Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Kuna kijiji kimoja niliwah kukuta kuna maduka mawili,hao majamaa wenye hayo maduka ni mamafia balaa,wengi wanaokuja kuanzisha hapo biashara kama hyo wanapigwa mikwara na kuibiwa pia wanabomoa usiku na ukija na bei ndogo ndogo kila siku wanakuwa wanakufata

Kwenye biashara lazima wafanyabiashara muwe kitu kimoja kumkandamiza mnyonge
Sio lzm kuwa kitu kimoja mm nilipo nauza Gas Oryx kg 15 ni 55000 wakat wenzangu 57,58 wakat ndogo nauza 23,000 wengine 24,25 .
 
Hao jirani zako hawajui kutumia fursa na mbinu za biashara kwanini wasingeungana alafu wakawa wanakuja kununua hizo nguruwe kwako kwa bei hiyo ya Tsh 8,000/= alafu wakawa wanauza kwao kwa bei hiyo hiyo wanayouza ya Tsh 12,000/= ?, Wajanga sana hao wangekuwa na akili wangekutumia wewe kama fursa na siyo kuwaza kukutishia maisha.
 
Kuna wapumbavu hii nchi mtaka kuifanya ya Baba yenu, kwanini umpangie mtu bei ya kuuza? Kama anauza bei ya hasara automatically hatachukua round biashara itakufa yenyewe, huku shinyanga na geita miaka ya nyuma jamaa wa kaskazini waliiteka biashara ukanda huu Kwa bei za kuumiza Ila tangu mnyantuzu kaijua biashara jamaa wote wamechora. Wote mnaotaka na kulazimisha kufix bei ni wapuuzi na wapumbavu wakubwa.
Nchi ni ya wenye pesa, nguvu na mamlaka.
 
Heri ya Pasaka!

Eneo nilipo kuna wafanyabishara 5 wanauza nyama ya nguruwe kilo 1 wanauza elfu 12, ilo eneo mimi ni mgeni nina miezi 4 tu Ila punde baada ya kufungua banda langu nilikuwa nauza bei sawa na wenzangu sh 12k lakini nilikuwa siuzi kabisa naweza kukaa mpaka siku 4 siuzi kabisa ikafikia hatua nyama ikawa tasteless napata hasara nyama natupa.

Baadae nikapiga hesabu nikasema ngoja nishushe bei niuze KG 1 kwa elfu 8, nikabandika tangazo kuwa nyama ni elfu 8 tu Mambo yakawa c haba nikaanza kupata wateja wakutosha tu kwa wiki nikawa nachinja mpaka nguruwe 3.

Juzi kijana wangu niliyemuajiri wakamfata wakamwambia dogo unatuharibia biashara tafadhali tunaomba uuze bei ile ile ya mwanzo 12k,dogo akasema mimi sio boss ngoja niwape namba za boss; walivyopata namba zangu wakanipandia hewani wakaanza kuniambia nishushe bei nawaharibia biashara na hiyo ndio biashara inayoendesha maisha yao na familia yao.

Leo asubuhi wamenifata nyumbani sijajua ni nani aliyewaelekeza wakanipiga mkwara mzito lazima roho yangu iende kuzimu.

Nipeni ushauri wananzengo, nifanyaje?Tusijekufika pabaya maana wanaoneka hawatanii.
Price skimming
 
Hii Ni dunia huru ya kibepari. Yaani hao jamaa wamekuwa wa kufunguliwa mabucha Kama Mia na Bei iwe 5k kwa kilo.

Kila mtu huwa anapenda ubabe ili awe mtawala.
Mfano wanasiasa wanatumia nyumbu wenzetu kuwalinda wao ili watunyonye wote na viongozi wa dini wanatumia uwoga wa wanadamu na kifo wanawatala na kuwaamrisha kutoa sadaka ili wapate mibaraka
 
Biashara zote ndio ziko hivyo, ndio maana kunakuwa na bei elekezi; atakayeenda tofauti na makubaliano ndio wanakutana na changamoto kama zako.
Kwa ushauri, kama una uwezo wa kuuza chini ya bei zao, jaribu kujadiliana nao wewe ndio uwe 'major supplier' wao, uwe unawauzia wao nyama kwa bei ya jumla.​
 
Heri ya Pasaka!

Eneo nilipo kuna wafanyabishara 5 wanauza nyama ya nguruwe kilo 1 wanauza elfu 12, ilo eneo mimi ni mgeni nina miezi 4 tu Ila punde baada ya kufungua banda langu nilikuwa nauza bei sawa na wenzangu sh 12k lakini nilikuwa siuzi kabisa naweza kukaa mpaka siku 4 siuzi kabisa ikafikia hatua nyama ikawa tasteless napata hasara nyama natupa.

Baadae nikapiga hesabu nikasema ngoja nishushe bei niuze KG 1 kwa elfu 8, nikabandika tangazo kuwa nyama ni elfu 8 tu Mambo yakawa c haba nikaanza kupata wateja wakutosha tu kwa wiki nikawa nachinja mpaka nguruwe 3.

Juzi kijana wangu niliyemuajiri wakamfata wakamwambia dogo unatuharibia biashara tafadhali tunaomba uuze bei ile ile ya mwanzo 12k,dogo akasema mimi sio boss ngoja niwape namba za boss; walivyopata namba zangu wakanipandia hewani wakaanza kuniambia nishushe bei nawaharibia biashara na hiyo ndio biashara inayoendesha maisha yao na familia yao.

Leo asubuhi wamenifata nyumbani sijajua ni nani aliyewaelekeza wakanipiga mkwara mzito lazima roho yangu iende kuzimu.

Nipeni ushauri wananzengo, nifanyaje?Tusijekufika pabaya maana wanaoneka hawatanii.
Mkuu
Umeshapata RB yao hao jamaa zako?

Nenda central kawashtaki maana hiyo ni serious threat
 
Nakodisha bastola mkuu
JamiiForums-940899099.jpg
 
Biashara zote ndio ziko hivyo, ndio maana kunakuwa na bei elekezi; atakayeenda tofauti na makubaliano ndio wanakutana na changamoto kama zako.
Kwa ushauri, kama una uwezo wa kuuza chini ya bei zao, jaribu kujadiliana nao wewe ndio uwe 'major supplier' wao, uwe unawauzia wao nyama kwa bei ya jumla.​
Nani kakudanganya biashara zote ndo zilivyo? Hizo ni pigo za washamba wachache kupangiana bei, soko ndo huamua bei na kuna factors kadha wa kadha zinazoweza kufanya mtu auze either juu au chini ya bei ya soko na huwa hakuna kulazimishana.
 
Tatizo wewe bado uko kwenye 'theory' za supply vs demand; uhalisia sio hivyo, ndio maana kuna taasisi au umoja unao 'regulate' bei; tofauti na hivyo mtoa mada akichukua ushauri wako anaweza kujikuta yuko mbinguni, kama alivyoonywa.​
 
Back
Top Bottom