Nimepewa lift nikiwa na mtoto wangu, roho imeniuma sana

Wewe ndiyo usome vizuri; kaandika raum nyekundu. Kama kiswahili hadi leo hujakielewa, bora urudi kwenu burundi
Sasa hata kusoma huwezi , unachangia mada nini?? RAUM na Rumion, unaona ni kitu kimoja?? ....
 
Kila la kheri mleta mada, maisha mapambano! 😄

Usikute ana changamoto zake zingine zaidi yako pia.!
 
Mimi nikajua roho imekuuma kwa kuogopa jamaa mwenye Raum angekuteka wewe na huyo madogo, kumbe wivu wa jamaa kumiliki ki-Raum ulikutesa.
Raum ni sh. 8-9m tu
Kamanda! Hiyo bei Kama used ya hapa bongo

Ila zile used za japan raum inaenda 14 million
 
kwakwelii ili watoto wetu waache kusema ningezaliwa kwenye familia Ile au ningekua na baba Kam yulee..

tunapaswaa tupambne na MUNGU atusaidiee
 
Ni vizuri kuwa na wivu wa maendeleo

Ila ukijihisi kila kitu huna utakuwa mwizi..
Kila mtu na vipaumbele vyake

We umejenga gari huna, mwenye gari kapanga
 
Wachawi watu wabaya! Unalogwa mpaka kupata gari ni mbinde! Wengine hata kununua TV! Radio! Friji! Freezer! Jiko! Smartphone! Nk, mpaka uombe na kufunga!
 
Nashangaa sana hii tabia ya kumuamini mtu usiemjua anapokupa lift au unaomba lift
Una mtoto halafu unapanda vya bure
Hapo niemeweka risk zaidi maana hata peke yako sio salama kabisa kupanda vya watu

Kama ni psychopath na anakuuwa
Wengine ndio fantasy zao hizo
Mtoto anaekuona shujaa kwa sasa na ukamdanganya
Hivi kama just kama lingetokea mwanao akaachiwa bado ungekua hero wake

Acheni tabia za kupanda vya bure wakati hela mnazo
 
Kwenye dunia ya sasa ilivyopinduka, msaada unaweza kuleta balaa. Ila usikate tamaa, kama kitu unakipenda na nia ipo. Utakipata, utupe mrejesho tu. Mambo huwa yanabadilika sekunde moja, unakuwa mwingine le millionea...
 
Utapata inshallah mm hata baiskeli Sina ila Mungu ni mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…