Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Wapigie na wewe waulize wakati nyama zinaoza mpaka natupa mbona hamkuja kunisaidia?,halafu waambie hivi wajikusanye wajipige kifuani Mara tatu waseme "sisi ni kusanyiko la wapumbavu " halafu kata simu.

Ila usisahau kutoa taarifa polisi,pili usikae kizembe,tatu jiandae kwa vita ya kiroho.
 
Hawa wahuni ndio huwa wanapandisha bei mwezi wa Ramadhani na sikukuu zinginei ili wapige faida kubwa
 
Sema bei ya kitimoto kwa walalahoi inavunja moyo hii Yako imekaa poa sometimes unaamua kupata kidogo ila mzunguko unakuwa mkali na jina linajengeka
Hapo toa taarifa polisi na maeneo husika
Bei usipandishe ila toa taarifa kwa baadhi ya watu muhimu eneo lenu na uombe ushauri kwao
Wafate tena mchana Kisha waambie hutafanya biashara kwa matakwa yao Bali Yako mwenyewe Kisha waambie kifo kipo wakijaribu wewe unamaliza
Chunga biashara Yako maana wataanza kuweka uvumi wa kuchafua biashara Yako hakikisha mazingira ni rafiki sana
 
Mkuu pole kwa yote yalokusibu.
Kikubwa karipoti kituo cha polisi na baada ya hapo uanze kuchukua tahadhari zote za kiusalama. Ikiwa n kwako na familia yako
PIa kabidhi maisha yako kwa Muumba maana yeye ndiye awezaye kuua roho ila mwana wa adamu hawezi
 
Uza 11,000

Ila ongeza ubora na ufundi, pishi liwe unique, huduma iwe fasta, customer care nzuril

Wateja wakishakuzoea unapandisha 12,000
 
Shusha tena bei iwe 7000,,then subiri watachukua hatua gani,, funga cctv kwako, anaweza kukuchoma moto,, usitembee gizani, nunua bastora na uwe unatembea nayo kiunoni ikining'inia hata mchana,
Watembelee mmoja mmoja usiku wa manane na uwape onyo kali👌
 
Hata mimi ningekufata, hawa watu humu wanakuvimbisha kichwa ila ukweli ni kuwa unaharibu biashara za watu na watakufanya kitu mbaya ukizidi kuwa kichwa ngumu.
Pandisha bei hadi 11500 au 11000 utaeleweka.
 
Pole sana! Badilisha mfumo uza bei kama yao elf 12 lakin lile punguzo la elfu nne huwe unawaongeza nyama wateja wako. Pia toa report police
...Hueleweki ! Uza Bei wanayotaka Wao ya Alfu 12, halafu Bado umuongeze marja nyama ?
Utafanya Biashara kweli ??? [emoji848][emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…