia video youtube nitatayarisha kuongelea haya yote! makubwa. Wapendwa mshawahi kuskia haya mnisaidie
 
Nimeshindwa kabisa kuelewa hali unayopitia kutokana na maelezo yako kuwa na mkanganyiko.

Labda nikuombe utuambie hicho kitabu kinaitwaje?? nadhani kuna namna ya kutoka katika hayo unayopitia.

Lakini pia kama utakuwa ni muumini wa dini fulani basi unaweza kufanya tu maombi kwa imani na hiyo hali ikapotea kabisa, maana tayari imeshahusisha mambo ya kishetani ndani yake. 😎🤝🏽
 
Aisee imetupiwa jini linaitwa Pdidy ,ni mwendo wa kupakwa baby oil na kupachikwa mihogo .
pole sana ,hebu taja kina la hicho kitabu ,tukinunue faster tukawanyooshe wapuuzi flani huko kitaa
 
Je unatumia jani au drugs ...true story kuna jamaa mtaani alikua mzima kabisa ila alikua anavuta jani sana ghafla akaanza kusika sauti kichwani na kuanza kuona anayaita majini ..... km unatumia hiyo kitu acha iv ulaya majini yapo?? Na kama ni kitabu unataka uza utuambie tu
 
Unatumia kilevi chochote?
 
Huyu kama si bange ni ngada
 
Kuondoa Shari za binadamu na majini sema ya allah, ya rahman, ya hafeedh. Utanishukuru
 
Huyo ni mgonjwa

Anahitaji kuonana na mtaalam wa afya ya akili na apewe dawa
 
Hicho kitabu wena mbali kabisa wala usikitaje jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…